Kitomai
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 1,061
- 281
Nini kifanyike kupunguza ajari za barabarani zinazosababishwa na mwendo kasi? Jamii yetu sasa imekuwa ikishuhudia ajari ambazo zinasababisha vifo visiyo rasimi na kuwaacha maelefu wengine wakipatwa na ulemavu. Awali ya yote nikusimulieni nilichokiona katika ajari iliyotokea hapo riverside tarehe 23 Jumatano majira ya mchana.
Nikiwa nimesimama pembeni ya barabara eneo la Ubungo Riverside nasubiri nivuke upande wa pili ili nichukuwe usafiri wa daladala nikiwa naelekea Mwenge. Mara nikaona lori aina ya Mercesdes Benz tanker lenye tela lenye nambari za usajili T264BUC likija kwa kasi kama ilivyokawaida ya magari hayo kwenda mwendo kasi baada ya kuruhusiwa kutoka katika mataa ya Ubungo pamoja na kwamba hapo kuna vibao na alama elekezi zilizowekwa kwa ajili ya kuwaongoza madereva wakiwa katika eneo ilo wanapaswa mwendo gani.
Alama kama michoro ya punda milia ipo mita chache karibu na kituo cha daladala cha Riverside. Basi hilo lori likiwa katika mwendo kasi amadi dereva wa daladala akawa anaondoka kituoni na kuingia barabarani ndipo huyo dereva wa lori katika kuhofia kuwa angeweza kuingia ile Hiace kwa nyuma akapanda tuta linalotenganisha barabara.
Baada ya kulipanda tuta, lori likagonga kigingi au jiwe kubwa kisha likawagonga vijana wawili (Maaarufu kama Wamachinga) mmoja alikuwa anauza sticers na mwingine alikuwa amebeba DvD/VCD na Cd, kisha likaanza kuyagonga magari yaliyokuwa upande wa pili wa barabara moja baada ya lingine kwa haraka haraka nilivyoyahesabu yalifika sita lakini mawili aina ya Honda salon yenye nambari za usajiri T918BUC na Toyota Mark II nyeupe yenye namba za usajiri T133ADC yalikuwa yamefanywa chapati (tazama picha).
Shughuli za uokozi zikaanza kwanza kupitia raia wema baadaye polisi wakawasili kutekeleza majukumu yao. Hapa napo nilishuhudia mapungufu makubwa lakini kwa kuwa nataka kuzungumzia kinga ni bora kuliko tiba sito ongelea hilo la shughuri za uokozi Sheria za barabarani zipo lakini nani mwenye jukumu la kuzisimamia?
Nani mhusika nambari moja, namba mbili na nambari tatu? Nambari moja bila shaka ni polisi wa usalama barabarani. Swali la msingi hawa polisi wa usalama barabarani wanafanya kazi yao sawasawa? Ripoti ya Jaji Warioba imewatuhumu hawa polisi wa usalama barabarani kuwa ni wala rushwa wakubwa.
Mapendekezo yangu kazi hii wapewe MP wa JWTZ kwa sababu hivi sasa hakuna vita hivyo hawana kazi nyingi kama wakati wa vita. Wewe una maoni gani katika hii hoja ya kwamba wapewe wanajeshi tuone matokeo yatakuwa vipi.
Nawakilisha hoja.

Attachments
-
askali 1.jpg35.9 KB · Views: 178
-
Honda.jpg43.1 KB · Views: 173
-
honda 1.jpg36.9 KB · Views: 148
-
IMG00227-20111123-1400.jpg38.9 KB · Views: 146
-
IMG00228-20111123-1400.jpg42.9 KB · Views: 149
-
IMG00230-20111123-1402.jpg39.2 KB · Views: 132
-
IMG00232-20111123-1437.jpg42.8 KB · Views: 132
-
mark II.jpg37.8 KB · Views: 151
-
IMG00252-20111123-1513.jpg34.1 KB · Views: 130
-
umati2.jpg40.4 KB · Views: 127
-
IMG00242-20111123-1446.jpg45.1 KB · Views: 138
-
IMG00233-20111123-1439.jpg37.7 KB · Views: 127
-
IMG00235-20111123-1443.jpg46.3 KB · Views: 146