Ajali ya ndege Bukoba: Nashangaa mpaka sasa si waandishi wa habari wala wadau wengine walioona umuhimu wa kupata maoni ya wataalamu wa hali ya hewa

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Tangu kutokea kwa ajali hii, kumekuwa na maoni mengi na watu mbalimbali kuhojiwa ili watoe maoni yao. Kinachonmishangaza ni kuwa, wakati chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni hali mbaya ya hewa(najua uchunguzi unaendelea) mpaka sasa sijaona waandishi wa habari wala wadau wengine walioona umuhimu wa kupata maoni ya wataalamu wa hali ya hewa ambao bila shaka wangesaidia sana kuongeza ufahamu wa nini kilitokea kuhusiana na hali ya hewa na hata kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wadau wakiwemo marubani na hata serikali yenyewe.

Watu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa ndio wenye dhamana na mambo ya hali ya hewa na ndio maana hata ofisi nyingi za Mamlaka ya Hali ya Hewa ziko katika viwanja vya ndege,hivyo kutotafuta maoni au ushauri wa wataalamu hawa katika swala hili, mpaka sasa kumenishangaza sana.

Mnapoongelea Mamlaka ya Viwanja Ngege(TAA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA) msisahau kuna Mamlaka ya Hali ya Hewa(TMA) wenye dhamana na maswala ya hali ya hewa.

Taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na mtu wa Control Tower, zimeandaliwa na wataalamu wa TMA na yeye kazi ni kumsomea tu rubani .

Ndege inapokaribia au inaptaka kutua au inapotaka kuruka, rubani hupatiwa taarifa za hali ya hewa na baahi ya taarifa muhimu ni kama speed na muelekeo wa upepo, air temperature, umbali ambao rubani anaweza kuona (visibility), hali ya mawingu (cloud cover), vitu vinavyoweza kuathiri visibility kama ukungu, mvua, n.k na ni kwa kiwango gani vina-reduce visibility.

Vile vile hali ya hewa inapokuwa mbaya(inapobadilika ghafla), taarifa maalumu ya hali ya hewa kwa marubani hutolewa ingawa uamuzi wa kutua ama kuruka hubaki kuwa ni wao kama marubani.
 
Back
Top Bottom