Ajali ya Meli: "Taifa Msibani, Umoja wetu na Utu wetu shakani!" - Zitto Kabwe

Kuiwashutumu Vodacom Zitto amekurupuka. Kama kweli watanzania wangekuwa na majonzi kamam Zitto na wenye akili finyu kama za kwake wanavyotaka kutuaminisha ukumbi ungekuwa mtuopu na waandaaji kupata hasra, ili siku inginbe wajue utamaduni wetu. Lakini kama ukumbi ulijaa na waliojazana humo ni watanzania taifa halina majonzi yoyote kama ambvyo tusivyokuwa na majoniz wakati kila mtu akitumia dhamna aliyonayo kukwapua chake mapema na kuwaacha watanzania wengine wakipoteza maisha kwa kukosa huduma.
 
TBC na VODACOM wanastahili adhabu. Pia ni wakati muafaka serikali kujifunza kuwa makini. Kuna mabo mengi yanatokea
VODACOM wanastahili kwa kosa gani, kudhamini mashindano ambayo yameruhusiwa na yanafanyika kihalali kwa mujibu wa sheria za Tanzania? Huu ni unafiki mtupu, kama kweli watanzania walikuwa na majonzi ukumbi ungekuwa mtupu.
 
In theory usemayo ni sawa, lakini lazma utambue sisi ni nchi maskini. Wananchi wengi hawalipi kodi na mapato ya serikali ni kiduchu, sasa huezi kutegemea TBC1 itume chopper, huku ndio kuwa out of touch kwenewe.
Kila siku baada ya masaa matatu zipo ndege ndogo zinaondoka Dar kwenda ZNZ na abiria hulipa nauli isiyofika Shs Laki moja. TBC wanashindwa hata nauli hiyo kumpeleka ntu na camera?
 
Zitto siku hizi ni mzuri mno kujenga hoja nyepesi kueleweka na zenye mvuto wa haraka kama hizi. Nilikuwepo Bungeni siku ile asubuhi sana alipoamka na hoja ya Jairo kurudishwa kazini na WM kuonekana amedhalilishwa na hivyo angekuwa yeye angejiuzulu! Umaarufu una gharama zake Zitto. Chombo cha habari kama Tv bila picha kinatoaje taarifa iliyokamilika.
 




Wakuu CCM ni sehemu tuu ya tatizo. Kama sijakosea Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ya Zanzibar inaongozwa na Waziri toka chama cha CUF: Hamad Masoud Hamad. Ni karibu mwaka sasa tokea wachukue hii wizara and as you can see nothing has really changed.


"Trickle down effect" ya mismanagement katika political system baada ya muda mrefu kupita madhara yake yanatapakaa kila mahala, na ni vigumu hata ku-pinpoint moja toka jingine ili kulishughulikia in isolation.
CUF wamekuwa madarakani kama miezi 9 tu sasa. CCM wamekuwa in charge kwa kipindi kirefu, kama kungekikuwepo na nia ya dhati kutatua tatizo, tusingelikuwa tunaomboleza hii leo. Mkuu wangu, ni neglect ya muda mrefu pahala pengi ambayo iko directly linked na uongozi wa Taifa letu. Na ni CCM iliyo madarakani!
 
Kwa bahati mbaya mbaya sana hata CCM waliendelea na uzinduzi wa kampeni zao baada ya haya maafa kutokea
 
Zitto,

Umeonyesha upeo mkubwa sana wa uongozi. Lakini siku hizi Tanzania hakuna kitu kinachoitwa Kuwajibika. Kuna matukio mengi sana kama mabomu mbagala na gongolamboto na mengine mengi lakini hakuna hiyo tarbia za kuwajibika.
 
Kwa bahati mbaya mbaya sana hata CCM waliendelea na uzinduzi wa kampeni zao baada ya haya maafa kutokea
Tuliwahi kupata ajali mbaya sana ya treni jirani na Dodoma. SMZ na TVZ yake walifanya nini? Mlimwona Rais wa Zanzibar kule? Bara tumefanya zaidi. Tumepeleka milioni 300, tumepeleka majeshi ya waokoaji, JK akaenda kule badala kwenda Canada, bendera iko nusu mlingoti,......
 
Naona ule mpango wake wa kuondoka na nusu ya Chadema bado uko hai.... Anatumia kila opportunity kupandisha chat. Hotuba yake ya kufunga Wizara ya Fedha + hii = Big problem kwa Chadema in future
 
Huyo ndo zitto mnafiki wa kweli! ukimfata unauvaa mkenge. anailaumu vodacom na miss TZ bila kusema chochote kuhusu chama cha magamba kuendelea na fiesta igunga siku hiyo hiyo tena mapema zaidi kuliko muda ilipofanyika miss tz.

Sijui kwa nini taarifa ya zitto haijagusa kabisa fiesta ya CCM pale Igunga, anaficha nini? anamlinda nani? ana maslahi gani ccm? unafiki. huyo ismael jissu hukumuuliza wakati wanafunzi wanakufa maji sengerema na mabomu yanaua watu gongo la mboto tvz ilikuwa inarusha kitu gani? we nee
Hiii isue ichukuliwe kirahisi tuuu kama MABOMU YA GONGOLAMBOTO!
NI BAHATI MBAYA NA AJALI HAINA KINGA!
RIP KWA WALIOTUTOKA!
 
jaribu kuficha ujinga wako ndugu, hii habari inaweza kurushwa kama hivi, "habari tulizozipata sasa hivi na ambazo hazijathibitishwa ni kwamba meli moja iliyokuwa inasafiri kutoka unguja kwenda pemba imezama na kuua watu wengi. Habari zaidi tutawaletea kadiri tunavyozipata."

baada ya kufanya hivyo wanaweka maandishi yanayotembea wakati wote kwenye screen, huku wakifanya bidii ya kutosha kupata habari na kuzitangaza wakati huohuo. Lakini hawakufanya hivyo na jumamosi wakaendelea kurusha mashindano wa wakaa uchi kutoka mlimani city kana kwamba hakuna kilichotokea. Wnastahili lawama zote kabisa.
acheni utani jamani hawa tbc ni kawaida yao mmesahau kipindi cha mabooomu gongolamboto walizidiwa na mlimani tv!
 
Inawezekana tukiamua kuwafanyia mgomombaridi hao Vodacom na TBC wao ni wetu tuutake uongozi ujiuzuru au wawajibishwe na mamlaka husika
 
Mimi ni mpinzani wa mashindano ya urembo, lkn ktk hili Vodacom wanalaumiwaje?! Sijui sana mambo ya udhamini lkn kumbe ukidhamini mchezo wewe ndiye unakuwa na maamuzi makubwa kuuhusu? Na hapa Vodacom inalaumiwa kwa sababu ya hao waonyesha uchi au na kwa sababu pia ya League kuu ya vodacom Tz?! Maana mechi za VPL zimeendelea hata jana, ilaumiwe Vodacom, TFF au wizara ya michezo? Kuhusu TBC mi siku zote naichukulia kama tv ya ccm,siku zote naiona iko kinyume na wananchi, so sishangai kuwa waliendelea na ndombolo na viduku, kwa sababu imelalamikiwa na watu na taasisi mbalimbali kwa mda mrefu na haibadiliki. Angekufa kiongozi au mfadhili wa ccm mmojawapo tbc ingeandaa mpaka vipindi maalum. For the time being tbc ni ya ccm hadi hapo wananchi tutakapoamka..
 
UJAMAA NA UPEBARI ni vitu viwili tofauti, siasa za ujamaa zainajali UTU.....tumeingia wenyewe kwenye ubepari ambapo faida ina nafasi kubwa kuliko utu twalaumu....VODACOM...si wa kulaumiwa pekee,wadhamini wengine walikuwepo kama ...

NAO WANA NAFASI, WASHIRIKI NYIE MWAITA WALIMBWENDE.....WAPO WALIOTOA GARI LA MILIONI 80.....WHY VODA PEKEE?

TBC.... kama chombo cha habari lazima kikusanye taarifa iliyokamilika na kuirusha hewani,hawawezi kurusha TETESI NA UVUMI....when we judge them we have to be fair enough

Comment yako haifai kuingia humu kwa GT
 
Hilo jambo hata mimi limeniumiza sana kichwa kwani iliktwa kila nnapowasha tbc1 naona wanatukuza upuuzi tu na ushetani,ama hapakuwa na watu studio mitambo ilikuwa inajiendesha yenyewe? Kama ndo hali hii sijui kama tutafika
 
naamini TBC ndo alaumiwe zaidi .. ila kwa suala la vodacom anatakiwa kulaumiwa mratibu na mwandaaji ambaye ni ucle lundega na team yake kwani vodacom na tbl walikuwa wadhamini tu na kazi yao iliisha kabla ya siku ya shindano yaani kuta zawadi ya msindi atakayoshindania
 
Hivi mabomu ya Gongo la Mboto yalipolika kwa uzembe wa dhahiri kabisa, je haukuwa msiba wa kitaifa? Mbona shughuli za uzalishaji mali ziliendela kama kawaida? Umeona Miss Tanzania tu peke yake; kumbi zingine za burudani si ziliendelea kutoa burudani kama kawaida? Na wenye harusi zao je, nao pia walitakiwa kuahirsha sherehe za harusi zao na kupata hasara?

Nina wasiwasi sana na jinsi jamii yetu inavyoweza kupambanua mambo. Miss Tanzania ni biashara kama biashara zingine; watu wametumia gharama zao kuandaa, na watoa huduma wameshalipwa. Kusimama kwa dakika moja kuonyesha kuungana na waombolezaji inatosha. Mbona mechi ya Simba na Azam jana imechezwa tena wakati tayari Rais ameshatangaza siku 3 za maombolezo? Tuache chuki binafsi kwenye biashara za watu. Vodacom watapeleka misaada kwa wahanga wa ajali. FULL STOP!!
 
UJAMAA NA UPEBARI ni vitu viwili tofauti, siasa za ujamaa zainajali UTU.....tumeingia wenyewe kwenye ubepari ambapo faida ina nafasi kubwa kuliko utu twalaumu....VODACOM...si wa kulaumiwa pekee,wadhamini wengine walikuwepo kama ...

NAO WANA NAFASI, WASHIRIKI NYIE MWAITA WALIMBWENDE.....WAPO WALIOTOA GARI LA MILIONI 80.....WHY VODA PEKEE?

TBC.... kama chombo cha habari lazima kikusanye taarifa iliyokamilika na kuirusha hewani,hawawezi kurusha TETESI NA UVUMI....when we judge them we have to be fair enough
Unafikiri kwa kutumia malaio
 
Back
Top Bottom