wiseboy.
JF-Expert Member
- Aug 11, 2014
- 2,932
- 4,534
Viongozi wa serikali wakisoma heading hii ni lazima washikwe hasira,kwao ni uongo na uchochezi,hata kwenye ukweli usiojificha wao huwa ni uchochezi tu.
Idadi kubwa ya vijana wa Tanzania hawana ajira,hata wanaomaliza vyuo kupata ajira imekuwa ni sawa na kupata dhahabu.
Vijana wafanyeje? Hawawezi kuiba,wameamua kucheza Kamari kwa nguvu zao zote,ni mwendo wa Ku bet mpira,BIKO ,Tatumzuka na mengineyo.
Kauli rahisi kutamkwa na viongozi wetu ni "kama huna kazi nenda kalime".
Hivi utalima bila mtaji? Kukodi shamba ni pesa,kununua mbegu,mbolea na kutunza shamba ni pesa,yaani unaambiwa ukalime as if kwenye kilimo ndo sehemu rahisi na suluhisho kwa mtu asiye na ajira.
Serikali haina strategies za kuwakomboa vijana kiuchumi,nimemshuhudia rafiki Yangu mmoja ambaye hana ajira alikuwa akisema,Mungu atamsaidia kupitia hata Kamari, nikampuuza,alijenga mazoea ya kucheza Kamari kwa pesa za kuombeleza ,na kweli Mungu si mwanadamu,jamaa akapiga zaidi ya mil 20,akaondoka mjini na kukimbilia vijijini kwenye kilimo,kwa sasa yupo vizuri hataki tena kusikia neno ajira.
Serikali ingeanzisha Benk maalumu ya vijana ambayo itakuwa ikitoa mikopo yenye masharti nafuu ili kuwakwamua vijana kiuchumi na kuwaepusha na kujihusisha na uhalifu kwa Sababu ya maisha magumu,
.
Tatizo Tanzania imegeuka kubwa taifa la siasa kwa kila kitu,hata maslahi mapana ya taifa watu wanaleta siasa.
Nawaambieni vijana ndo taifa thabiti,kuliacha bila chanzo cha mapato ni hatari kwa usalama wa nchi.
Yaani kila kona mjini ni Kamari kwa kwenda mbele,na Kamari ni Kamari tu,tuendako kama serikali haitashtuka tutakuwa taifa la Kamari tu.