Elections 2010 Akaya Kikwete alipodai ilibidi wafanye kazi kubwa ya ziada kushinda uchaguzi huu ulimwelewaje?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,174
Kauli ya JK jana kwenye hotuba ya kuapishwa kwake ambapo alikiri upinzani uliwasumbua na ilibidi wajipange upya na kufanya kazi ya ziada ili kushinda uchaguzi huu ulimwelewaje?

Mimi tafsiri yangu ya haraka haraka iliniongoza kuamini JK alikuwa anakiri kuwa nguvu za ziada ni uchakachuaji wa kura zetu na hivyo kurudi madarakani isivyo halali na kinyume na sheria.......

Vile vile JK aliposema ilibidi wajipange upya niliamini moja kwa moja ni vikao vingi vya siri kama kile ambacho barua yake ya kule Mwanza ilikamatwa ya kupanga kuiba kura na ambayo wengi wa walioshiriki kikao hicho wamekuwa wakijigongagonga katika utetezi wao kuwa hawakushiriki hicho kikao.......................ni JK tu ambaye hadi leo yupo kimya juu ya ushiriki wake wa hicho kikao ikiashiria ya kuwa anakubali alishiriki.........................kimya maanake ni ndiyo.............tu................hakuna utetezi mwingine.....................


Sijui nanyi mna tafsiri zipi juu ya kauli hizi za huyu Mheshimiwa ambaye mimi ninaamini ameingia madarakani kwa mlango wa pembeni siyo ule wa kisheria hata kidogo.............
 
Kama mnakumbuka kuna mchangiaji mmoja aliwahi kutuhahablisha hapa kuwa Jakaya alikuwa amefanya safari ya ghafla na alikuwa Mwanza katika bilika pilika za uchaguzi!! Ndio wakati huo huo hicho kikao cha siri kilipofanyika!!
 
mimi ninamshangaa huyu "jini-ass Braini" hataki kuyaona haya, RUTA, ninaunga mkono hoya kwa 1979%. Ni vigumu kutuambia leo dr. Slaa kapata kuta 2.3ml, wakati kipindi cha kuomba UDHAMINI TU wa kugombea Urais alipata wadhamini 1.87ml (hawa ni LAZIMAAAAAAAAAAA wawe wapiga kura wenye shahada) kwa mikoa KUMI TU!!, vipi kuhusu mikoa mingine ambayo hakutembelea, ambazo baadae tulikuja gundua kuwa ni ngome imara za CHADEMA?? hata kama wadhamini hawakujitokeza kupiga kura si zaidi ya 30% ya wadhamini?? in this case -30% ya 1.87ml ni around 0.58ml ambao waliopiga kura ni almost 1.3ml ya WADHAMNI PEKEE?? vipi KUHUSU MIKOA iliyobaki na mikoa mingine ambayo ni ngome ya CHADEMA, kwamba chadema imepata kura 1ml tu (TAFAKARI)?. sitaki kutukana maana naiheshimu hii forum, kwa maendeleo ya hoja , ila ningekuwa mtaani @>:#KK$K#::#PPK<#&$*^&@* ZAO
NAUNGA MKONO HOJA
 
Ni vyema JK akakiri mapungufu yote yaliyojitokeza na halafu akakaa na Dr. Slaa kuja na mikakati ya kuboresha utawala bora ya kuhakikisha chaguzi zijazo zinakuwa ni za huru na haki badala ya hivi sasa ambapo CCM ndiyo imejivika joho la kutuchaguliwa viongozi wetu ambao hatuwahitaji
 
JK ni vyema akajitokeza na kuteleza ukweli alifanya nini hadi akwa Raisi wa hiki kipindi cha pili......................Only the truth will set him free..................................
 
Nasema Igweeeee kwenye hoja, uchakachuaji umefanyika sana hili hata asiyetaka kukubali kinywani analitambua moyoni mwakeikiwa ni pamoja na mheshimiwa JK. Ila yana mwisho, 2015 will not be the same again. :nono:
 
kwa mtazamo wngu kazi kubwa waliyoifanya kurudi madarakani ni ujambazi wa kuiba kura za wananchi!
 
Makamba kasema 2015 watanzania watasahu yote maovu ya CCM na watawapa kura tu!, kama sivyo wizi mtindo mmoja. Tume huru ndio dawa ya hii kansa ya CCM ya wizi
 
Back
Top Bottom