Ajali YA Ndege Mbeya leo

Ajali YA Ndege Mbeya leo

tafadhali fanya haraka kutafuta hbr, kwani tunahisi huu mwaka wa shetani kama Temba alivyoimba.

1. ajali ya meli znz watu zaidi ya 200 wapoteza maisha
2. ajali ya bomba la gesi kupasuka-200 wapoteza maisha-kenya.
3. hbr yako ya ndege -----mbeya tz
 
aksante sana kiongozi kwa clarification<br />
Actually kujua chanzo cha ajali ya ndege mara nyingine si rahisi sana,,,,inachukua muda! maana hadi uchunguzi wa kiufundi ufanyike!
halafu nataka nijue sesina ndio ndege gani
 
[h=3]Michuzi blog: breaking nyuzzzzz: ndege ndogo aina ya 9J-BIO SESINA 206 yapata ajali jijini mbeya leo[/h]Ajali ya ndege namba 9J-BIO SESINA 206, imetokea leo asubuhi majira ya saa tatu eneo la Nanenane Uyole jijini Mbeya na abiria wanne wanusurika kifo na hakuna aliyefariki.Abiria walionusurika kifo ni pamoja JVER WAAK Umri wa Miaka 49 ambaye alikuwa Rubani, Raia wa Afrika Kusini, Bwana CHRISTIAN BASIL MMASI umri miaka 30, Ambaye ni Afisa Utawala wa mashamba ya Kapunga wilaya ya Mbarali, Balozi MOHAMMED RAMIA kabula leke ni Mmakua mwenye umri wa miaka 64, mkazi wa Masaki jijini Dar es Salaam ambaye ni mfanyakazi EXPORT TRADING na Bwana SUNNY TAYIR mwenye umri wa miaka 50 ambaye ni Mhindi na ni mfanyakazi wa EXPORT TRADING.Na chanzo cha ajali hiyo hakijafahamiaka mpaka sasa. Imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Bwana ANACLET MALIMBISA
 
halafu nataka nijue sesina ndio ndege gani
Ha ha haaa!
Preta bana!...kama unajua inavyoandikwa si umwelekeze aisee!
Mi nakumbuka tulitembelea kiwanja cha ndege tukiwa darasa la 6 mwaka 1966, na tukafundishwa kuwa inaitwa Cessna-206, 6-seater a/c.
 
Mbeya Yetu Blog: Mbeya Yetu: TAARIFA KAMILI YA AJALI YA NDEGE JIJINI MBEYA.. PICHA ZITAFUATA BAADAE




Ajali ya ndege namba 9J-BIO SESINA 206, imetokea leo asubuhi majira ya saa tatu eneo la Nanenane Uyole jijini Mbeya na abiria wanne wanusurika kifo na hakuna aliyefariki.


Abiria walionusurika kifo ni pamoja JVER WAAK Umri wa Miaka 49 ambayealikuwa Rubani, Raia wa Afrika Kusini, Bwana CHRISTIAN BASIL MMASI umri miaka 30, Ambaye ni Afisa Utawala wa mashamba ya Kapunga wilaya ya Mbarali, Balozi MOHAMMED RAMIA kabula leke ni Mmakua mwenye umri wa miaka 64, mkazi wa Masaki jijini Dar es Salaam ambaye ni mfanyakazi EXPORT TRADING na Bwana SUNNY TAYIR mwenye umri wa miaka 50 ambaye ni Mhindi na ni mfanyakazi wa EXPORT TRADING.

Na chanzo cha ajali hiyo akijafahamiaka mpaka sasa.

Imetolewa na Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Bwana ANACLET MALIMBISA






Kuna kitu sijakipata vizuri hapa, huu utambulisho wa polisi umekaaje?

1.Rubani ametambuliwa kama raia wa South Africa.

2.Christian Mmasi ametambuliwa kama afisa tawala wa kapunga bila kutaja utaifa wake

3.Balozi Mohamed Ramia ametambuliwa kwa kabila lake -mmakua

4.Bwana Sunny Tayir ametambuliwa kama mhindi,....!

Huh, kazi ipo.
 
Ha ha haaa!
Preta bana!...kama unajua inavyoandikwa si umwelekeze aisee!
Mi nakumbuka tulitembelea kiwanja cha ndege tukiwa darasa la 6 mwaka 1966, na tukafundishwa kuwa inaitwa Cessna-206, 6-seater a/c.

Huh, mkuu kumbe umekandamiza chumvi kiasi hicho??

Hivi hiyo Sesina ni chapa ya Urusi?
 
Ndege imepata ajali Uyole mbeya,lakin wamenusurika kifo!

Thanks kwa info. Siku nyingine ukipata habari kama una uhakika nayo ilete tu details zitaibuka zenyewe mbele kwa mbele. Usikatishwe tamaa na waliokuattack ama kukukosoa
 
[h=6]AJALI YA NDEGE NAMBA 9J-BIO SESINA 206 YATOKEA HUKO JIJINI MBEYA LEO ASUBUHI.http://networkedblogs.com/mZd1w abiria walikua wanne,hakuna aliye fariki ila majeruhi..mwenye taarifa zaidi atupe.
[/h]Nchi imeingiwa na nini?
au mzee anahitaji kubadilishwa.
 
Pole nyingi kwa waliojeruhiwa. Asante kwa taarifa mkuu
 
Poleni sana majeruhi, tunaamini Mungu atawaponya mapema ili mrejee kwenye kazi zenu za kila siku.
 
Hizi ndege ndogo inaelekea mazingira ya Mbeya ni magumu sana kwazo.
 
wanajf kwa mujibu wa habari ya saa saba mchana huu TBC TAIFA imeripotiwa kuanguka kwa ndege ndogo takribani kilometa tano kutoka uwanja wa ndege wa mbeya, cah kusahangaza eti jeshi la polisi linafanya uchunguzi kujua chanzo cha ajali. HIVI tanzania kweli jeshi la polis lina uzoefu wa kuchunguza ajali za ndege? kwa nchi za wenzetu waliotuzidi hata kiutaalamu jeshi bado haliwezi bali kuna vitengo maalumu vinavoundwa vikishirikisha marubani wa zamani na mainjinia wa ndege ndio wanaoweza kufanya utafiti wa ajali za ndege sasa hawa polisi wetu wengi hata ndege hawajawahi kupanda au kusomea muundo wake watawezaje kuchunguza ajali???
 
polen sana ndugu zangu. jamani tatizo nini mbona ajali nyingi zinaikumba afrika mashariki?
 
poleni majeruhi wote but i think huu ndio wakati hasa kwa wale viongozi wetu wa dini wafanye kazi kubwa sana ya kuliombea taifa letu kwa ujumla maana haya majanga ya ajali yanazidi kila kukicha.jamani tumuombe MUNGU na kutubu kweli ili hii hali ituondoke
 
Back
Top Bottom