Hapa lazima tuangalia kwanini ajali ilitokea na tuone ni vipi tunaweza kufanya ili isitokee tena au kuwasaidia waliokumbwa na huu mkasa..
Sababu ya ajali kutoka ni kujaza sana boti.., na lazima watu wajue kwamba kila boti/meli ikitengenezwa na kuanza kazi inakuwa na maboya ya kutosha kutokana na idadi ya watu amabo wanatakiwa kuingia kwenye chombo.., hivyo basi kwa Clouds kuongezea hayo maboya ni kama kusema kwamba watu waendelee kujazwa kupita kiasi na hawa wa ziada ndio tuwape maboya...
Jambo la maana ni kuhakikisha vyombo husika vinasimamia ili kuepusha meli/boti kujaa (na wanaweza kufanya hivyo kwa kuongeza vyombo vingi vifanye kazi ili kuepusha msongamano) pia inabidi kusaidia vyombo vya kuokolea kuwa na vyombo vya kisasa vya kutosha kama Helicopter, boti n.k.
Hivyo Clouds cha kufanya ni eitheir kuwasaidia waliopatwa na maafa kwa hali na mali au kuwabana wahusika wawajibike ili kuacha kujaza vyombo..., hili la maboya ni good gesture lakini sidhani kama itasaidia tatizo (sio kwamba kuna uhaba wa maboya na kama mmiliki chombo atashindwa kununua maboya basi inabidi abadilishe aina ya biashara)