Ajinyonga hadi kufa sababu ya kupigwa na mkewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajinyonga hadi kufa sababu ya kupigwa na mkewe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by X-PASTER, Aug 11, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Ajinyonga Hadi Kufa Sababu Ya Kupigwa Na Mkewe.

  Mkazi mmoja katika Mtaa wa NHC katika Mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti wilayani Mara, Samson Kitoshi (32) amejinyonga hadi kufariki dunia kwa kamba chumbani kwake kwa kile alichodai kuwa: “Amechoka kupigwa na mkewe kila wakati

  Tukio hilo lililovuta umati mkubwa wa watu, linadaiwa kutokea jana saa tano asubuhi. Akisimulia mkasa huo, mtoto wa marehemu (jina tunalihifadhi) alisema kabla ya kutokea kwa tukio hilo, mama yao alimpa Shilingi 1,000 akanunue sukari na vitafunwa, lakini asimpe baba yao chai... "Mama aliaga kuwa anakwenda Hospitali DDH kwa kuwa anaumwa. Baba akasema hatakunywa chai hiyo na kutuambia kuwa hatutamwona tena anatuaga na tusiingie ndani."

  Marehemu baada ya kuingia chumbani kwake anadaiwa kuwa alifunga kamba juu ya dari na kujining'iniza hadi alipokata roho. Mtoto huyo wa darasa la tatu ambaye ana umri wa miaka 10 alisema hawakuweza kuingia ndani kama walivyoambiwa na baba yao, lakini baadaye aliamua kumwamsha akidhani kuwa amelala ili anywe chai ndipo alipokuta amening'inia. Alipiga kelele kuomba msaada.

  "Baba alikuwa amevua shati akawa amening'inia chini kuna meza nikaweka stuli ili nifungue kamba sikuweza nikapiga yowe majirani wakafika wakasema ameshakufa," alisema.

  Kuhusu migogoro ya ndani, mtoto huyo alisema kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara hasa ukisababishwa na mama yao ambaye anauza pombe ya kienyeji ya wanzuki anaporudi akiwa amelewa kwani humfanyia vurugu baba yao.

  "Hivi karibuni baba alifikia hatua ya kumtaka mama aondoke amechoka na mateso anayomfanyia, lakini mama alikataa kuwa hawezi kutoka na kudai yeye ndiye atakayetoka," alisema. Ndugu wa Kitoshi ambaye anaishi katika Kijiji cha Morotonga alisema kuwa marehemu aliyekuwa akifanya kazi ya kusaga nafaka alikuwa akilalamika kupigwa na mkewe mara kwa mara.

  "Huyu ni ndugu yangu hata leo amefika kwangu na akanikosa na kurudi nadhani alitaka kuniambia kitu. Baada ya muda nikapigiwa simu kuwa amekufa kwa kujinyonga, amechoshwa na kupigwa," alisema.

  Kamanda wa Polisi Wilaya ya Serengeti, Paulo Mng'ong'o alijaribu kumtafuta mwanamke huyo kwa simu lakini mara baada ya kujitambulisha kuwa yeye ni OCD, mama huyo alikata simu.

  Baada ya muda mama huyo alifika nyumbani na kumkuta mume wake akining'inia kwenye kamba. Huko alipokewa kwa maneno makali kutoka kwa wanawake wenzake waliokuwa na hasira baadhi wakisema: “Ulitaka afe ujitawale sasa amekufa tanua... unadanganya ulikuwa hospitali mbona umelewa..."

  Maneno hayo makali yalimwingia mwanamke huyo kwani alikaa chini kisha akalala chali na kupoteza fahamu. Hakuweza kunyanyuka hadi alipopakiwa kwenye gari la polisi pamoja na mwili wa mumewe na kupelekwa hospitali.

  Akizungumzia tukio hilo, Kamanda Mng'ong'o alisema polisi inalifanyia uchunguzi na kwamba itatoa taarifa kwa umma. Alisema wangefanya mahojiano na mke huyo wa marehemu baada ya kuzinduka kujua chanzo cha kifo hicho.Mwenyekiti wa Mtaa wa NHC, Elias Nyamraba alisema kuwa wanasubiri ndugu wa marehemu kwa ajili ya hatua nyingine ikiwemo ya mipango ya mazishi akisema Kitoshi ni mzaliwa wa Kijiji cha Issenye.  Source: Mwnanchi
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Soma Nyakati Kamanda.
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,656
  Trophy Points: 280
  Kila nikisema hii ni aina ya ukichaa na ugonjwa mnanibishia!!
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  RIP kamanda, umemkosea Mungu though.....
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Aug 11, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,408
  Trophy Points: 280
  Daaah hawa wanawake wa siku hizi hawa. Matata kweli kweli.

  Lakini mwanaume mzima hadi unafikia hatua ya kudundwa na mkeo basi wewe hufai tena kuitwa mwanaume. Ni heri tu ujinyonge aisee.

  Piga picha eti Ngabu kadundwa na mkewe...ahahahahaaaaaa daaaaah....hell no. Not even hell no. It's hell to the nooooooooo. It ain't happening and it ain't gonna happen.
   
 6. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #6
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaaaani aibu tupu kweli bora kujitundika tupu kuliko kufedheheshwa.

   
 7. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #7
  Aug 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wanaokataaga kwa sauti hivi ndo haswaaaa hua yanawakuta!!!Subiria baunsa lako likupate uone!!
   
 8. M

  Masuke JF-Expert Member

  #8
  Aug 11, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Mke wangu akinipiga toka siku hiyo ndoa inavunjika na nitahesabu nilikuwa na date naye tu hata kama tuna watoto wana ndevu.
   
 9. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #9
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  ngoja nijifue na mie,watu kwa mifumo dume siwawezi wanaona sawa mwanamke kupigwa na mwanaume ila si sawa mwanaume kupigwa na mwanamke..........mnalo mbona!
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Aug 11, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mhhhhhhhhhhhhhhhh
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Aug 11, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  yaani ni kama mie nnavyoshangaa eti mwanamke anapigwa na mumewe! hellll noooo! yaani nalengesha riasi moja tu ikulu, i destroy u for life even ur mamma wont recognise her poor lil buoy! lol
  <br />
  <br />
   
 12. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #12
  Aug 11, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br /
  Who knows what the future holds? Wanawake wengine wako fit kwenye masumbwi bwana.
   
Loading...