Ajira kugawanywa bara na visiwani, nafikiri kuna tatizo

chikambabatu

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
1,334
1,318
Ajira kugawanywa bara na visiwani nafikiri sana kuwa ingefaa ajira zipatikane kupitia taratibu za ushindani, bila kujali mtu anatoka wapi, iwe kwa taasisi za umma, serikali ya JMT, iwe kwa ajira kwenye vyombo vya usalama.

Ni nini kimepelekea kubadili mfumo wa ajira? Kama watu wa upande mmoja utakosa sifa kwa watu wa upande huo, watalazimisha kuajirawa tu? Hali hiyo naona kuzidi kutengeneza 'gap' la muungano!
 
Mbona naona kama mpaka sasa waliochangia ni wale wanaoitwa SG!

Au kuna mambo yanaunganisha timu zote zinakuwa moja?

Kazi iendelee
 
Hapa ndipo panatengeneza madai ama ya serikali tatu au moja.

Wazanzibar Wanahaki ya ajira au teuzi pande zote mbili za muungano lakini Watanzania bars ambao kiuhalisia ni watanganyika hawana haki na teuzi au ajira Zanzibar.

CCM inatukandamiza watanganyika kwa maslahi ya chama chao
 
Muungano una matatizo mengi sana, ndio maana malalamiko hayaishi toka pande zote bara na visiwani.

Bora uvunjwe au wakae chini waufumue utengenezwe mpya utakaoleta manufaa kwa pande zote mbili ili kuondokana na malalamiko yasiyoisha.

Huu muungano uliopo unawalea wazanzibar kama watoto wadogo, umeme wao unatoka bara na mara ya mwisho nilisikia wanadaiwa.

Bado pesa za sherehe za muungano zikagawanywa nusu wakati nao wana vyanzo vyao vya mapato, bado tena nafasi za ajira zigawanywe nusu wakati bara tuko wengi zaidi ya visiwani, hizi zote ni kero.
 
Katika muungano nadhani kuna vitu ambavyo vipo katika masuala ya Muungano na ambavyo havipo na si kila kitu tumeungana hivyo basi hakuna haja ya kila kitu tuwe sawa.
 
Ajira kugawanywa bara na visiwani nafikiri sana kuwa ingefaa ajira zipatikane kupitia taratibu za ushindani, bila kujali mtu anatoka wapi, iwe kwa taasisi za umma, serikali ya JMT, iwe kwa ajira kwenye vyombo vya usalama.

Ni nini kimepelekea kubadili mfumo wa ajira? Kama watu wa upande mmoja utakosa sifa kwa watu wa upande huo, watalazimisha kuajirawa tu? Hali hiyo naona kuzidi kutengeneza 'gap' la muungano!
Ndio swala msingi mambo ya kuzingatia ukabila kwa kigezo cha utaifa hakipo
 
Back
Top Bottom