AJILA Vs AJIRA

Wakuu Mambo VP

Naomba mnidadavulie hayo maneno

Asante


Hayo ni maneno yaliyotokana na kiarabu, linalotumika sana kwa kiswahili hapa kwetu ni ajira, wengi hulitamka na kuliandika visivyo "ajila", hii haileti maana sahihi kwani ajila nalo ni neno pia, lenye maana tofauti kabisa na ajira, lakini halitumiki sana katika kiswahili cha siku hizi hususan cha bara. Wa-pwani, wenye asili ya kiswahil tena wazamani, wanaijuwa maana ya neno "ajila", kwa sasa naliwacha kulitolea maana hili neno kwa sababu za kiufundi.

Natumai maana ya ajira unaijuwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom