Ajira kwa misingi ya vyama italivuruga Taifa

Kule Zanzibar kulishamiliza kuvurugika zamani. Kadi ya CCM ndio muhimu kuliko Certificate ya Degree
 
Ukweli wake ni upi? Watendaji wa kata walioajiriwa mwezi wa 8, interview wamefanyia wapi?

Matabaka yameshaanza kutengenezwa ndani ya nchi...
Wataneemeka wale wanao wanaoendana kisiasa, kikabila na kiundugu kinyume kabisa na mahitaji,sifa na uwezo..
 
Mm mwenyewe nilifanya intaview ya civil engineering office ya manispaa huku kwetu Zanzibar tunaita baraza La mji walihitaji MTU aliyena digree ya civil engineering ili wapate mtu wa kuwarekebishia mipango miji pamoja na siter plan tulienda kufanya inteview ile ktk shule ya Fidel Castro iliyopo vitongoji Chake Chake tulikuwa watu watatu mm na wenzangu wawili wote tulikua wanaume.

Kwa bahati mzuri ile nafasi nikabahatika kupita jina langu na jina lango likaenda ktk office flani nyeti na jina lile wakaagizwa vijana watatu ktk office ile wanifuatilie nyendo zangu ndio wakafika mpaka kwa sheha kwajina huko bongo munamwita mwenyekiti wa mtaa basi walupo fika walisalimiana vizuri na wakamuliza yule sheha jee hili jina hili unalijua naakapewa na picha ya passport size sheha akajibu nalijua na akauliza ananini akaambiwa huyu ameomba ajira na amefanikiwa lkn tumekuja kwako utupe sifa zake sheha akawambia wale vijana huyu MTU hafai kumpa kazi na wala hafai kufanya kazi ktk serekali hii mmoja wa wale vijana akauliza kwanini sheha akajibu huyu kijana wazazi wake ni wa vyama pinzani na yy mwenyewe ni mpinzani kwahiyo bora hata mutafute MTU kutoka sehemu yoyote lkn huyu hafai

Basi jamaa wakaenda zao na wakapeleka maelezo Yale Yale waliyopewa .sasa kuna msemo ambao wahenga husema kwenye wabaya na mwema hakosi siku hiyo nimo ktk uwanja wa gombani uliopo chake chake Pemba ilikua nikiangalia mechi kati ya timu ya jamhuri na jangombe boys kuna yule kijana aliyetoka ktk office nyeti akaja kuniambia umemkosea nini sheha wako nikamwambia mm sija mkosea akanimbia mbona anakuchukia na anazizuia rizki zako nikamwambia mm sina ugomvi mbona akaniambia basi kama ww huna ugomvinae lkn jina lako ilikua lishapita lk. Sheha wako kalizuia kasema ww hufai kupewa kazi ile kwa sababu wazaziwako ni chama cha upinzani

naombeni muniamini kwa haya maneno niliondika mm sikusingizia wala sikuandika kwa chuki Bali huo ndio ukweli na mpaka barua nilizoomba ninazo nilizotoa kopy
pole sana Ami. babu zetu enzi za kuikomboa nchi kutoka mikono ya mkoloni mweupe waliuliwa kwa risasi za moto. mkoloni mweusi anaua kisaikolojia kama hivyo. mapambano yaendelee.
 
Unaajiri watu wakiwa ofisiani kila kitu kupinga tu ,ofisi zinajaa migogoro na masiasa yasiyoisha

Mara kila siri za ofisi unazikuta mitandaoni kila siku.mtakaa sana nyumbani hadi muitwe baba wa nyumbani


Nashauri usaili uangalie background za kisiasa watu wawe eliminated mapema .


State agent
Kwa hiyo unatarajia CCM itatawala milele hongera sana mkuu! Unashindwa kabisa kutambua kwamba kuna watu lukuki ambao hawaaamini katika chama chochote cha siasa unafikiri hao unawaweka katika situation gani!
 
Back
Top Bottom