Suala la Bodaboda msipotoshe. Kuna kuhangaika na kuna kuwa na ajira

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,566
41,085
Kuna watu ni kama walikuja Duniani kueneza unafiki, uwongo na kufanya hadaa.

Katika maisha yetu ya kila siku, kila mmoja angependa kupata kazi, iwe ya kuajiriwa au kujiajiri. Hata hivyo, kuna wakati watu wengi wanakosa kazi za kuajiriwa, na wanashindwa kutengeneza ajira zao wenyewe na wengine.

Mtu anapokosa kupata ajira, na akakosa kazi ya kujiajiri, atafanya nini? Hawezi kukaa tu akisubiria ajira au uwezo wa kujiajiri. Ni lazima atalazimika kuhangaika ili angalao maisha yaende, akiwa na matumaini kuwa siku moja atapata ajira au atakuwa na uwezo wa kujiari. Kuhangaika siyo ajira. Kuna kuhangaika na kujiajiri.

Watu wengi Duniani, hata walio na makampuni makubwa leo, asilimia kubwa kabisa, kuna wakati waliajiriwa, wakapata mitaji, ujuzi, uzoefu na networks, ndipo wakajiajiri na baadaye kuajiri watu wengine.

Hapa kwetu kuna hadaa kubwa, mtu amemaliza tu chuo, anaambiwa akajiajiri. Atajiajiri vipi wakati hana mtaji, hana uzoefu wala hana networks?

Kuendesha bodaboda, kupanga nyanya, mitumba barabarani au kutembeza soksi mitaani, siyo ajira bali ni kuhangaika ili kuganga njaa. Watu hawa ni wa kuonewa huruma, ni wa kusaidiwa, wapo kwenye mazingira ya mpito wakitarajia siku moja watakuwa kwenye ajira, iwe ni kwa kuajiriwa au kujiajiri.

Kauli ya Lema, ni kauli ya mtu mkweli. Kufanya kazi ya bodaboda au kupanga bidhaa barabarani au kutembeza tenga la nyanya mtaani, huwezi kunidanganya eti ni baraka. Na hakuna bodaboda, mpanga bidhaa barabarani au mtembeza tenga mtaani anayetaka mwanaye aje naye afanye kazi hiyo.

Watu wanafanya kazi hizo ili angalao wao wenyewe na familia zao wapate kuishi. Na wengine katika hayo mahangaiko wanatafuta chochote ili kutimiza mahitaji ya shule ya watoto wao ili wakiwa wakubwa wapate ajira, wasifanye kazi za kuhangaika kuganga njaa kama wao.

Enyi wanafiki, ebu niambieni, ni nani al8wahi kushangilia au kufanya tafrija eti kwa sababu yeye mwenyewe, mwanae au nduguye amefanikiwa kupata kazi ya kuwa bodaboda, ya kupanga mitumba barabarani au kutembeza tenga la nyanya mtaani?

Kama bodaboda ni kazi ya baraka, kama wanafiki wengi wanavyotaka kutuaminisha, ni waziri, mbunge au RC gani amemtafutia kazi mwanaye ya kuwa bodaboda? Mkumbo na Kohongozi watuambie, ni watoto wao wangapi wamewapeleka kwenye kazi hii ya bodaboda yenye baraka tele?

Kwanza ni kazi yenye risk kubwa ya maisha. Tumepoteza vijana wengi sana kwenye ajali za pikipiki na wengine ni vilema wa kudumu. Nina kumbukumbu mbaya moja, ambapo rafiki yangu alikuwa akimgharamia masomo kijana yatima (baba yake alifariki, mama yake alikuwa hai).

Alipomaliza kidato cha 6, anasubiri kujiunga chuo kikuu, alimwomba huyo rafiki yangu amnunulie bodaboda ili angalao ahangaikie matumizi ya nyumbani pao. Rafiki yangu alimnunulia pikipiki kijana yule.

Baada ya wiki mbili akapigiwa simu kuwa kijana wakati yupo barabarani kuna lorry lilimwaga oil, pikipiki yake ikateleza akaanguka, gari iliyokuwa nyuma yake nayo ikateleza ikashindwa kusimama, na kumwua yule kijana. Huyo ni mmoja, lakini wengi wamepoteza maisha.

Bodaboda ni ndugu zetu, ni watoto wetu, ni marafiki zetu, wanahangaikia maisha lakini kama si wote, basi wengi wao wanatamani wawe kwenye ajira. Kama Taifa tutambue kuwa tuna jukumu kubwa la kuwaleta vijana hawa kwenye ajira kuliko kuwahadaa na kuwafanyia ghiliba kuwa eti hiyo ndiyo ajira yenye baraka.

Niambieni ni kijana gani yupo chuoni au shule, au ni mzazi gani anamsomesha mwanae ili siku moja aje kuwa bodaboda mzuri?

Hata ukienda bima ukataka kukata bima yako binafsi ya maisha na ajali, kuna mashirika ya bima, kwenye fomu yao wanauliza kama unatumia usafiri wa pikipiki, ukisema ndiyo, malipo ya bima ya kila mwaka yanapanda, kwa sababu inaonekana dhahiri kuwa kwako wewe uwezekano wa kupata ajali ni dhahiri zaidi kuliko ambaye hatumii usafiri wa pikipiki.

Tuwe wakweli, Taifa lina tatizo kubwa sana la ajira. Tunatakiwa kuwa na mipango madhubuti ya kutengeneza ajira ili vijana wetu waliopo kwenye shule na vyuo wasikate tamaa wakijua hata baada ya masomo yao, hatima yao ni kuwa bodaboda, wauza mitumba barabarani na watembeza matenga ya nyanya na vitunguu mitaani.
 
Maisha ni safari

Kwa taarifa Yako Kihongosi alikuwa Bodaboda pale Kihesa Iringa na akapanda hadi kuwa Mkuu wa Wilaya anayoishi Lema

Kwa sasa Kihongosi ndiye mtendaji Mkuu wa mambo ya Vijana nchini

Safari ni hatua hata kule Moshi mwanzo wa kumiliki Bar huanzia na kumiliki Kilabu cha mbege!

Siyo kila binadamu ana Ujasiri wa kufanya Uhalifu ili afanikiwe

Mchungaji Msigwa alianzia kwenye umachinga wa Mitumba pale Miyomboni lakini leo ni boss wa Chadema Kanda ya Nyasa
 
Safi sana
 
Tanzania ni nchi masikini na uthibitisho ni hao boda boda na wapanga bidhaa chini ndani ya nchi ambayo zaidi ya 60% ya ardhi yake ni fertile.

Nchi yenye Madini tele, Maliasili, Maziwa, lakini watu wake wanasoma History of Russia sijui slavery, Matrix, na ujinga ujinga.

Hivi kama mitaala yetu mashuleni ingekuwa relevant, practical na direct kama hivi

1. Agriculture 50%
2. Minerals 5%
3. Manufacturing 10%
4. Health 15%
5. Other 30%

Tungekuwa nchi tajiri kiasi gani?

Kwanini watoto wasiwe na masomo yanayo base kwenye real life experience, kuweka lazima masomo kama kilimo?

Watu wasingejazana Dar wakati Songea, Moro, Mtwara, kagera nk kuna ardhi ya kutosha.
 
Siku hizi wanasomea Political science
 
Maisha ni safari

Kwa taarifa Yako Kihongosi alikuwa Bodaboda pale Kihesa Iringa na akapanda hadi kuwa Mkuu wa Wilaya anayoishi Lema

Kwa sasa Kihongosi ndiye mtendaji Mkuu wa mambo ya Vijana nchini

Safari ni hatua hata kule Moshi mwanzo wa kumiliki Bar huanzia na kumiliki Kilabu cha mbege!

Siyo kila binadamu ana Ujasiri wa kufanya Uhalifu ili afanikiwe

Mchungaji Msigwa alianzia kwenye umachinga wa Mitumba pale Miyomboni lakini leo ni boss wa Chadema Kanda ya Nyasa
Nadhani hujanielewa. Au soma tena ili uelewe hoja. Nimesema wazi kuwa kuwa bodaboda au kutembeza matenga, kila anayefanya hivyo, anahangaika kama shughuli ya mpito akiwa na matumaini ya kupata ajira.

Labda ungeniambia kuwa Kihongosi alikuwa bodaboda na mpaka leo ni bodaboda au anatamani aiache nafasi aliyo nayo sasa ili akawe bodaboda, hapo ungekuwa na hoja.
 
Kwahiyo siyo ajira ya laana?
 
Unajaribu kumtetea Lema ila tatizo neno alilolitumia "laana" dah ni Kali mno.

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
Nakubaliana nawe kuwa neno alilolitumia ni kali mno, lakini lenye ukweli. Hoja ya msingi ni kwamba kuwa na bodaboda wengi siyo baraka bali ni kiashiria cha ukosefu mkubwa wa ajira.

Viongozi wasitulaghai kuwa kazi ya bodaboda ni baraka.
 
Boda boda haijawahi kuwa ajira, zaidi ni mihangaiko inayowapelekea vijana kuwa kwenye risk ya kufa. Bodaboda ni moja kati ya makundi yaliyotokana na mfumo mbovu wa elimu wacha wajibless na dabokii wakiwa speed na helmet amefunga nyuma kama mzigo huku kichwa ikiwa wazi.
 
Back
Top Bottom