field marshall1
JF-Expert Member
- Sep 17, 2017
- 1,171
- 2,730
Nimesikitika kusikia waziri Hamis Kigwangala amepata ajali. Namuomba Mungu amponye kwa wepesi na haraka.
Hizi habari za waziri zilitangazwa sana na wengi wetu watanzania tuliziona kwenye magazeti na wengine kuziona kwenye TV's. Inapotokea ajali mengi yanasemwa kama vile mwendo, umakini wa dereva, hatari zingine kama wanyama kukatisha barabara na uchakavu/ubovu wa gari husika n.k. Lakini si nia yangu kueleza chochote au kuuliza chochote kuhusu haya hapo juu bali nitaongelea jambo moja tu kubwa ambalo wanaJamiiForums mnaweza kusaidia kutoa mawazo yenu.
Katika ajali hiyo ambayo imezungumzwa sana na vyombo vya habari hasa magazeti wale majeruhi wengine wanne pamoja na dereva hatufahamu hali zao na wanatibiwa wapi. Wengine tungependa kufahamu wanaendeleaje!
Pili ni faraja kuona jinsi Emergency unit ilivyofanya kazi kuokoa maisha yake kuanzia alivyopelekwa kwenye center ya Magugu baadaye Selian AMLC na mwisho kule Muhimbili kwa kutumia Helicopter na ndege. Hiyo system iliyotumika inahitaji pongezi kwa kufanya kazi haraka haraka kwa kuokoa maisha ya mtanzania na waziri wetu.
Swali la kwanza ninalouliza ni je huduma kama hiyo(Ndege na Helicopter) inakuwepo kwa watanzania wote wenye health insurance?
Nchi zilizoendelea hayo ni mambo ya kawaida kurusha helicopter kutoka eneo la tukio hadi kwenye hospitali ambazo mara nyingi hazipo mbali sana na miji.
Kwa wenzetu hata kama huna insurance (bima ya afya) utatibiwa na maisha yataokolewa. Hutaulizwa una bima au la.
Swali la pili, tumeona waziri amepelekwa hospitali zaidi ya moja. Ina maana bado hakuna specialized treatment kwenye hospitali zetu za mikoa au za rufaa?
Swali la tatu kwa wale raia wa kawaida wanaopata ajali kama aliyopata mhe. Kigwangalla je wanatibiwa vipi? Ke wanapelekwa kwenye specialized treatment(Kama wanayo bima au hawana)?