Ajira zilizoko mbioni kutoweka

Ajira zilizoko mbioni kutoweka

sandpiper

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2018
Posts
209
Reaction score
186
Watu wengi wanapendelea watoto wao waje kufanya kazi ambazo wao wanafanya . Lakini miaka inayokuja baadhi ya ajira zitakuwa hazipo tena badala zitafanywa na maroboti au mashine. Hizi ni baadhi ya ajira ambazo ziko mbioni kutoweka:

Bank teller
Mara nyingi ukienda benki kuweka au kutoa pesa unahudumiwa na mtu , ni miaka michache ijayo mashine zitafanya hiyo kazi kwa ufanisi mkubwa na kwa weledi. Pia watakuwa kwenye counter zao wakati wote.

Dreva tax
Uber imeweka kazi ya dreva taxi hati lakini ni muda tu pale ambapo gari zisizohitaji dreva kuanza kutumika . Nchi kama Singapore zimeshaanza majaribio na ujenzi wa barabara kwa ajili hiyo.

Wauza magazeti
Hawa ni wa kuwahesabia siku , polepole kwa sasa wanaanza kupotea

Wakulima.
Kazi ngumu zitaweza kufanywa na mashine na maroboti yenye kutumia akili bandia kwa ufanisi

Actor wa movies
Hawa bado kidogo actors wa kutengeneza na computer wameonyesha mafanikio makubwa . Mfano Itakuwa hata kuona movie mpya ya marehemu Kanumba ikawa si kitu cha ajabu .Mfano Carrier Fisher alivyoonekana kama Leia kwenye STAR WAR.

Mashine na Maroboti yataweza kufanya kazi kwa ufanisi basi inaweza ikawa sio kitu kibaya . Ina maana maendeleo yatakuja kwa haraka huku muda wa kazi ukiwa mchache
 
Kwa upande wa Bank teller wana majukumu mengi zaidi ya Yale ya kuweka na kutoa pesa mkuu, kwaio wataendelea kuwepo tu.
 
Meet Asia and Automation.
Hawa ndio watareplace ajira nyingi sana.
 
Hata kazi ya ubunge pia itaanza kufanywa na robots
 
Back
Top Bottom