Ajikata uume kisa urijali

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Chemba. Mkazi wa Kijiji cha Itolwa wilayani Chemba Mkoani Dodoma, Juma Juma (34) amelazwa katika kituo cha Afya cha Hamai wilayani Chemba akiwa hoi baada ya kujikata uume wake.

Inadaiwa kuwa Juma amefikia uamuzi huo baada ya kupata ajali na kuteguka kiuno na kusababisha asiwe rijali.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumapili Novemba 19, 2021 mjomba wa Juma, Yasini Nkusa amesema tukio hilo la Juma kujikata uume lilitokea Ijumaa nyumbani kwake Kijiji cha Itolwa ambapo alitumia wembe kukata uume wake.

Hali ya majeruhi huyo imeelezwa kuwa mbaya pamoja na kwamba jitihada za madaktari wa Kituo cha Afya Hamai kuendelea kuokoa maisha yake.

Juma ambaye ana mke na watoto watatu alipata ajali ya gari wiki mbili zilizopita.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Itolwa, Daudi Ally amethibitisha tukio hilo akisema mhusika amechukua maamuzi magumu huku akidai kuwa ni tukio la kwanza kutokea Kijijini hapo.

Ametoa wito kwa wananchi kuacha kufanya maamuzi ambayo yanaweza kuathiri maisha yao.

Mkazi wa kijiji hicho, Maulidi Kijongo amesema ameshangazwa na uamuzi huo akidai hakupaswa kufanya hivyo.

Chanzo: Mwananchi

Pia soma: Rukwa: Mwanaume ajikata Uume kwa kukosa mpenzi
 
Huyo jamaa kwa kweli ni wa kuhurumiwa tu kwa sababu hajui alilolitenda. Kwanza Mungu alishambariki kuwa na watoto watu sasa alitaka Mungu ampe nini tena. Kuna watu wanamuomba Mungu usiku na mchana kuanzia Januari mpaka Disemba angalau wapate japo mtoto mmoja lakini bado hawajajaliwa na hawajakata uume wao. Au hao watoto wote watatu walikuja na mama yao hamna wa kwake hapo? Pili anatakiwa ajue tunaishi kwa mapenzi ya mwenyezi Mungu kwa hiyo lolote linaweza tokea wakati wowote ndio maana waswahili wakasema "hujafa hujaumbika".

Jambo lingine baya alilofanya huyo jamaa ni maamuzi ya haraka tena ya kukurupuka hasa. Hivi alijuaje kuwa mnara wake hautasimama daima wakati kapata ajali wiki mbili tu zilizopita. Alipaswa aendelee na matibabu angalau hata miaka miwili au mitatu hivi aangalie maendeleo yake lakini hata kama mnara usingesimama baada ya muda bado maamuzi ya busara sio kuukata huo mnara wake.
 
Jamaa chizi sana mtu unaeza ukawa hujapata ajali na mnara usisimame hata wiki ka kichwa kimevurugika na maisha...

Angevuta mda aone
 
Sasa uume una shida gani jamani?

Angekata kiuno tu.

Omba Mungu akupe maarifa ya kutambua kuwa uume siyo kwa ajili ya kugegeda.

Akili za Wagogo ni fupi sana, kama yule jamaa MC
Usiseme hivyo omba MUNGU akulinde.
Huyo tayari ana mke na watoto.
Unajua mkewe anataka Nini?
hapo mke ameshaomba alafu jamaa kashindwa kupeleka Moto .kinachofuata NI dharau na kugongewa
Acha tu
 
Inawezekana japo alikuwa na mke na watoto lakini alikuwa msingi kiuno. Kwa ghadhabu ya kitendea kazi kutofanya kazi tena akaona akinyofoe tu.
Labda ana plan B ya kutaka kutumia njia nyingine ambayo imebaki kwa starehe.
 
Sasa si tayari kuna sababu ya yeye kushindwa kugegeda, shida nini hadi kujiua.....
 
Mpuuzi sana huyo jamaa.
Na hapo aombe Mungu matabibu waokoe maisha yake,ole wake afe halafu aache hao watoto yatima...ntaomba wanaume wa huko waichape mikwaju maiti yake!!.
 
Back
Top Bottom