Ajali ya Waziri Kigwangala: Je, kila mtanzania anahitaji matibabu bila ubaguzi?

Kweli Tanzania tuko nyuma sana kama yunaaminishwa kuwa helikopta haiwezi kubeba wajeruhi wote na kuwapeleka katika matibabu
bora.
Mwandishi wa habari aliyekufa alikuwa anamhudumia huyo waziri.lakini serikali inashindwa hata kumtaja pamoja na hao wengine walioumia.
Kuna Mwana jf hapa anasema ni kupotosha kusema mtu amekufa ina maana yeye hana habari kabisa kama mwandishi kijana mdogo kabisa kafa katika ajali hiyo! Lol! Afruika tuna riho mbaya na umwinyi mwingi.
Mola atusamehe!
 
Katika ajali hiyo ambayo imezungumzwa sana na vyombo vya habari hasa magazeti wale majeruhi wengine wanne pamoja na dereva hatufahamu hali zao na wanatibiwa wapi. Wengine tungependa kufahamu wanaendeleaje!


Kumbuka mwaka 2007 kama sijakosea alipopata ajali Marehemu Salome Mbatia, je ulisikia au kusoma popote juu ya dereva wa lile gari dogo?

Nilichojifunza ni kwamba watumishi wa viongozi hutumiwa kama vyombo, yanapotokea majanga umuhimu wao huishia pale
 
Nilipokuwa Butiama, wakati wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu, mara nyingi tulikula pamoja na Mwalimu chakula kile kile. Sisi kila mmoja akila kwenye sahani yake lakini yeye akila na wajukuu zake kwenye chombo kimoja.

Mwalimu hata kwenda Uingereza alilazimishwa sana. Yeye binafsi alikataa kabisa. Ikafikia mpaka Mkapa mwenyewe kuingilia kati.

Tuongelee watu wengine lakini siyo mwalimu. Alikuwa zaidi ya wengi wetu tunavyoweza kufanya. Mungu amrehemu kwa kuiishi fadhila ya umaskini


He was unique
 
Nilipokuwa nikifanya kazi kwenye kampuni moja ya kigeni, wote tulikuwa na bima za aina moja


Ndugu yangu bima za hapa nchini na hasa NHIF haipo kwaajili ya watu wa kipato cha chini, ipo kwaajili ya wanene wa huo mfuko.
 
Marekani mtu anachangia bima ya afya wastani wa dola 12000 kwa mwaka ambayo ni sawa na shilingi milioni 24 ndio maana huduma ni nzuri.Huwezi toa huduma zote hizo kwa mtu kuchangia bima shilingi Elfu hamsini kwa mwezi.Hospitali haziwezi toa hizo huduma kwa pesa zipi?
Siyo kweli kwamba Marekani wanalipa Dola 1000 kwa mwezi kama unavyosema! Kama bima ya afya unapata kupitia kazi unaweza kukatwa dola 90 hadi dola 110 kwa kila paycheck hivyo kwa mwezi ni kuanzia dola 180 hadi 220 kwa mwezi hivyo hapo ni kama $2,160 hadi $2,640 kwa mwaka mmoja, kama huna kazi (most unlikely) unaweza kulipa chini sana au usilipe kama huna pato (income)lakini unapewa bima yenye coverage sawa na anayelipia hapo juu ( refer Obama care au Affordable Care Act-ACA) Co-pay unaweza ukalipa au usilipe kutegemeana na aina ya bima kama Aetna, Blue Cross Blue Shield, Anthem nk. Ukifanya kazi part time contribution yako inakuwa kidogo unaweza ukalipa kila check $50 kwa kila check hivyo kwa check mbili kila mwezi utalipa $ 100 lakini unapata huduma sawa na anayelipa zaidi, Unaweza ukalipa co-pay ya dola 10 au 15 kila unapoenda kumuona daktari au usilipe. Nachosema ni kiwango cha huduma ni sawa, hakuna cha anayepata huduma bora zaidi kwa sababu ni waziri au Gavana. Ushauri wangu ni ku-improve huduma zetu za afya ili ziwafikie wananchi wengi zaidi.....Kama Cuba wanaweza kwanini sisi tushindwe? Wananchi wengi wakiwa na bima hata hizo gharama za matibabu zitapungua.
 
Nimesikitika kusikia waziri Hamis Kigwangala amepata ajali. Namuomba Mungu amponye kwa wepesi na haraka.

Hizi habari za waziri zilitangazwa sana na wengi wetu watanzania tuliziona kwenye magazeti na wengine kuziona kwenye TV's. Inapotokea ajali mengi yanasemwa kama vile mwendo, umakini wa dereva, hatari zingine kama wanyama kukatisha barabara na uchakavu/ubovu wa gari husika n.k. Lakini si nia yangu kueleza chochote au kuuliza chochote kuhusu haya hapo juu bali nitaongelea jambo moja tu kubwa ambalo wanaJamiiForums mnaweza kusaidia kutoa mawazo yenu.

Katika ajali hiyo ambayo imezungumzwa sana na vyombo vya habari hasa magazeti wale majeruhi wengine wanne pamoja na dereva hatufahamu hali zao na wanatibiwa wapi. Wengine tungependa kufahamu wanaendeleaje!

Pili ni faraja kuona jinsi Emergency unit ilivyofanya kazi kuokoa maisha yake kuanzia alivyopelekwa kwenye center ya Magugu baadaye Selian AMLC na mwisho kule Muhimbili kwa kutumia Helicopter na ndege. Hiyo system iliyotumika inahitaji pongezi kwa kufanya kazi haraka haraka kwa kuokoa maisha ya mtanzania na waziri wetu.

Swali la kwanza ninalouliza ni je huduma kama hiyo(Ndege na Helicopter) inakuwepo kwa watanzania wote wenye health insurance?

Nchi zilizoendelea hayo ni mambo ya kawaida kurusha helicopter kutoka eneo la tukio hadi kwenye hospitali ambazo mara nyingi hazipo mbali sana na miji.

Kwa wenzetu hata kama huna insurance (bima ya afya) utatibiwa na maisha yataokolewa. Hutaulizwa una bima au la.

Swali la pili, tumeona waziri amepelekwa hospitali zaidi ya moja. Ina maana bado hakuna specialized treatment kwenye hospitali zetu za mikoa au za rufaa?

Swali la tatu kwa wale raia wa kawaida wanaopata ajali kama aliyopata mhe. Kigwangalla je wanatibiwa vipi? Ke wanapelekwa kwenye specialized treatment(Kama wanayo bima au hawana)?
Mkuu umeibua hoja nzuri sana!
Kuhusu bima ya afya mfano NHIF hawagharamii vipimo vyote na sio dawa zote wanagharimia, sembuse ndege! Labda ujiunge na AAR kama una uwezo!
Kuhusu hospitali zetu ndio hivyo tena, vitu vya kuunga-unga havieleweki, maadam wakuu wote wanakaa Dar es Salaam muhimbili ndio inatupiwa jicho zaidi! na sasa hivi wanatupia jicho Ben-Mkapa Dodoma kwa sababu wengi watahamia huko!
Hii ndiyo Tanzania yetu, wananchi wa kawaida tupambane na hali zetu!
 
Mkuu field marshall 1
  1. Ni swali la msingi sana, tena kumetokea loss of life kwa mtu mmoja mwana fani mwenzetu, wengine hata pole tuu sikuzisikia!.
  2. Emergency unit hizo zipo kila mahali penye uwekezaji wa kimataifa kama migodini, uchimbaji wa gesi na vivutio vya utalii ambako ni mwekezaji ndio ameweka premium kubwa kwenye bima ya afya kuhusisha flying doctors, tena hospitali kubwa kwenye bima hiyo Nairobi Hospital na sio Muhumbili, the next level ni South Afrika na final level ni Europe na America na sio India!.
  3. Yes inapatikana sio tuu kwa Watanzania wote bali kwa mtu yoyote mwenye bima ya Afya ya international yenye highest premium inayohusisha flying doctors. Its very unfortunate NHIF hawana international coverage bali wana referrals only tena zitolewe na Muhimbili,
  4. Nchi za wenzetu kuwa na bima ya afya kwa wananchi wao wote ni lazima kama ilivyo kwa kuwa na social security ni lazima hata kama huna kazi utalipwa UB, hivyo huko kunapotokea emergency, they save life first, mengine yote ni next, na wenzetu na sisi tusio na bima, safari za kuingia nchi hizo huishia kweye dirisha la visa kwa sababu kuwa na bima ni lazima na kwa wasionazo unakata travel insurance ndipo unapewa visa,
  5. Kunapotokea emergency inayohusisha kuitwa flying doctors, wanakupeleka kwanza kwenye the closest proximity standard hospital, baada ya diagnosis ndipo unapelekwa kwenye specialized hospital, and take it from me, soon utasikia Dr, Kigwa is flown to India!. Situation kama hiyo ikitokea kwa wananchi wa kawaida, unahudumiwa kikawaida!.
  6. Specialize treatment ni baada ya diagnosis na prognosis.
Natoa pole na RIP kwa waliopoteza maisha, na get well soon kwa majeruhi.

P.
Mkuu Paschal, hata NHIF kuna vipimo na dawa ambazo hawagharamii!
 
Ndugu yangu bima za hapa nchini na hasa NHIF haipo kwaajili ya watu wa kipato cha chini, ipo kwaajili ya wanene wa huo mfuko.
NHIF inasevu wafanyakazi (3% wewe, 3% mwajiri wako), kuna family package (Nadhani laki saba hivi kwa mwaka), kuna bima toto (50,000 kwa mtoto mmoja kwa mwaka), pia kuna bima mkiwa na kikundi maalum kilichosajiliwa ambapo kila mwanachama anapewa kadi yake! Kwa hiyo usipotoshe sana mkuu!
 
Mkuu Paschal, hata NHIF kuna vipimo na dawa ambazo hawagharamii!
Yes sio tuu kuwa kuna vipimo na dawa hawagharimii, bali kuna magonjwa pia hawatibu na kuna mengine yanahitaji kibali maalum ndipo utibiwe. Lengo sio kufanya ubaguzi, bali kuratibu na kulinganisha na uwezo wa mfuko vinginevyo ukitibu kila kitu, mfuko utafilisika!, mfano mimi hapa nilipo nina complex implant ya neuro stimulus implant, inatumiwa na watu waliopata tatizo linaitwa brachial plexus injury, inauzwa US $ 20,000, inawekewa South Africa, India na Ulaya ba Amerika. Wakitoke Watanzania 100 wanahitaji at a time, mfuko utakuwa na hali gani?. Ndio maana kuna bima za afya na bima za afya, ziko huduma kibao NHIF hawatoi kakini mashirika mengine wanatoa, ikiwemo flying doctors.

Hata hivyo huduma kama hizi, NHIF wanatoa ila kwa kibali maalum
  • Cancer chemotherapy for cancer patients
  • Immunosuppressant medicines for patients, who have organ transplants,
  • Haemodialysis and erythropoietin for patients with renal failure,
  • Reading glasses and special radiological imaging such as CT scan and MRI
  • Medical and Orthopaedic appliances
  • Complex Implants
  • Advanced Cardiac Services
  • Some selected Medicines
  • PolypropyleneMesh
  • EMG needle
  • Dentures
  • Orthodontic Services
  • Radiotherapy services
P.
 
NHIF inasevu wafanyakazi (3% wewe, 3% mwajiri wako), kuna family package (Nadhani laki saba hivi kwa mwaka), kuna bima toto (50,000 kwa mtoto mmoja kwa mwaka), pia kuna bima mkiwa na kikundi maalum kilichosajiliwa ambapo kila mwanachama anapewa kadi yake! Kwa hiyo usipotoshe sana mkuu!


Wanachokisema na reality kwenye huduma ni kama mashariki na magharibi zilivyo mbali
 
Yes sio tuu kuwa kuna vipimo na dawa hawagharimii, bali kuna magonjwa pia hawatibu na kuna mengine yanahitaji kibali maalum ndipo utibiwe yakiwemo. Lengo sio kufanya ubaguzi, bali kuratibu na kulinganisha na uwezo wa mfuko vinginevyo ukitibu kila kitu, mfuko utafilisika!, mfano mimi hapa nilipo nina complex implant ya neuro stimulus implant, inatumiwa na watu waliopata tatizo linaitwa brachial plexus injury, inauzwa US $ 20,000, inawekewa South Africa, India na Ulaya ba Amerika. Wakitoke Watanzania 100 wanahitaji at a time, mfuko utakuwa na hali gani?. Ndio maana kuna bima za afya na bima za afya, ziko huduma kibao NHIF hawatoi kakini mashirika mengine wanatoa, ikiwemo flying doctors.

Hata hivyo huduma kama hizi, NHIF wanatoa ila kwa kibali maalum
  • Cancer chemotherapy for cancer patients
  • Immunosuppressant medicines for patients, who have organ transplants,
  • Haemodialysis and erythropoietin for patients with renal failure,
  • Reading glasses and special radiological imaging such as CT scan and MRI
  • Medical and Orthopaedic appliances
  • Complex Implants
  • Advanced Cardiac Services
  • Some selected Medicines
  • PolypropyleneMesh
  • EMG needle
  • Dentures
  • Orthodontic Services
  • Radiotherapy services
P.
Umesomeka mkuu!
 
Back
Top Bottom