Ajira Serikalini: Rais Magufuli, mwezi mmoja na nusu umekatika kama ulivyoahidi

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,400
Heshima kwako Rais Magufuli....

Tafadhali tunaomba tukukumbushe kuwa muda usiozidi miezi miwili (mwezi moja na nusu) za kufungulia ajira za serikali kama ulivyoahidi umeisha jana. Sasa tunaomba ufungulie ajira. Vijana wanahitaji ajira...

Kwa kuwa serikali yako ni sikivu, basi ni mategemeo yetu kuanzia wiki hii tutaanza kuona matangazo ya ajira katika magazeti mbalimbali...

#Tunaomba sana sana!
 
Kijana tulia, raissss hakumbushwi na hata akikumbushwa hadi aridhie

Mkuu Rais ni wetu watanzania.... Tunapojadili mambo ya msingi kaeni pembeni... Vijana wanahaha huku mtaani wanataka ajira..

Punguzeni ukada. Mimi ni kada tena nafaidi ukada kuliko hata wewe. Ila hili suala linagusa wadofo zetu na ndugu zetu. Acheni unazi..
 
Ajira mbona zina tolewa mbona ma dc ,das,na wakurugenzi wamepata ajira ww kama haupo...ujue no ajira nyingine.... kalime uwe kama shetani
 
Mpaka sasa serikali imefanya vyema katika hilo... Nafkiri liwe zoezi endelevu ambalo lisizuie ajira mpya kutangazwa kwani watumishi hewa lishafanikiwa kwa kiwango cha juu
Sasa hivi wameanza kuangalia Muundo wa Serikali ili Kubaini na Kuunganisha Taasisi zenye Majukumu yanayofanana. Na likimalizika hilo litaanza lingine jipyaaaa!
 
Heshima kwako Rais Magufuli....

Tafadhali tunaomba tukukumbushe kuwa muda usiozidi miezi miwili (mwezi moja na nusu) za kufungulia ajira za serikali kama ulivyoahidi umeisha jana. Sasa tunaomba ufungulie ajira. Vijana wanahitaji ajira...

Kwa kuwa serikali yako ni sikivu, basi ni mategemeo yetu kuanzia wiki hii tutaanza kuona matangazo ya ajira katika magazeti mbalimbali...

#Tunaomba sana sana!
Kumuamini mwanachama YEYOTE wa CCM ni sawa kuamini kufufuka kwa maiti jambo ambalo haliwezekani
 
Back
Top Bottom