Ajali ya ndege: serikali isitutoe nje ya reli

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,603
29,743
Tarehe 06 Novemba 2022 Tanzania iliingia tena kwenye majonzi na simanzi kubwa baada ya ndege ya Precission kuanguka ziwani ilipokuwa inataka kutua uwanja wa Bukoba.

Tumepoteza Watu 19 huku kukiwa na sintofahamu kubwa ya namna serikali ilivyoshiriki kuokoa wahanga.

Ajali hiyo imemuibua raia shujaa ambaye alkiwa na wavuvi wenzake wenye vyombo duni walifanikiwa kufungua mlango wa ndege na kuanza kuwatoa abiria ambao endapo wangechelewa kutoka ingewezekana idadi ya vifo ingeongezeka. Katika maelezo ya msamaria shujaa huyo Majaliwa alisema kulikuwa na uwezekano wa kuwaokoa rubani na msaidiIzi wake endapo angeruhusiwa kuvunja kioo cha mbele cha ndege lakini alikataliwa na wataalam ambapo aliishia kuwapungia mkono wa kwaheri rubani huyo na msaidizi waliokwama kwenye cockpit. Hii hadithi inasikitisha sana.

Kiongozi wa nchi yupo kwenye Mkutano wa COP27 huko Misri amnapo angeweza kukatisha ziara yake kuja kuomboleza na Taifa kuwafariji wafiwa na wahanga lakini akamtuma waziri Mkuu ambaye alifika Bukoba na helikopta kutokea Mwanza.
20221108_062528.jpg
Wananchi wameilaumu serikali kwa kushindwa hata kurespond haraka kwenye uokozi wa ndugu zetu waliokwama.ndani ya ndege kwa masaa kadhaa.

Tarehe 07 Novemba 2022 serikali iliongoza mazishi ya kitaifa kuwaaga marehemu wa ajali hiyo ya ndege pale uwanja wa Kaitaba. Hqpo ndipo ilipofanya drama kubwa ili kuwatoa relini Watanzania wanaohoji uwajibikaji wa serikali kwenye eneo la maafa. Waziri Mkuu alitoa zawadi ya Tshs milioni moja kwa kijana mvuvi Majaliwa ambaye pia kwa maagizo ya rais alipewa ajira mara moja kwenye jeshi la polisi kikosi cha zimamoto na uokoaji.

Wataalam wa mipango ya mbinu mbinu serikalini wamehakikisha habari ya ajira na zawadi kwa majaliwa inafika kila kona ili kufunika hoja ya kitaifa kuhusu uwezo na utayafi wa serikali kwenye eneo la uokozi wa wahanga kwenye maafa mbaki mbali. Ikumbukwe kuwa hivi katibuni serikali haikuweza kushiriki kikamifu kuukabili moto uliokjwa unaunguza mlima Kilimanjaro ambapo raia walijitokea kuukabili moto huo na hatimaye Mungu akashusha mvua iliyosaidia kuuzima.

Sehemu kubwa ya wapiga ramli wa serikali na walamba asali wameshusha pumzi kubwa kupitia tukio la kumpaisha Majaliwa na wanahakikisha kwa gharama yeyote habari ya mvuvi Majaliwa inafunika story nzima ya ajali ya ndege ili kufunika uzembe mkubwa wa serikali hususani ofisi ha Waziri Mkuu kitengo cha Maafa kushindwa kuwa msaada kwenye majanga yanayoendelea kutokea nchini

TUTAFAKARI KWA PAMOJA
  1. Serikali ambayo imewekeza bajeti kubwa kwenye ununuzi wa mitambo ya kuchunvuza na kudukua raia wake ili kuwabaini wanaoikosoa serikali na kuwatungia sheria kali ya kuwadhalilisha viongozi
  2. Serikali ambayo inatumia vyombo vyake vya ndani kuwafuatilia raia wake na kuwakamata ama kuwaua wale ambao wanaonekana ni tushio kwa CCM kuendelea kushika hatamu
  3. Serikali ambayo imewekeza bajeti kubwa kwenye ununuzi wa mitambo na zana za kuwaumiza raia wake ili kuwatishia wasihoji wala kuandamana kushinikiza ama kulalamikia utendaji mbovu wa serikali
  4. Serikali ambayo inakopa bila ya kuwa msimamizi bora wa matumizi ya mikopo hiyo kwenye miradi lakini haijalli ukuaji wa deni la Taifa
  5. Serikali ambayo inatoa majibu ya vitisho kwa wanaohoji nankukosoa sera mbovu na ubanwaji wa demokrasia nchini
  6. Serikali ambayo ilipitisha sheria ya vyama vingi vya siasa lakini ikiivunja aheria hiyo kwa kudhibiti shughi halali za vyama pinzani huku Chama-Dola CCM ikipewa kipaumbele kufanya siasa bila hata kikwazo chochote.
  7. Serikali ambayo inabinya uhuru wa kutoa maoni huku viongozi wake wakitoa lugha kali zinazotishia wananchi wanaoikosoa
Serikali hii inaonekana imefikia ukomo wa fikra zake na inaweza isiwe na jipya zaidi ya kushika dola bila kuwa na mikakati na mipango chanya ya kuikwamua nchi kwenye mdodoro uliosababishwa na CCM

Najua kuwa hizi posts zangu za siku za karibunj zinaniweka doa kubwa ndani ya chama changu CCM lakini I must pay the price if possible kwa kuwa sitonyamaza nitaeneelea kuikosoa CCM kwa sababu kwa makusudi imelipeleka Taifa kwenye shimo kubwa la shokoa na Mtanziko mkubwa kijamii na kiuchumi.

Je utaipigia kura CCM 2025?
Kwa nini?
 
You got the point nilisema tangu jana kuwa huyu kijana kafanya kazi nzuri ila kwa sababu watanzania ni wasahaulifu "spinning" imefanyika wametumia story hii kukwepa maswali muhimu.

Kuna maswali mengi yanapaswa kujibiwa pia kujitafakari kuhusu "disaster preparedness"
 
Hapo kwenye disaster preparedness ni wazi serikali haina jibu na haitokuwa na jibu kwa sababu stream ya utafunaji wa fedha za maafa ni kansa inayohitaji kuikata CCM isijinasibishe na serikali ili itibike
 
Fimbo ya mbali haiui nyoka!

Kwa kuanzia tu, ilichukua muda gani kwa serikali kufika eneo la tukio?
 
Tarehe 06 Novemba 2022 Tanzania iliingia tena kwenye majonzi na simanzi kubwa baada ya ndege ya Precission kuanguka ziwani ilipokuwa inataka kutua uwanja wa Bukoba.

Tumepoteza Watu 19 huku kukiwa na sintofahamu kubwa ya namna serikali ilivyoshiriki kuokoa wahanga.

Ajali hiyo imemuibua raia shujaa ambaye alkiwa na wavuvi wenzake wenye vyombo duni walifanikiwa kufungua mlango wa ndege na kuanza kuwatoa abiria ambao endapo wangechelewa kutoka ingewezekana idadi ya vifo ingeongezeka. Katika maelezo ya msamaria shujaa huyo Majaliwa alisema kulikuwa na uwezekano wa kuwaokoa rubani na msaidiIzi wake endapo angeruhusiwa kuvunja kioo cha mbele cha ndege lakini alikataliwa na wataalam ambapo aliishia kuwapungia mkono wa kwaheri rubani huyo na msaidizi waliokwama kwenye cockpit. Hii hadithi inasikitisha sana.

Kiongozi wa nchi yupo kwenye Mkutano wa COP27 huko Misri amnapo angeweza kukatisha ziara yake kuja kuomboleza na Taifa kuwafariji wafiwa na wahanga lakini akamtuma waziri Mkuu ambaye alifika Bukoba na helikopta kutokea Mwanza.
View attachment 2409804Wananchi wameilaumu serikali kwa kushindwa hata kurespond haraka kwenye uokozi wa ndugu zetu waliokwama.ndani ya ndege kwa masaa kadhaa.

Tarehe 07 Novemba 2022 serikali iliongoza mazishi ya kitaifa kuwaaga marehemu wa ajali hiyo ya ndege pale uwanja wa Kaitaba. Hqpo ndipo ilipofanya drama kubwa ili kuwatoa relini Watanzania wanaohoji uwajibikaji wa serikali kwenye eneo la maafa. Waziri Mkuu alitoa zawadi ya Tshs milioni moja kwa kijana mvuvi Majaliwa ambaye pia kwa maagizo ya rais alipewa ajira mara moja kwenye jeshi la polisi kikosi cha zimamoto na uokoaji.

Wataalam wa mipango ya mbinu mbinu serikalini wamehakikisha habari ya ajira na zawadi kwa majaliwa inafika kila kona ili kufunika hoja ya kitaifa kuhusu uwezo na utayafi wa serikali kwenye eneo la uokozi wa wahanga kwenye maafa mbaki mbali. Ikumbukwe kuwa hivi katibuni serikali haikuweza kushiriki kikamifu kuukabili moto uliokjwa unaunguza mlima Kilimanjaro ambapo raia walijitokea kuukabili moto huo na hatimaye Mungu akashusha mvua iliyosaidia kuuzima.

Sehemu kubwa ya wapiga ramli wa serikali na walamba asali wameshusha pumzi kubwa kupitia tukio la kumpaisha Majaliwa na wanahakikisha kwa gharama yeyote habari ya mvuvi Majaliwa inafunika story nzima ya ajali ya ndege ili kufunika uzembe mkubwa wa serikali hususani ofisi ha Waziri Mkuu kitengo cha Maafa kushindwa kuwa msaada kwenye majanga yanayoendelea kutokea nchini

TUTAFAKARI KWA PAMOJA
  1. Serikali ambayo imewekeza bajeti kubwa kwenye ununuzi wa mitambo ya kuchunvuza na kudukua raia wake ili kuwabaini wanaoikosoa serikali na kuwatungia sheria kali ya kuwadhalilisha viongozi
  2. Serikali ambayo inatumia vyombo vyake vya ndani kuwafuatilia raia wake na kuwakamata ama kuwaua wale ambao wanaonekana ni tushio kwa CCM kuendelea kushika hatamu
  3. Serikali ambayo imewekeza bajeti kubwa kwenye ununuzi wa mitambo na zana za kuwaumiza raia wake ili kuwatishia wasihoji wala kuandamana kushinikiza ama kulalamikia utendaji mbovu wa serikali
  4. Serikali ambayo inakopa bila ya kuwa msimamizi bora wa matumizi ya mikopo hiyo kwenye miradi lakini haijalli ukuaji wa deni la Taifa
  5. Serikali ambayo inatoa majibu ya vitisho kwa wanaohoji nankukosoa sera mbovu na ubanwaji wa demokrasia nchini
  6. Serikali ambayo ilipitisha sheria ya vyama vingi vya siasa lakini ikiivunja aheria hiyo kwa kudhibiti shughi halali za vyama pinzani huku Chama-Dola CCM ikipewa kipaumbele kufanya siasa bila hata kikwazo chochote.
  7. Serikali ambayo inabinya uhuru wa kutoa maoni huku viongozi wake wakitoa lugha kali zinazotishia wananchi wanaoikosoa
Serikali hii inaonekana imefikia ukomo wa fikra zake na inaweza isiwe na jipya zaidi ya kushika dola bila kuwa na mikakati na mipango chanya ya kuikwamua nchi kwenye mdodoro uliosababishwa na CCM

Najua kuwa hizi posts zangu za siku za karibunj zinaniweka doa kubwa ndani ya chama changu CCM lakini I must pay the price if possible kwa kuwa sitonyamaza nitaeneelea kuikosoa CCM kwa sababu kwa makusudi imelipeleka Taifa kwenye shimo kubwa la shokoa na Mtanziko mkubwa kijamii na kiuchumi.

Je utaipigia kura CCM 2025?
Kwa nini?
Nani anawatoa kwenye reli mkuu? Ni umbea wenu huo waTanzania kutaka kurukia kila kitu ndiyo mnajitoa kwenye reli
 
Vifo vya abiria wa ndege ya Precision Air vimechangiwa na design flaw. Hii ajali ingehusisha ndege kama Airbus au Boein dreamliner huenda abiria wote wangetoka salama.
Ikumbukwe kuwa hizi ndege ili ziweze kuelea lazima mabawa yaguse maji. Bahati mbaya ndege za ATR na Bombadier mabawa yako juu ya fuselage wakati zile ndege kubwa mabawa yako chini ya fuselage.
Wito wangu kwa mamlaka na serikali kote ulimwenguni ni kuhakikisha hizi ndege ambazo mabawa yako juu ya fuselage hazitengenezwi tena.
Tujikite kutengeneza ndege ambazo mabawa yako chini ya fuselage ili ziweze kuelea kipindi itokeapo hitilafu zikalazimika kutua kwenye maji!

images (1).jpeg
 
Back
Top Bottom