Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Kila mtanzania ni hazina ya Taifa, wazima na walemavu
Mbona huulizi walemavu wanahudumiwa vipi kwenye hii nchi?
usisahau kuwa nchi yetu ulikuwa inaongozakwa kua ALBINO sasa jiulize wenye ulemavu mwingine wakoje hali zao?
Nadhani hata tuliobaki tunaweza kupata somo kutokana na yale yaliyotokea. Kwa hiyo nadhani ni muhimu tukajadili hili kwa kina, si kwa maana ya kumshushia lawama marehemu, bali kupata funzo la nini kilifanywa vuisivyo na kuwa uwezekano wa chanzo cha ajali ile ili sisi tuliobaki tujiepushe kufanya kama hivyo.
Tulishajadili hili toka jumamosi.........mwacheni apumzike na ile ilikuwa ni ajali tu......hata Sokoine alikufa kwa ajali japo hakuwa na ulemavu
Ajali kama hii iliyokatisha maisha ya Regia Mtema, si mpango wa Mungu. Ni dhambi kubwa kusema kwamba huu ni mpango wa Mungu. Kama barabara ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro, ingekuwa ni ya njia nne, ajali kama hii ya Regia Mtema na nyingine nyingi zinazotokea kila wakati kwenye barabara hii zisingetokea.
Wakulu
Nimesukumwa kuandika haya baada ya kufuatilia tukio zima la ajali ya Mh. Mbunge ambaye sasa ni marehemu.
Mh. Regia alikuwa mlemavu wa mguu wa kulia.Gari aliyokuwa anaendesha kwa mujibu wa taarifa za jeshi la polisi lilikuwa halijafanyiwa -modification kwamba ni gari maalumu kwa ajili ya walemavu.
Sasa swali, ni mamlaka gani ilitoa leseni kwa Marehemu? wakati anajulikana kwamba ni mlemavu...... (ukizingatia kwamba kwa mujibu wa sheria zilizopo, hata ukiwa na makengeza huruhusiwi kupewa leseni)
Nauliza hili kwa uchungu tukizingatia kwamba Regia alikuwa ni hazina ya taifa...... mpaka lini tutaendelea kupoteza vijana wenye uwezo mkubwa wa kulisaidia taifa hili ...kwa kuruhusu uzembe,kutoheshimu sheria na mambo yanayofanana na hayo?
Ilikuwaje mfumo mzima kuanzia serikali kupitia vyombo vyake vya TRA, Trafiki polisi, ndugu, chama chake, marafiki zake, abiria aliokuwa nao kwenye gari kwa nyakati mbalimbali hawakuliona hili kwamba ni tatizo kwa marehemu kuendesha gari wakati yu mlemavu ? kwa nini hawakumkemea, hawakumshauri ....n.k
Sheria , kanuni na taratibu zipo kutulinda.....naamini TUNA TATIZO KUBWA KULIKO TUNAVYODHANI.....
Naomba tujadili objectively...bila jazba...
Ushabiki unatuharibu, na ukweli unaonekana kupotoshwa. Kifo cha Regia kwa vyo vyote kimechangiwa kwa vikubwa na Regia mwenyewe kwa hoja zifuatazo:
Kuna mengi tu ingawa yanafunikwa funikwa, lakini ukweli unabaki kifo hiki ni uzembe wa hali ya juu ambao unagusa hata vyombo na mamlaka ya sheria, usalama na utoaji leseni. Tusifanya kufuru kwa Mungu kwamba Mungu alipanga wakati mambo haya yanaweza kukwepeka. Mbona mmoja aliyenusurika katika ajili hiyo aliongea kuwa kilichomwokoa ni kuvaa ukanda, na possible wengi waliomo walifanya hivyo na ndio usalama wao. Tunajifunza mengi katika ajali hii na tuongee ukweli kwa uwazi kwani yanatufunza wewe na mimi kuwa makini tuwapo behind the wheel. Hata kama taifa halitutegemei kwa uwazi kama aliyokuwa mbunge, lakini ndugu, jamaa familia na marafiki tunakuhitaji, na bado Mungu amekujalia uhai una haki na kuwajibika kuulinda vinginevyo uzembe hautapokeleka kwa utetezi wa aina ye yote.
- Kuendesha gari akiwa mlemavu akitumia mguu mmoja alio nao tena wa kushoto
- Kutovaa ukanda wakati akiwa behind the wheel, maana yake alichomoka toka kwenye kioo cha mbele
- Kutokuwa na gari ambalo ni maalum kwa ulemavu wake
- Kutofuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na usalama wa over take, mwendo kasi nk
- Kutokuwa mfano wa kuigwa kutokana na wajibu wake kuwa mtunga sheria za nchi nii na kisha kuwa ndiye mvunjaji
- Kutomheshimu mwajiriwa wake (dereva wake) ni dalili ya ubinafsi
- Kupuuzi sheria za bima
- Hakuna hakika kama alikuwa na leseni ya kuendesha gari kihalali kutokana na utata wa ulemavu wake
- Kupuuzi utaratibu wa viongozi kuwatumia madereva wao
- Kujiona yuko juu ya sheria kwa hoja ya kuwa mbunge
mi bado sijaelewa logic unayojenga hapa ni nini??
je unauliza swali mamlaka gani iluruhusu yeye kuendesha gari???
au unataka kutuambia kuwa ni uzembe wake???
au unailaumu serikari???
anywai ni hivi 'MHESHIMIWA MBUNGE ALIYEKUWA NA ULEMAVU WA MGUU ALIPATA AJALI YA GARI ALILOKUWA ANALIENDESHA MWENYEWE, NA ALIFARIKI DUNIA HAPO HAPO! (Sasa hayo mengine yaache kama yalivyo, kama ni uzembe wake au serikali au dreva wake poa, mungu amuweke mahari pema peponi)
Mkuu Wayne Heshima Mbele
Nadhani ulikuwa na hoja nzuri lakini ukuifanya kikamilifu kwa kuweka ushahidi wa baadhi ya lawama/Shauku zako
1) Swali lako la pili unauliza ni mamlaka gani iliyotoa leseni kwa Marehemu
Nadhani kwanza ungetuwekea hiyo leseni ya Marehemu na tukaiona imetolewa ikiwa kwenye Category gani, maana najua leseni zote zinakuwa na sehemu ya kuonyesha mwenye leseni ana ugumu gani wa kuendesha gari, (Mlemavu, anavaa miwani nk)
2) umesema Polisi walilikagua gari na kuthibitisha kuwa halikufanyiwa marekebisho ya kuendana na mlemavu
hapa point kumbe sio tatizo kwa mlemavu kuendesha gari (na ndio maana wana leseni za kuendeshea), maana hata polisi wanalijua hilo na Marehemu sio Mlemavu wa kwanza kuendesha gari, kumbe tatizo ni gari alikuwa kwenye kiwango staili kwa mlemavu
Mimi nakubaliana na wewe kuwa ukiukwaji wa kanuni na sheria ulifanywa na MArehemu, kwa kutumia leseni yake kuendesha asichoruhusiwa, ni uvunjwaji wa sheria unaoonekana ni wa kawaida machoni pa watu, ni kama mtu mwenye leseni ya gari ndogo kuitumia kuendeshea malori nk
Pamoja na hayo yote, kwa mujibu wa waliopona hiyo ajali, ni kuwa hiyo ajali haihusiani na ulemavu hata kidogo, kama alikuwa anataka kuovertake na likatokea gari lingine mbele, hapo hata kama hakuwa mlemavu hali ingekuwa ni hiyohiyo tu,
Pamoja na kuwa na hoja ya kuwa kwa nini watu wa kwenye gari hawakumkemea kwa kuendesha gari, lakini nadhani wangemkemea zaidi kwa speeding, umakini wa kuangalia kabla ya kuovertake na vitu kama hivyo
ajali inakuwa na maana endapo umetimiza sheria zote za barabarani lakini ikatokea tu. kwa mfano umefunga mkanda, gari liko hali nzuri, umefuata sheria zote za barabarani, watu atasema kweli mungu ametwaa!!! ila hizi nyingine ni wewe kujitwalisha maana ukiwa barabarani lazima 100% brain yako iwe hapo hapo tu hasa kwenye long safari. Madereva wengine utakuwa hupo 120km/h then anakula kula au anapiga ma-story na abilia aisee!!! au anaongea na simu.... Sasa hapo wakuu si ni kum-beep islael.Nadhani ajali ni ajali tu. Mama wa kaya aliwahi kugonga mtu na msafara wake. Mumewe aliwekewa Mafuta machafu huko kaskazini. Then Gari lake tairi zilibuma huku Dar. Mwakyembe je Si alikuwa na qualified driver akala mzinga?
Kuna Mzee mwingine alikufa kwa ajali ya ndege Mbeya Kama sijakosea.
Hiyo ni mifano michache tu. Mchango wako haujengi. Angekuwa hajui kudrive asingefika hata huko Ruvu. Tumwache apumzike kwa Amani jamani.
Ingekua Busara ukaanzisha thread yako kuliko kuchakachua hoja iliyopo kwa kutumia hoja yenye msingi lakini tofauti.Kila mtanzania ni hazina ya Taifa, wazima na walemavu
Mbona huulizi walemavu wanahudumiwa vipi kwenye hii nchi?
usisahau kuwa nchi yetu ulikuwa inaongozakwa kua ALBINO sasa jiulize wenye ulemavu mwingine wakoje hali zao?
aiseeeeeeeeeeeee arifu a yu shua?wakati nachangia kwenye thread za kifo chake, niligusia suala hili japokuwa sikusema juu ya mamlaka. Nilisema yeye mwenyewe kasababisha kifo chake, kwani ni mlemavu halafu anaendesha gari MANUAL, ambayo inahitaji kutumia viuongo mbalimbali vya mwili kuliendesha.
pili nilizungumza kuwa, kitendo cha yeye kutokuwa na dereva kwa safari hiyo wakati tayari serikali inamlipa hela ya dereva tena wa daraja la juu la kuendesha viongozi wa serikali, nao ni ufisadi. kunyima vijana wenye daraja lessen C, kumemgharimu maisha, kumetugharimu watanzania kwani tulikuwa bado tunamhitaji tuendelee kupambana.
Mwisho nilisisitiza vyombo vilivyopewa mamlaka kusimamia sheria visiangalia sura ya mtu katika kusimamia sheria, japokuwa vinalalmikiwa lakini wasimame kama taasisi wawashitaki wale wanaotumia fedha za walipakodi kujinufaisha. Na waanze na wabunge ambao mpaka sasa wamekataa kuajiri madereva wenye sifa kuwaongoza safarini, huu ni ufisadi kwa wabunge
Nimependa comment yako mkuu, tuache mawazo finyu sisi binadamu!!uache kufunga mkanda, tuendeshe magari kwa speed kali tupate ajali useme Mungu amependa??? ni Mungu gani huyo anaependa watu wake wafe kwa uzembe!!!??
Uache uongozi wa chadema, wao wanashughulikia masuala makubwa kama Ufisadi na maandamano, usalama wa uhai wa mtu kama marehemu Regia kwao sio muhimu, ingekua muhimu wangemshauri awe na dereva japo kwa safari ndefu kama hizo.