Ajali yaua Wanandoa Dodoma, kichanga wao anusurika

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Watu wawili mke na mume wamefariki dunia kwenye ajali iliyohusisha gari ndogo na treni katika makutano ya reli, Kata ya Tambukareli, Dodoma.

Akizungumzia marehemu hao Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Ibenzi Ernest amesema walipokea mwili wa mwanamke Furaha Rashid huku mume wake Hussein Chilala akiwa katika hali mbaya.

“Ilikuwa majira ya saa tatu usiku mwanamke tulimpokea akiwa tayari amefariki, lakini mwanaume alikuwa na hali mbaya na wakati anapatiwa huduma akafariki muda mfupi baadaye,” amesema Ibenzi.

Ibenzi amesema marehemu waliumia zaidi kichwani hali iliyosababisha kuvuja damu nyingi na kupoteza maisha.

Hata hivyo, katika ajali hiyo ambapo marehemu walikuwa na mtoto wao anayekadiriwa kuwa na mwaka mmoja, Ibenzi amesema walimpokea mtoto huyo akiwa mzima na alisema amechukuliwa na mama yake mdogo kwani hakuumia sehemu yoyote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema atamrudia mwandishi baada ya kumaliza kikao.

MWANANCHI
 
Hawa wanao kufa kwa kugonga treni wana kufaga kwa ujinga wao tu na mahakala ya kijinga
Hujui chochote masta

.. Tema mate Chini na omba yasikukute

Nakumbuka nilikuwa naenda Mwanza usiku, nimefika Manyoni kwenye saa nane kasoro hivi.. Baridi ni 14 ⁰c sina hili wala lile nastuka Treni hili hapa...
This has nothing to do with knowedge.. likifika limefika.

Raha ya Milele uwape ee Bwana...

Wapumzike kwa amani.
 
Jamaa kaandika kimihemko sana
 
Kwa nini mamlaka(TRC) hawafungi njia ili treni ipite kwanza?, wakiweka hata magogo pande zote mwa barabara napo ni vigumu?
 
Hujui chochote masta

.. Tema mate Chini na omba yasikukute

Nakumbuka nilikuwa naenda Mwanza usiku, nimefika Manyoni kwenye saa nane kasoro hivi.. Baridi ni 14 ⁰c sina hili wala lile nastuka Treni hili hapa...
This has nothing to do with knowedge.. likifika limefika.

Raha ya Milele uwape ee Bwana...

Wapumzike kwa amani.
Mwnyw imewahi kunikuta usiku mmoja tunatoka ifakara kuzika, tuko kama msafara wa gari 6 hivi,
yangu ndo ya mwisho, nmempakia wife,washkaji na wazee wa heshima kadhaa.

Nmefunga vioo, tunakula kiyoyozi
zinapiga kwaya na story kadhaa zinaendelea
Kuna reli flani Iko kwny Kona kali (sipakumbuki jina).
Ile nmevuka tu Yale machuma chuma, naona mwanga mkali sn unanipiga Kwa nyuma kupitia side mirror.
Nikajua litakua fuso hili, nichek namna ya kumpisha.
( Kawaida Sipendagi kuongozana na malori barabarani)

Kuangalia nyuma mwanga umepotea,
Ikabd kushusha kioo, duh! Naskia mtikisiko mno
Kumbe ni treni limetupita na liko spidi Kali balaa. Nilisimama kwanza kuvuta pumzi mara tatu maana lingetuvaa tu pale hakuna mtu mmoja angesalia
 
Ungekufa kijinga.
 
Hilo eneo hapo lishaua washkaj zangu kama watatu walikuwa wanalima Ifakara,
Walikuwa kwenye Coaster... walichinjwa karibu wote na treni..

Usiku focus ipo kwenye mambo mengine sana, na huwezi weka akilini hatari ya "kugonga" treni.
 
Back
Top Bottom