Ajira kugawanywa bara na visiwani, nafikiri kuna tatizo

Ajira kugawanywa bara na visiwani nafikiri sana kuwa ingefaa ajira zipatikane kupitia taratibu za ushindani, bila kujali mtu anatoka wapi, iwe kwa taasisi za umma, serikali ya JMT, iwe kwa ajira kwenye vyombo vya usalama.

Ni nini kimepelekea kubadili mfumo wa ajira? Kama watu wa upande mmoja utakosa sifa kwa watu wa upande huo, watalazimisha kuajirawa tu? Hali hiyo naona kuzidi kutengeneza 'gap' la muungano!
Wazanzibari wengi uwezo wao mdogo kuanzia mashuleni hadi kwenye ajira, huo mgawanyo wa ajira sawa mm siuafiki maana wataajiriwa watu wasio na uwezo kisa usawa wa ajira. Tumepigwa
 
Huo ustaarabu wa kizenji ni upi Mkuu,ambapo bila huo ungetufanya tuhame nchi.Fafanua kidogo mkuu jinsi huo ustaarabu ulivyowaokoa Watanganyika.
Mapenzi kwa wote, chukia dhulma na tenda yaliyo sawa bila kubagua.

Sasa niambie yule jamaa yenu si mngeishia kuhama tu nchi hii
 
Tunahitaji serikali moja. Visiwa vya unguja na pemba view mikoa. Na neno Muungano libaki kwenye kumbukumbu tu
 
Tuwaache watanzania wenzetu waje wafanye kazi bara kwanza idadi yao ndogo na ningeshauri teuzi za ma DC, RC, wakurugenzi nao wachukuliwe kuboresha zaidi muungano hakuna madhara yoyote mfano zile ajira za walimu katika ile idadi Zanzibar wangechukuliwa hata walimu mia kwao ni wengi sana.
 
Back
Top Bottom