Ajira bomba la mafuta kutoka Ohima- Uganda mpaka Chongoleani-Tanga

Shararizo

Member
Aug 14, 2017
40
19
Ni miezi kadhaa sasa imepita tangu Rais wa Uganda Yoweri museveni na Rais wa Tanzania John Magufuli kusain makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta katika nchi hizi mbili.

Swali ni je, ujenzi utaanza lini? maana tuliambiwa kuna ajira zaid ya elf 10 na vijana wengi wamekaa mkao wa kula kusubir hizo ajira.

Ikumbukwe, mwaka 2018 TaESA walitoa waraka watu wakajiandikishe ili wajue kama wataalamu wanatosha na toka hapo hawajasema lolote mpaka leo hii.
 
Ikumbukwe, mwaka 2015 TaESA walitoa waraka watu wakajiandikishe ili wajue kama wataalamu wanatosha na toka hapo hawajasema lolote mpaka leo hii.
Vuta subira mkuu.ajira zitakuwepo kama wewe una vigezo.endelea kufuatilia
 
Magufuli hataniii, subirieni tu....
Tunapokosea ni hapa sasa ajira na Magufuli vinawiana wapi? Total hawana longo longo ktk utendaji sio kama wale waturuki wa reli ya kati, kuna maswali huwa wanayauliza kwenye mikutano na serekali kwaajili ya kujiridhisha kabla ya utendaji kuanza, unakuta makatibu wa wizara wanajiuma uma tu. Kuna swala la kuimalizia bandari ya Tanga wao Total hawataki Double hendeling wakati wa kushusha mzigo na huku bandari ya Dar haijamalizika ujenzi kwa sasa berth 3 tu ndizo zinatumika.
Kuna maswala mengi sana yanapashwa kuwekwa vyema ndipo kazi ianze tuvumilieni kwanza wataalamu wajiridhishe utendaji uwe wa uhakika zaidi, huo ndio uelewa wangu juu ya huu mradi.
 
Hv kwa mtu ambaye anaishi eneo tofauti na hayo maeneo ya ujenzi ataweza kupata hy ajira.?
Mfano mtu anaishi mtwara ataweza kupata hy ajira.?
 
Haiwezekani... Kwanin upate wew wakat wazawa wapo eneo lile. Kila sehem na fursa zake...

Mradi umeanza kwenye early stage...na maexpert wengi ni wazungu, waTanzania tunajua kulalamika sana lakini hatutaki kuongeza proffesional skills! tukipata tu Masters tunaona tumetoboa wakati mradi unaconsider international profresional standards. Tuende sasa tukawe maadmin, vibarua na wajasiriamali (local suppliers) wa mradi. !
 
Ni miezi kadhaa sasa imepita tangu Rais wa Uganda Yoweri museveni na Rais wa Tanzania John Magufuli kusain makubaliano ya ujenzi wa bomba la mafuta katika nchi hizi mbili.

Swali ni je, ujenzi utaanza lini? maana tuliambiwa kuna ajira zaid ya elf 10 na vijana wengi wamekaa mkao wa kula kusubir hizo ajira.

Ikumbukwe, mwaka 2018 TaESA walitoa waraka watu wakajiandikishe ili wajue kama wataalamu wanatosha na toka hapo hawajasema lolote mpaka leo hii.
Wenye Pesa za kugaramia hili Bomba bado
 
Back
Top Bottom