Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

Tatizo la ajali hàlitaisha kwa utaratibu wa kukusanya mapàto wakati huohuo kuzuia ajali lazima tuchàgue.moja kati kukusanya mapato ya serikali au tuzuie ajali. Speedgavaner ziliishià wapi,road time table ziliishia wapi n.k.ebu tuache dili tupambane na ajali.turudie mfumo sheria za Cap 169 .
 
Basi la Dar Lux limepata ajali usiku huu saa sita hapo kibaha limekwaruzana na Semi trailer abiria wote wapo salama hakuna majeruhi. Wahusika na uokoaji wapo eneo la ajali
 
Hizi ajari zimetosha jamani.
Halafu hii kitu ya magari kuwaka moto nadhani kunashida upande wa umeme wa magari mafundi wetu muwe makini
 
Kuna haja ya kubadili mitizamo, jinsi tunavyoangalia na kuendesha mambo yetu. Nimeangalia leo eneo la pale Ubungo mataa na ujenzi unaoendelea nikabaki na maswali lukuki. Dereva anatoka Kimara anafika Kibo anaingia service road achilia anakuja kutaka kulazimisha kuingia barabara kuu pale Ubungo maji. Kwa wingi wa magari yanayopita njia hiyo ya kuchepuka na haya yanayobakia njia kuu, wote wawili wanaishia kupoteza muda pale Ubungo na wengine wanaishia kukwaruzana.

Nahisi kwa hili bado madereva wana-beep ndugu zetu wa usalama barabarani ili siku wakiwatembelea eneo hilo walalamike kwa tiketi watakazopewa. Pia wanasababishia wajenzi wa barabara jipya usumbufu usio wa lazima.
 
Utaratibu wa kutoa leseni uwe kama zamani lazima mtu apitishwe na police traffic bila longolongo wala rushwa hakukidhi arudi kusoma tena,leseni zinatolewa kama birth certificates ?!
 
Nikufikiri nje ya box tu ndicho kitakachoepusha ajali. Nitatoa sababu 3 tu za muhimu:
1. Ongeza mwendo (speed) kutoka wastani wa 80 kwa saa kwenda 100/ph. Lengo ni kuongeza ufanisi barabarani na kuruhusu magari yafike mapema. Itasaidia pia kupunguza msongamano barabarani na kuepuka madereva wengi kulazimisha ku-overtake. Think about it. Kama magari yana speed ya 240 au 180, kwa nini kuweka mwendo wa wastani wa 80/ph? Yaani kweli nchi inajivunia kujenga barabara za kisasa, lakini mtu hawezi kusafiri umbali kwa kilometa 1200 kwa masaa 18? This is just ridiculous.
2. Ondoa matuta yote barabarani: Ni upuuzi. Yanaleta usumbufu si wa lazima. Yanachosha na kufanya safari kuwa ndefu. Yanasababisha uharibifu wa magari n.k. Ukisafiri Dar - Sumbawanga unaruka matuta zaidi ya 5,000. Ili uruke tuta moja, unalazika kupunguza mwendo hadi 10/ph. ukiruka matuta 5000 unakuwa umepoteza kilometa nyingi sana. Think outside the box.
3. Ondoa makazi ya watu barabarani: Sasa tunalalamika mwendo wa magari kwa sababu tumeruhusu shughuli za watu kuhamia barabarani. Kila mtu anakimbilia barabarani. Biashara, makazi, mifugo, shule, hospitali n.k. It is just crazy. Matokeo yake tunalazimisha kupunguza speed kila mahali eti kwa ajili ya usalama. Bullshit.
4. Tumia treni kusafirisha mizingo badala ya watu. Treni zetu za kizamani zinazotumia siku mbili kwenda mwanza na kigoma, zinafaa zaidi kusafirisha mizigo na si watu. Zitumie kwa ajili hiyo na kuondoa idadi kubwa ya malori barabarani. Katika karne hii, hakuna sababu ya kusafirisha abiria kwa treni iliyotengenezwa kwaka 1900. Nani ana muda? Kila mtu anapigana na muda. Kila mtu anataka kufika mapema. Ni wajinga tu wanaoweza kufikiri kuna mtu anafurahia mwendo wa polepole na kukaa siku nzima barabarani. Kama watu wangekuwa na uwezo, asingekuwepo mtu anayeweza kusafiri kwa masaa matano au sita kutoka Dar kwenda Morogoro. Think outside the box.

Endelea kufikiri nje ya box. Hicho ndicho kitakachosaidia. Mawazo yale yale kila mwaka haisaidii kitu.
 
What we need isimproved regulations kwenye governance ya motor vehicle transportation.

1. 100% Liability ya reckless driving iende kwa dereva na owner wa Gari, pikipiki, basi na Lori : this means:- Bima za magari zipitiwe na kuwe na breakdown ya liability ya causing an accident, including footing all expenses (medical, funeral, car repair and replacement) for the driver who is at fault.

2. Reclassification ya leseni za udereva na kuweka masharti magumu na requirements. Wanaoendesha abiria, wanaoendesha mizigo ya kawaida hata kwa uzito na aina ya cargo (hazard versus non hazard)

3. Leseni zote za udereva ( Gari, Lori, trekta, pikipiki, magreda etc) ziwe na 2 year limit kisha renewal ambapo lazima recertification ifanyike (point ya 4) na driving record kutoka Usalama Barabarani na kampuni ya Bima zitoe points. Good driving record Iwe incentive ya low premium kwenye Bima. Bad driving record premium ziwe kubwa na ikibidi kufungia leseni.

4. Recertification and testing. Madereva wa magari ya abiria na mizigo regardless ya idadi ya watu, aina na uzito wa mizigo lazima kila 2 or 3 years waende kwenye designates shule ya udereva ya Mkoa, kanda au Chuo cha Usafirishaji for recertification na testing, then wapate renewal ya leseni.

5. Annual vehicle inspection kabla ya registration kuwa renewed. Fitness ya Gari ifanywe na certified mechanics (si polisi wa Usalama Barabarani), kuanzia body, electronics, drivability, emissions, suspension-springs, brake system, lighting system, Matairi. Kuna mafundi wengi wa kutoka Veta, Technical colleges na NIT, kuwe na special program kwa kila fundi na garage ya vehicle inspection for road worthiness. Gari liki-pass inspection, na proof of insurance , a digital certificate inatumwa TRA ambapo wata-issue renewal ya registration. Hiyo registration na proof of insurance ifike mahali tutumie ICT ziwe kwenye Database ambayo ita link Insurance company, service stations za vehicle inspection, na Usalama Barabarani. Ukisimamishwa they can link the digital certification ya Gari, bima na leseni ya udereva na driving records. Hapa you kill to birds with one stone: unazuia Rushwa kwa polisi na kufanya fine ziwe captured electronically including driving record za offender, pili unaongeza efficiency ya Polisi wa Usalama Barabarani kwenye traffic na road violation management.

6. Polisi wa Usalama Barabarani wawe trained na wApate annual certification ya oversight ya mfumo mzima wa uendeshaji magari na necessary knowledge wafanye kazi more efficiently.

7. Driving record; hapa bad driving record na poor score za recertification na testing zilasimishe dereva kuwa na high premium ya Bima na kulazimishwa awe na full coverage including liability.

8. Madereva wa malori na mabasi- public transportation ( teksi, bajaj, pikipiki) lazima wakati wa renewal ya leseni wafanyiwe medical test ya macho, reflexes, drug/substance and alcohol usage/abuse kabla ya kupewa pass grade to renew leseni.

Ukiweka mfumo kama huu, kisha watu wakajua they will be responsible zaidi ya makosa ya Barabarani na fines... udereva utanyooka na kupunguza recklessness na neglect inayofanywa.

Kuongeza accountability kuokoa maisha ya abiria na mali ni through clearly refining responsibility na monetary liability kwa dereva na owner wa vehicle.

That is better solution kuliko kutumia age as qualifier ya kuendesha magari more responsibly!
 
Mabasi na Malori yafungiwe gps system mwendo wao uonekane kwenye screen akizidisha speed faini milioni 1 kwa kila kosa. Ila kwa Hali ya sasa bado hatujafika inavyotakiwa udhibiti kamili. Mchana wanatembea kwa Sheria usiku wanakimbiza Kama kawaida maana hakuna trafiki
Wenye mabasi na malori watawabana madereva wao ili wakifanya makosa madereva walipe makosa yao wenyewe
 
Mchango wangu wa kupunguza ajali ni kujifunza kwa wenzetu. Mimi nimebahataika kusafiri nchi mbali mbali za nje kusini mwa bara letu la Afrika na Uingereza, Uholanzi na Marekani. Kwa wenzetu hawa wana magari mengi kuliko sisi ingawa pia barabara zao ni bora zaidi kutokana na uchumi wao. Lakini wamepunguza sana ajali kwa kutenganisha barabara kwa kuwa waligundua kuwa asilimia kubwa za ajali zinatokana na ku-OVERTAKE (kulipita gari lililoko mbele yako kwa spidi kubwa, kabla ya kurudi upande unatakiwa uwe unakutanan na gari lingine linatoka upande wa pili. Barabara kuu za wenzetu (Highways) zote zimetenganishwa, magari yanakwenda upande moja tu hukutani na gari linalotoka upande wa pili. HILI PEKEE LIMEPUNGUZA AJALI KWA ZAIDI YA ASILIMIA 65. Ni kweli kuwa na barabara zilizotengwa ni GHARAMA KUBWA lakini tukianza kidogo-kidogo tutajikuta tuna Highway za kweli za upande moja tu. Hapo ndipo tutaweka SPEED CAMERA barabarani na alama zinazoonyesha kuwa mbele yako kuna Camera angalia mwendo wako, ukizidisha speed iliyowekwa UTAIKUTA FAINI NYUMBANI KWAKO WALA HUHITAJI KUWA NA ASKARI WENGI BARABARANI. Huo ndio ustaarabu wa wenzetu. Sisi, ninaona tunawatesa sana askari wetu ambao ni wachache kudhibiti mwendo kila siku barabarani. Huo ndiyo mchango wangu kwa leo.
 
Huu ndo ukweli pekee niliowai kukutana nao kuhusu ajari nchini. Asante kwa kuhalalisha nilichokuwa naamin siku zote ingawa sijafika ulaya. Umetenga tafiti zenye kachumbari ya kisiasa na utafiti halisia. Nitaongeza nyama kwenye hoja hii nikitulia.
 
Hii comment imenifikirisha san
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok baadhi uko ushauri wako unafaa ,ila nyongeza na kusisitiza leseni za udreva ziwe recorded ikitokea dreva anasababisha ajali kwa uzembe wake Mara mbili afutiwe leseni yake na asiluhusiwe kupata leseni nyingine ,2-ajari zilizo jeruhi au kuua Sheria iwe kali zaidi na viwango kuhusu faini iongezeke na Sheria itamke majeruhi alipwe fidia kuanzia 6 mil-12mil na bima isihuke kulipa kwa kuwa Kuna usumbufu mwingi na wenye magali huwa na viburi kwa kuamini bima itadaiwa ,walipe wao na gali litaifishwe kabisa kukomesha jeuri za wamiliki baadhi wasio na utu hasa pindi gali zao zikisababisha ajari ,

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hahaha roho ya kimaskini katika ubora wake. Mambo ya uswahilini - mtu anatamani apate ajali ili alipwe. Kwa vile bima kuna usumbufu basi alipwe na mwenye gari maana hapo atapata chake chap chap.

Roho ya kimaskini sana. Hongera!
 
Akizungumza jijini Dodoma wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu usalama barabarani, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani na Mwenyekiti wa Kamati ya Bloomberg Deus Sokoni alisema kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeendeea kutoa elimu kwa umma pamoja na uboreshaji wa miundombinu ili kupunguza ajali na vifo kwa watanzania.

Mrakibu Msaidizi wa huyo wa Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani na Mwenyekiti wa Kamati ya Bloomberg Sokoni alisema “Barabara nyingi zinazojengwa hivi karibuni zimekuwa zikizingatia viwango vya ubora vyenye kukidhi mahitaji ya watumiaji wote wa barabara ikiwemo watembea kwa miguu”

Alifafanua zaidi kuwa siku za nyuma barabara hazikuwa zikijengwa kwa ubora wa kuzingatia watumiaji wote wa barabara mfano wa barabara ya Dar es salaam iliyopo jijini Dodoma, ambayo imesababisha ajali mara kadhaa.

Aidha, Mrakibu Msaidizi huyo wa Polisi ametaja jitihada nyingine za Serikali za kupunguza ajali ni pamoja na ujenzi wa barabara za mzunguko na mchepuko ambazo zinasaidia kuondoa msongamano wa foleni katika majiji mbalimbali nchini.

Baadhi ya miradi ya Serikali inayoendelea kutekelezwa kwa lengo la kupunguza ajali na foleni nchini ni pamoja na ujenzi wa barabara za mzunguko ndani ya Dodoma yenye urefu wa kilomita 39 pamoja na barabara za mchepuko zinazojengwa katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.

Naye, Mwendesha pikipiki wa jijini Dodoma Amos Majenda alisema kuwa Serikali imesaidia kupunguza ajali kwa kutoa elimu kwa umma kuhusu usalama barabarani ambayo inawafikia watumiaji wengi wa barabara.

Majenda alisema “Serikali imejitahidi kutoa elimu si kama kipindi cha nyumba ambapo ajali zilikuwa nyingi zaidi, ajali zinazotokea hivi sasa ni kwa sababu watu hawazingatii sheria za usalama barabarani na hivyo madereva wanaendesha vyombo vya moto kwa mwendokasi na kutovaa kofia ngumu kwa waendesha pikipiki pamoja na abiria”

Mafunzo hayo yanayotolewa kwa waandishi wa habari kuhusu usalama barabarani nchini yana lengo la kuwajengea uwezo waaandishi wa habari ili waweze kusaidia kufikisha elimu kwa umma, sambamba na kutoa mapendekezo yatakayosaidia kutatua changamoto za ajali za barabarani nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…