Ajali: Watu watatu wafariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kugongwa na gari jijini Arusha

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,762
21,230
Kuna ajali imetokea hapo jijini Arusha maeneo ya Mount Meru hotel karibu naofisi za Zola, taarifa isiyo rasmi watu zaidi ya 4 wanasadikiwa kugongwa na kupoteza maisha.

Waliopata ajali inasemekana ni kina mama wafanya biashara pembeni mwa barabara ambapo gari aina ya saloon ndiyo iliyosababisha ajali hiyo ambapo kwa usalama wa dereva wake aliokolewa na askali waliofika hapo baada ya wananchi wenye hasira kutaka kumpiga.

Habari zaidi hapa hapa JF.

---------------------

UPDATE

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Arusha Jonathan Shanna, watu watatu wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya gari dogo kuacha njia na kuwaparamia

Inasemekana waliofariki dunia ni wakina Mama ambao walikuwa wanafanya biashara zao pembezoni mwa barabara

Dereva wa gari hiyo anashikiliwa na Polisi, ambaye baada ya kumpima walimkuta alikuwa amelewa
 
Ki usalama ni hatari sana, kila siku polisi wa usalama barabarani wanaliongelea hilo, lakini hawana jinsi, kwani kwa sasa lipo ki siasa zaidi, na jiwe kaishasema wasibuguziwe nani tena awaondoe? Hadi itokee ajari kubwa sana ndio itakuwa fundisho, wewe nenda pale mbagala hata sehemu ya magari kupita ni tabu, na wana jeuri hao!!
 
Hili la wamachinga kuvamia kufanya biashara pembezoni mwa barabara liangaliwe upya, unakuta watu wamepanga nyanya hadi gari zinakosa pa kupita RIP marehemu

Hawajali usalama wao kabisa,Hapa Arusha barabara ya kutoka france kona kwenda unga ltd inajazwa na wamama wafanya biashara na wala hawajali hilo,
Wapumzike kwa amani.
 
Hili la wamachinga kuvamia kufanya biashara pembezoni mwa barabara liangaliwe upya, unakuta watu wamepanga nyanya hadi gari zinakosa pa kupita RIP marehemu
Ni maeneo mengi yako hivyo kwa sasa, ingawa wanatafuta riziki lakini usalama wao ni muhimu ila wabishi mnoo
Innalillah wainnailillah raijuun
 
ma fox mmeongezeka hahahhaha natania you are right. Lugha inaharibika.
Hahaha yule ndo founder mrekebishaji!kiukweli mm nikiona mtu anaandika kiswahili kibovu huwa nakua mzito sana!sijui ni uvv wa kuhudhuria shule?yaan nawasubiri tu wanangu wawe wanaandika ovyo...🤣!nimejizatiti balaa!
 
Kuna lipumbavu linatafuta sifa za kijinga kuruhusu wafanyabiashara wadogo wadogo kuvamia barabara! Hii siyo sawa kwa usalama wao!
 
Back
Top Bottom