• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2008
Messages
8,771
Points
2,000
SMU

SMU

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2008
8,771 2,000
Hivi karibuni na hata siku za nyuma tumeshuhudia malumbano kati ya wamiliki wa mabasi ya abiria kwa upande mmoja na serikali (Polisi, Sumatra) kwa upande mwingine juu ya ulazima wa kufunga vidhibiti mwendo (Speed Governor) kwenye mabasi.

Wamiliki wa mabasi wanasema speed governor hazijasaidia kupunguza ajali za barabarani. Na zaidi wanaona msisitizo wa serikali wa kufunga speed governor unamsukumo wa kibiashara zaidi kuliko kupunguza ajali.

Je ni kweli speed governor hazisaidii kupunguza ajali? Kama hazisaidii, je nini kifanyike kupunguza ajali za barabarani?
------------Ndg wanabodi Heshima kwenu..

Bila shaka vifo vingi vinavyotokea kwa kiasi kikubwa hivi sasa ni kutokana na ajali za magari barabarani hasa Mabasi..

Tunaipongeza serikali kwa hatua mbalimbali ambazo imekua ikichukua ili kukabiliana na Changamoto hii kubwa japo kwa kiasi kikubwa bado ajali ni janga kwa nchi yetu..

Kwa kua akili ni nywele na kila mtu anazake,nami pia naomba kuwashirikisha fikra nilizonazo kama ifuatavyo..

1)SERIKALI IANZISHE VYUO MAALUMU KWA AJILI YA MAFUNZO YA UDEREVA WA MAGARI YA ABIRIA PEKEE..

Serikali na sio vyuo binafsi vianzishe vyuo maalumu kwa ajili ya Madereva wa Abiria pekee...
Hii itasaidia kupunguza madereva wa Mtaani wanaopiga dayworker kisha baada ya Muda wanaendesha mabasi ya Abiria.

Nimesema vyuo maalumu na wala si VETA wala vyuo binafsi Kutokana na sababu kua sasa ,VETA na vyuo vingine binafsi vimekosa credibility yaani mtu yeyote anaweza pata leseni hata kwa magumashi ilimradi awe na pesa..

Lakini pia ili mtu A-qualify kusomea udereva wa magari ya abiria awe amesoma mpaka kidato cha nne na awe amefaulu ili kupata watu makini wanaojielewa na si kuokoteleza hadi STD VII kama ilivyo sasa.

2)KILA BASI LISAFIRI NA ASKARI WA BARABARANI ANGALAU MMOJA:

Sio lazima askari aanze mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari...kunaweza kua na utaratibu wa askari maalumu wa barabarani kupokezana kila wilaya ambako gari hiyo itapita..hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kum-control driver hivyo kufata sheria zote za barabarani kama inavyopaswa.

3)MISHAHARA YA MADEREVA IBORESHWE

Hii itasaidia watu wengi kuwa motivated na kupenda kazi ya udereva ma mabasi hivyo kupata watu wengi wanaoqualify,hii inamana mtu aiendeshe gari kwa kua ameona ndo sehemu ya kutokea bali udereva uwe tamanio la mtu mwenyewe.

Wapewe pesa ya kutosha na posho juu ili kumfanya Dereva afurahie kazi yake na kupunguza msongo wa mawazo..

4)MISHAHARA YA ASKARI WA BARABARANI IBORESHWE

Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa askari hawa kutoshawishika kuchukua pesa ndogondogo wanazopewa njiani hivyo kupelekea kufanya kazi zao kwa uaminifu na umakini wa hali ya Juu.

5)ASKARI WA BARABARANI WAPUNGUZWE

Wingi wa Askari wa barabarani waliopo hivi sasa haimanishi ni kuboresha utendaji na udhibiti wa ajali barabarani..unaweza kua na askari wachache na wakafanya kazi nzuri yenye zaidi,iwapo madereva hawataokotwa mitaani,wakalipwa pesa vizuri na askari nao wakalipwa pesa vizuri hakika makosa barabarani yatapungua kwa kiasi kikubwa..hii ina apply kwa madereva wa magari yote barabarani...

Iwapo adadi ya askari barabarani itakua ndogo itakua rahisi kuwa hudumia financially na kwa pesa nzuri zaidi.
Nashauri askari barabarani walipwe kuanzia milioni 1 kwa Mwezi.
Utitiri wa askari barabarani haimanishi ndio uimarikaji wa utendaji kazi.

6)UKAGUZI WA MABASI YA ABIRIA KABLA YA SAFARI UIMARISHWE..

Ukaguzi wa maramojamoja unaofanywa na askari wa barabarani kwa sasa unamapungufu makubwa..
Pawe na kikosi kazi maalumu ambacho kazi yake ni kukagua mabasi yote ya abiria siku moja kabla ya safari na gari hiyo iwe na alama kua imekidhi vigezo vya kusafirisha abiria kesho yake..Hii itasaidia hasa kupunguza ajali zitokazazo na uchovu wa magari yenyewe hasa yale yanayounga safari bila kupumzishwa..
ikiwa na pamoja na kumpima dereva kabla ya kuanza safari kama hatumii madawa ya kulevya wala kilevi chochote..

7)SUMATRA WASIFANYE KAZI KWA MATUKIO PEKEE
SUMTRA Wasisubiri kupaza sauti katika kuwaambia umma kua nauli zitapanda kutokana na bei za mafuta kuongezeka,na wasisubiri mpaka matatizo yatokee ndo wajitokeze kwa waandishi wa habari kama wanavyofanya hivi sasa.SUMATRA Ifanye kazi yake ipasanyo na isifanye kazi kisiasa...

Nimesema ni mawazo tu sio msaafu wala Biblia unaweza kosoa au kuboresha kwa Mtazamo chanya ili kutoa mawazo sahihi kisha yafanyiwe kazi na mamlaka husika.

Karibuni kwa Mawazo chanya pia.

Mpangawangu said:
Kwanza kabisa nikupongeze kwa kuguswa na hili na kutuletea mada yanye tija kwa kila mmoja wetu,nategemea kuwaona watu mkiweka maoni yenu hapa kuliko kushabikia siasa zinazojadili watu badala ya mijadala yenye tija kama hii.

Naungana na yote uliyoyasema isipokuwa hilo la mabasi kusafiri na Askari.

Mawazo yangu ili kudhibiti ajali ni lazima kwanza kutambua vyanzo vya ajali,

pamoja na vyanzo kuwa vingi lkn mwendo kasi na uzembe wa madereva ndio chanzo kikuu cha ajali za barabarani.

Suluhisho ni kuwapangia muda madereva kufika kwenye vituo.

Mfano mabasi yaondoke Dar saa 12.00 alfajiri na yafike morogoro saa 4:00 yafike Dodoma saa 8:00,yafike manyoni saa 9:30,Singida Saa 11:00,Misigiri saa 12.30, Igunga saa 1:50,Nzega Saa 2:30 na hatimae kahama saa 4:00.

Masaa hayo yapangwe kitaalamu na watu wa sumatra baada ya kujiridhisha umbali toka eneo moja kwenda eneo jingine,

Kila kituo kiwe na askari ambao wapo serious na kuwepo na utaratibu kama ule wa treni wa kupewa line clear,hivyo mtu atachukua kibali maalum mahala anapoanzia safari kinachoonyesha muda na atapaswa kukabidhi kibali hicho kwenye kituo cha mbele na kupewa kingine kinachomruhusu kuendelea na safari,afanye hivyo mpaka mwisho wa safari yake,.

ili kuepusha usumbufu maeneo vinapotolewa vibali pawepo na vyoo pamoja na hotel za kula chakula,lengo ni kutumia mudaa wa kuonyesha kibali huku abiria wakiruhusiwa kuchimba dawa na kupata chakula,hivyo hakutakuwa na malalamiko,

Kama hilo halitoshi tunaweza kuyatumia maeneo mizani kama check point ya muda wa kuwasili eneo husika.

tukifanya hivi italeta self control ya madereva ,adhabu yake iwe kuahirishwa safari na abiria kuwekwa katika mabasi mengine kwa kibali maalum na dereva kuwekwa ndani mwezi mmoja na gari kufungiwa kusafirisha abiria kwa muda wa mwezi mmoja.

kama tutafanya hayo hakika hakuna dereva wala mmiliki wa gari atakaefika eneo husika kabla ya wakati.

Kufanya hivyo kutawafanya madereva kutembea mwendo wa kawaida na hivyi kupunguza ajali kwa kiwango kikubwa.

Pendekezo hili ni baada ya safari yangu toka Dodoma,gari ya kwanza kufika Dodoma ilikuwa campuni ya KISBO ikiduatiwa na Leina na CITY BOY.

Hizi ni basi zilizojizolea umaarufu kwa kukimbia kupita kiasi kiasi cha kufika kahama saa 12:30 badala ya saa tatu usiku.

Tulipofika manyoni walisimama petrol station na kutueleza abiria kuwa tunasubiri muda wa kufika Singida.

ilikuwa saa 7:20 za mchana na singida tulipaswa kuingia kuanzia saa 10.30 au zaidi ya hapo.

Hivyo tulilazimika kukaa muda wa saa moja na nusu ndipo tukaendelea na safari,

Gari zoote zilizotoka Dar zilikuwa kama msafara na hakuna aliethubutu kukimbia,waliogopa faini kubwa ambayo hutozwa singida endapo Gari itafika kabla ya muda uliopangwa.

Mwisho ni kwetu wapiga kura ambao ndio wahanga wa ajali hizi,tusiwachague tena wafanyabishara kuwa wabunge wetu,maana wengi wao hutumia fursa ya vyeo vyao kuwafanya hata askari Polisii wayaogope magari yao.

Chrizant Kibogoyo, post: 21072131, member: 380599"]KUNA UHUSIANO GANI KATI YA VYETI ALIVYONAVYO DEREVA, UJUZI ALIONAO DEREVA, KIPATO HALALI APATACHO DEREVA, NA ONGEZEKO LA HIZI AJALI ZA BARABARANI?

Kwa muda mrefu kama taifa tumekuwa tukijaribu kupunguza ajali za barabarani kwa kutumia mbinu za askari wa usalama barabarani kuwabana madereva. Japo yapo mafanikio, lakini kushindwa kwa sekta/idara zingine kushiriki kupambana Na ajali barabarani husussn zinazohusisha mabasi ya abiria kuna punguza mafanikio hayo.

Katika mchezo wa soka kuna msemo maarufu kuwa "Football is a game of mistakes" Na inadaiwa karibu magoli yote yanayofungwa katika mchezo huo utokana Na kosa/makosa ya wachezaji wa timu iliyofungwa. Hivyo basi kama kila kosa lingeweza kusababisha maafa, majanga,misiba na simanzi kama makosa ya kibinadamu afanyayo dereva. Dunia/nchi vingekuwa na katika wakati mgumu sana.

Hivyo basi dereva ana nafasi ya kipekee katika Jamii. Je ni kweli Jamii zetu zinatambua hilo? Chukua mfano wa kosa/makosa ya kibinadamu aliyofanya dereva mwenzetu wa basi la wanafunzi lililopata ajali huko Karatu. Kosa/makosa take yalisababisha simanzi nchi nzima, watu 33 wakapoteza uhai Na madhara mengine mbali mbali.

Ni kwanini jitihada kubwa za kikosi cha askari wa usalama barabarani zinashindwa kupunguza kwa uendelevu tatizo hili (yaani hata zisipokuwepo tochi, pasiwepo ajali za mabasi ya abiria)?

Kwa mtazamo wangu kutokana na uzoefu nilioupata nikiwa kiongozi was madereva wa mabasi. Mchawi ni mfumo wetu wa usimamizi was sekta ya ussafirishaji unamfanya dereva was basi la abiria kuwa mtekelezaji muhimu wa ukuzaji mapato ya kampuni Na yeye binafsi.

Kutokana na upungufu huo dereva w basi kipaumbele chake cha kwanza in mapato ya kampuni ili aweze kuendelea kuwepo katika ajira hiyo kupitia kushindana kuipatia kampuni abiria zaidi. Pili ni kuongeza kipato chake binafsi kwa kuwa ujira wao ni Mdogo sana kulinganisha na majukumu yao na umuhimu wao katika Jamii. Tatu ndio hufuata kutumia ujuzi wao vyema na Nne ndio kuzingatia n kutii sheria za usalama barabarani. Mfano hai ni ajali za hivi karibuni za mabasi ya Ally's Na BM coach.

Mfumo wa uendeshaji wa BRT unamfanya dereva kipaumbele chakeiwe ni kiwe kutii na kuheshimu taa na alama za vivuko vya waenda kwa miguu n.k ili aweze kuendelea na ajira yake. Hii ni kutokana ukweli kuwa dereva was BRT sio sehemu ya utekelezaji wa mipango ya kukuza mapato ya kampuni kupitia ushindani wa kupata abiria zaidii.

Tukiondoa umachinga ktk sekta yetu ya usafiri wa umma kwa kuwepo utitiri wa kampuni za mabasi hususan kati ya mkoa mmoja hadi mwingine. Na badala yake tukawa na professional passengers operators wenye uwezo wa kuwekeza ktk yafuatayo:- a) Mabasi ya kisasa kulingana Na miundombinu yetu (b) Raslimali watu yaani madereva, makondakta, mafundi n.k wenye ujuzi Na weledi was kutosha (c) Kuwekeza ktk stahiki za watumishi ikiwemo mishahara bora, malipo mengine kama vile Masaa ya ziada, matibabu,kiinua mgongo n.k (d) Kuwekeza ktk teknoljia za kufuatilia Na kudhibiti mienendo ya watumishi kama vile Tachometer, Tachograph katika Magari yao n.k. Na hivyo kupunguza ajali za mabasi kama sio kuzimaliza kabisa Na vile vile serikali kupunguxiwa mzigo mkubwa was kuwa idadi kubwa ya askari bsrabarani kudhibiti madeteva hawa toka utitiiri wa kamouni za mabasi kutokana uwepo was kamouni za mabasi zenye mifumo ya ndani (inernal mechanisms) ya kudhibiti madereva wake Na kuwaondoa wale wasiofaa kabla yavkusababisha ajali

"Samurai, post: 28308232, member: 28531"]Tumekua na ajali za mara kwa mara ambazo haziishi lakini sidhani kama mpaka sasa vyanzo hivi muhimu vya ajali vinazungumziwa zaidi ya kuambiwa tatizo ni mwendo kasi, na Uzembe wa dereva.

Fatigue, Umasikini, Ubovu wa barabara, Elimu ndogo ya vyombo vya moto, Elimu ya msingi (std 1 to std 7), pia ni vyanzo vikubwa sana vya ajali hapa Tanzania.
Nitaelezea kwa uchache na wengine wataweka nyama.

FATIGUE (UCHOVU):
Madereva wengi wa malori, mabasi na hata gari ndogo huwa hawapumziki vya kutosha kiasi cha kufanya safari ndefu, Madereva wa mabasi na malori husafiri mamia ya km lakini huwa hawalali vya kutosha kiasi cha kuwa na nguvu ya kuanza safari siku inayofuata. Wengi wa madereva hawa wakifika kwenye vituo vyao vya kupumzika huanza kufanya starehe kwa maana ya pombe na umalaya na matokeo yake asubuhi huamka na hangover ya K**MA na POMBE, hangover ya hivi vitu viwili ni usingizi na uchovu kupitiliza siku ya pili yake. Elimu ya kujitambua na kuirasimisha hiyo ajili ndio muarobaini pekee kwenye hili, vijana wanahitaji elimu ya kutosha ya kujitambua na Serikali iifanye hiyo kama ajira rasmi kwa maana ya watu walipwe mishahara, night allowance's na wawe na mikataba inayotambulika kisheria wakatwe PAYE NA HIFADHI YA JAMII.

UMASIKINI:

Jamii nyingi sana za kitanzania ziko kwenye umasikini mkubwa na huu umasikini ni chanzo cha matatizo mengi sana Tanzania.
Jamii nyingi za kimasikini ndio zimetoa hawa madereva wengi wanaoendesha roho za watu huko barabarani, na jamii hizi za kimasikini zimekuwa tegemezi sana kwa hawa ndugu zao ambao ni madereva wetu, Shida/Umasikini huleta stress na mwisho wa siku hupunguza umakini barabarani. Dereva huyu anapenda kuwapa wanae elimu bora kama wengine maana anaona mateso anayoyapata yeye barabarani, Dereva huyu anahitaji kusomesha ndugu zake wapate elimu bora, Dereva huyu anahitaji kuwa na nyumba bora ya kuishi, Dereva huyu anahitaji kuwapa matibabu ndugu na wanae, Dereva huyu anahitaji kuwa lishe bora watoto wake, Dereva huyu anahitaji kulea wazee wake choka mbaya wanaishi kijijini huko, HAYO YOOTE MWISHO WA SIKU HULETA STRESS KWA HUYU DEREVA NA MATOKEO YAKE NI KUPUNGUZA UMAKINI AU KUTOKUWA MAKINI KABISA.

Serikali au wenye mamlaka lazima watambue umasikini ni tatizo kubwa Tanzania na tukiwatoa watanzania kwenye umasikini tutakuwa tumetatua mengi, Dereva na ndugu zake wakiwa na kipato kizuri ataishi maisha ya furaha na kazi yake ataifanya vizuri na kwa umakini maana ndio inamuweka mjini ( mfano Madereva South Africa, Botswana, Namibia,Zambia pale London, USA nk).

UBOVU WA BARABARA:

Tanroad jaribuni kuwa na road patrol za mara kwa mara kila mkoa, kila wilaya ili mjue matatizo yaliyopo kwenye barabara zebu na muamue haraka, uzibaji wenu wa viraka bado ni wakizamani na huchukua muda mrefu, barabara zinakaa na mashimo na mibonyeo kwa muda mrefu sana (hapa ni vyema kila Tanroad mkoa ikawa na fungu la emergency){naikumbuka ajali ya basi la MAJINJA PALE KATI YA IRINGA NA MBEYA NA LILE KONTENA CHANZO NI LILE SHIMO PALE).

Tanroad ni vyema mpeleke watu wenu nje wajifunze namna bora ya usimamizi na ujenzi wa barabara ili mwisho wa siku tuwe na Standard yetu ya ubora wa barabara zetu ili kila mjenzi akija tunampa specifications zetu, Kona zisizo na msingi ni nyingi kwenye barabara zetu kiasi cha kutengeneza hatari zisizotakiwa, Maeneo korofi yote yakijengwa mjaribu kuyafanya yawe mapana na ikiwezekana muweke TAA eneo husika ili usiku iwe rahisi. TANROAD NA SERIKALI acheni siasa kaeni chini mchunguze kwa wenzetu ili tupata standard yetu ya ubora wa barabara zetu na tuachane na hizi barabara zinazobonyea na kuchimbika kila siku, kona sehemu zisizohitajika (kifupi makona sio muhimu mbona Kenya hapo wanatushinda hawana kona zisizoeleweka, kule Zambia pia mbona hakuna makona kona kila mahali)

ELIMU NDOGO YA VYOMBO VYA MOTO.

Watanzania wengi wanamiliki na kuendesha vyombo vya moto lakini hawajui matumizi sahihi ya vyombo hivi kifupi wengi hawavijui hivi vyombo sio lazima uwe fundi au proffesional driver hapana hapa tunaongelea General knowledge ya kujua magari na tabia zake mfano huwezi ukawa na IST unataka kuovertake FORTUNER na mbele yako linakuja LANDCRUISER V8 na bado unajiamini utaliwahi, huwezi ukawa na gari yako inachelewa kubadili Gia na wewe huna habari, Ufanyaji wa service kwa wakati na kujua wakati sahihi hii sio kazi ya Fundi, Oil sahihi kwa matumizi ya Gari, Upepo sahihi kwa matumizi ya Gari lako, kwa wale wanaondesha manual kujua wakati gani utumie gia gani, Waendeshaji wa Magari sio lazima uwe umeajiriwa kuna umuhimu wa kulijua gari zako hata kwa kusoma broachure mbali mbali za magari, kuangalia vipindi mbalimbali vya magari, kuzungumza na wataalamu wa magari upate abcd za magari ili ubongo ujue matumizi sahihi ya magari na barabara.

ELIMU YA MSINGI (STD 1- STD 7).
Hii elimu ni nzuri na muhimu sana kwa watu kuwa na uelewa na kujitambua, Elimu ya msingi humsaidia mtu kujijua yeye ni nani na anatakiwa afanye nini, Elimu ya msini humsaidia mtu kujua kusoma na kuandika na hili litamsaidia mtu kujua na kuelewa alama mbalimbali za barabarani, Elimu ya msingi itamfanya mtu kuwa muelewa hata pale anapokosea na kuruhusu kueleweshwa na sio kuwa mbishi, Elimu hii humfanya mtu ajielewe na kuwa na utu barabarani kiasi cha kureport jambo lolote baya alionalo barabarani, Elimu hii humsaidia mtu kuwa na ubongo active kiasi cha kuwa na maamuzi sahihi barabarani.

Watanzania tuitilie mkazo sana elimu ya Tanzania ili watu wengi waweze kuipata, Serikali ni vyema ikahakikisha elimu ya msingi inakuwa bora ili watu wamalizapo shule ya msingi wawe na content sahihi kichwani itakayowawezesha kweli kupambana na mazingira yao, Elimu bora ya msingi ijikite zaidi kwa watu kupata uelewa na kujitambua na kuwafundisha watu mambo yasiyo na msingi, vitu kama alama za barabara,namna bora ya matumizi ya barabara inaweza kuwa kipindi maalumu kwa wanafunzi wa darasa la sita, tusifikirie sana watu kufanya mtihani au mitihani migumu katika level hii hapana ziwepo tu test za kupima uelewa na continuous assessment , Elimu bora ya msingi itajenga watu bora wenye msingi imara ambao mwisho wa siku watatupunguzia matatizo mengi..[/QUOTE]
 
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2014
Messages
35,438
Points
2,000
hearly

hearly

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2014
35,438 2,000
Kuwa makini, mwendokasi ni sehemu ndogo sana ya kusababisha ajali, inaonekana wenye magari wanakukera sana. Ajali nyingi za sasa ni sababu ya miundombinu mibovu (barabara) ila kwa kuwa serikali inahusika hawataki kuliona hili. Sababu nyingine ni ubovu wa magari...hapa ndio kuna rushwa ya ukaguzi. Na sababu ya tatu ni rushwa katika upatikanaji wa leseni hapa pia Polisi na TRA wanahusika
Shikamoo" hapo kwenye miundo mbinu "" (kongole mkuu)...kama hiki kipnde cha morogoro road kuanzia chalinze kwenda dar "" ni hatari ..bara bara ina mawimbi mawimbi "" kama kimbunga cha tsunami
 
B

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Messages
1,541
Points
2,000
B

brazaj

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2016
1,541 2,000
Sheria za nchi yetu zipo vizuri tu na zimeelekeza kila kitu na hata kanuni za udereva wa kujihami zipo na vitabu vipo.
Vyuo vipo watu hawataki kwenda kusomea udereva wanabaki na lawama kwa jeshi la polisi.
Mtu umepata leseni kulingana na uwezo wako wa kuendesha lakini unataka ujionyeshe barabarani kuwa unaweza kuendesha kwa mbwembwe nyingi na speed kubwa kwa kujidanganya kuwa huna Limit ya speed.
Limit ipo kwenye kwenye alama za barabara.
Ukiona kibao cha speed 100 huruhusiwi kuendesha zaidi ya kiwango hicho. Na kama haujui ni wajibu wako kutafuta elimu Darasani au kuwatafuta Wataalam wa mambo ya uchukuzi au wakaguzi wa magari uwaulize.

Tatizo Watanzania wengi wanadharau mambo mengi na kujifanya kuwa wanajua.
Profesa anajiona yeye hawezi kukaa darasani na kujifunza udereva wa kujihami anaona ni elimu ndogo sana.

Matokeo yake bosi yupo kwenye gari na ana leseni na hua anaendesha gari ya nyumbani lakini anaendeshwa na dereva hovyo barabarani bila kumkemea kuwa anakiuka kanuni za bora za udereva na maadili take.

Wasimamizi wa sheria tutawalaumu bure mana wao wanajutahidi kuadhibu kama kanuni na sheria zinavyowaelekeza.
Elimu inatolewa kabla ya kosa kutendeka lakini ukisha vunja sheria jukumu la wasimamizi wa sheria ni kukuadhibu kwa mujibu wa sheria inayohusika.

Ingekua ni masuala ya kutoa elimu basi watu wangeomba wapekekwe mahakamani ili wakapewe elimu na hakimu.
Watu wanashindwa kutofanutisha kuonya na kutoa elimu.

Elimu inatolewa kwa wajinga na wale wanaotaka kujiendeleza ambao wao wanaelimu Ila wanaamua kusoma zaidi.
Sasa sio kazi ya Askari barabarani kumfundisha dereva alama za barabarani wakati yuko ndani ya gari anaendesha .

Lakini ni jukumu la wasimamizi hao wa sheria kutoa elimu mashuleni na kwa watembea kwa miguu wasiojua sheria na kanuni za usalama barabarani.
Ndio maana Mara nyingi wanafanya hivyo kwa abiria lakini sio kwa madereva.

Ni vizuri madereva hasa wa magari binafsi wakatafuta vitabu vya kanuni za udereva wa kujihami kwa Walimu wa NIT au Veta.
Ni kwa faida ya Taifa na wao wenyewe.
Sioni sababu ya kutegemea huruma ya Askari wakati mtu amevunja sheria kwa makusudi.

Askari tuwalaumu kwa kubambikiza makosa yasiyopo kama vile kumwandikia mtu faini kwa sababu gari INA vumbi. Hapo kama atafanya hivyo basis tumlaumu lakini kwa mwendo kasi kwa kuvuka Taa nyekundu,kutofuata alama za kukataza kupita gari jingine.
Kutozingatia speed ya wastani kwenye makazi ya watu ambayo sheria iko wazi kuwa isizidi 50km/hr. Hapa kwa kweli tusiwalaumu wasimamizi wa sheria.

Mara nyingi madereva wanawashawishi askari kwa kutoa rushwa baada ya kufanya kosa.
Kama huna kosa huwezi kutoa Rushwa kamwe utakua ni ujinga wa kupitiliza.
Kama sina kosa mtu akiniandikia nitakwena mpaka kwa Rais kama IGP hatanisikiliza.

Yani gari yangu taa zinawaka halafu uniandikie faini kuwa haziwaki. Itakua ni balaa la hatari.
Kwenye speed 50 ukitembea 48 nani atakuandikia?

Tukitimiza wajibu wetu kama madereva nadhani tutabaki kwenye suala la miundo mbinu na Ubovu wa gari lakini kwa dereva aliyesoma udereva hawezi kuendesha gari bovu.
Kitu cha kwanza kabisa kufundishwa kwenye udereva ni namna ya dereva kukafua mifumo muhimu ya gari.
Mkuu ni ajabu na kweli kwa Sheria za sasa hivi zenye uvundo wa RUSHWA private vehicle Haina speed limit. Tuyapige Vita haya wanaoyaleta hawana nia njema na sisi.

Wanao yaleta haya wamejificha nyuma ya pazia wanajua RUSHWA sana katika hili. Wanapaswa kujua sasa tumechoka. Hatutaki kufa kwa ajali tunataka kuishi.

Polisi mnatusaliti sana katika hili. Hatudanganyiki tena na malengo yenu tumeyajua.

Hivi Sheria za kibaguzi barabarani mlizitoa wapi?

Mnasoma wapi private vehicle hata 500km/h ni sawa na kuwa nyie na wenzenu wenye bendera hata 50km/h haziwahusu?

Loo! Mnaishngaza Dunia.
 
neo1

neo1

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2013
Messages
571
Points
1,000
neo1

neo1

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2013
571 1,000
Sababu kubwa kabisa ya ajari ni barabara!!,
Yaan watanue na kuwa na high way.. Basi Hapo tutapishana na ajari... Na xikiwepo hazitakuwa kwa wingi.
 
G

gunz

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2018
Messages
269
Points
500
G

gunz

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2018
269 500
Miundombinu ni chanzo kikubwa. Mengine yanafuata.
=Nchi yoyote iliyoendelea wanatumia metro train,underground train,train za umeme safari za mbali.
=nchi zilizoendelea Barabara unakuta 4 kwenda 4 kurudi. Tz mtu akiovertake na kuja upande wako inabidi uingie porini. Tairi ikipasuka huna jinsi utaingia porini.
=barabara mashimo kibao. Ukipishana na magari makubwa inabidi ubane sana pembeni ufinyu wa barabara.
=teknolijia bado. Tz watu wanasafiri usiku kukwepa trafiki. Wenzetu barabara zinaangaliwa na camera. Huwezi kudanganya. Hivyo dereva anakua makini muda wote. Usiku na mchana. Ukivunja sheria unakuta fine nyumbani kwako.
 
=nchi za wenzetu wapo makini kusimamia sheria. Rushwa ipo kidogo sana.dereva anaweza kunyang'anya leseni asiendeshe kabis a kama makosa yanajirudia.
 
G

gunz

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2018
Messages
269
Points
500
G

gunz

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2018
269 500
Maelezo yako yana akisi kwa nini pasipo kuwepo limit zilizo wazi tunatembea barabarani kwa kudra tu na tuendelee kusubiria rambirambi.

Haipo barabara au kipande chochote cha barabara popote hapa nchini chanye kupitisha gari yoyote katika mwendo wa kufika 180km/h kama ilivyokuwa hapo kwenye maelezo yako.

Pathetic!
Kwa africa barabara zetu hazikidhi kwenda speed za mwisho. Maz speed za magari. Mfano bmw min van ndogo kama vitz ina max speed 220 hadi 240 km/h. Nilijaribu kuuluza kigari kama hiki unaweza kutembea hiyo sppeed? La kwa bongo barabara hairuhusu ila kwa nchi zilizoendelea unaweza kwenda hiyo speed. Sometimes ni kutumia akili na reasoning. Zipo bmw speed 330 km/hr kwa tz hakuna barabara ya kwenda hiyo speed.
 
1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2012
Messages
4,455
Points
2,000
1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2012
4,455 2,000
Mkuu ni ajabu na kweli kwa Sheria za sasa hivi zenye uvundo wa RUSHWA private vehicle Haina speed limit. Tuyapige Vita haya wanaoyaleta hawana nia njema na sisi.

Wanao yaleta haya wamejificha nyuma ya pazia wanajua RUSHWA sana katika hili. Wanapaswa kujua sasa tumechoka. Hatutaki kufa kwa ajali tunataka kuishi.

Polisi mnatusaliti sana katika hili. Hatudanganyiki tena na malengo yenu tumeyajua.

Hivi Sheria za kibaguzi barabarani mlizitoa wapi?

Mnasoma wapi private vehicle hata 500km/h ni sawa na kuwa nyie na wenzenu wenye bendera hata 50km/h haziwahusu?

Loo! Mnaishngaza Dunia.
Kwanza sijakuelewa unapohusisha rushwa na sheria ya speed limit na ubaguzi wa sheria.
Nimesema tutawalaumu Trafiki bure wakati kazi yao ni kusimamia sheria zilizopo na sio kutunga sheria.

Gari za abiria na gari za mizigo na gari zote zenye uzito wa zaidi ya Tani 3 na nusu ziwe ama za mizigo ,abiria au la zimeelekezwa na sheria kuwa zisizidi 80KM /HR.
Hii ni sheria iliyowekwa na Bunge ambalo lina watu wenye busara ya kitosha na waliozingatia tafiti mbalimbali na mazingira ya barabara zetu.

Wewe kama umewahi kendesha TANKER au Semi Trailer ungejua ni kwa nini hayo magari makubwa yamewekewa speed limit hasa ikitokea jambo la ghafla na dereva akafunga brake.
Magari madogo kama Land Cruiser na Benzi hata kama lipo speed 180 likikutana na jambo la dharura kama dereva analazimika kufunga brake madhara yake sio kama gari kubwa kama basis au Lori.

Hata hivyo magari yote barabarani na madereva wote wanatakiwa kufuata speed signs za barabarani muda wote isipokuwa magari ya viongozi wakati yakiwa yanasindikizwa na king'ora cha polisi kwa ajili ya kutoa tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara.
Kwa hiyo kama kuna alama ya speed 30 km/hr. Hapo hakuna cha basi wala cha private car. Dereva unatakiwa uongee na alama tu.

Kama kuna kibao cha 60km /hr kwenye mteremko au kona hakuna mjadala madereva wote wanapaswa kufuata.
Sasa huo ubaguzi uko wapi?

Speed limit imewekwa kuzingatia utaalam na tafiti zilizofanywa kwa kuangalia uwezekano wa kulimudu gari kubwa au dogo wakati wa dharura. Sio suala la rushwa.
Hata kupata Leseni ya Urubani wa kuendesha ndege za abiria kuna masharti magumu zaidi ya ndege za abiria na hata usimamizi wake ni tofauti lengo hasa ni kulinda abiria wenye lengo la kufika salama. Sio suala la rushwa.

Serikali iko makini haiwezi kutunga sheria za kuhamasisha utoaji wa rushwa.
Ndio maana kuna shule za udereva ili kila dereva asome na kujua kanuni na maadili ya udereva kabla ya kuingia barabarani. Na ajue kuwa anaendesha gari la aina gani na afuate kanuni ili asiangukie kwenye mikono ya sheria.
 
kayaman

kayaman

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2013
Messages
3,953
Points
2,000
kayaman

kayaman

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2013
3,953 2,000
Mwaka jana mwezi wa nane nikiwa njiani kutoka mwz kuja dar nimefika maeneo ya singida nilipitwa na v8 ya polisi kwa mwendo wa risasi kufika mbele nikakuta imepata ajari na ndani yake alikuwemo rto wa pwani, sikushangaa sana nilijua kwa mwendo ule na njia za bongo lazima angebutuka tu!
 
Trimmer

Trimmer

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2014
Messages
1,326
Points
2,000
Trimmer

Trimmer

JF-Expert Member
Joined Apr 25, 2014
1,326 2,000
Kwanza sijakuelewa unapohusisha rushwa na sheria ya speed limit na ubaguzi wa sheria.
Nimesema tutawalaumu Trafiki bure wakati kazi yao ni kusimamia sheria zilizopo na sio kutunga sheria.

Gari za abiria na gari za mizigo na gari zote zenye uzito wa zaidi ya Tani 3 na nusu ziwe ama za mizigo ,abiria au la zimeelekezwa na sheria kuwa zisizidi 80KM /HR.
Hii ni sheria iliyowekwa na Bunge ambalo lina watu wenye busara ya kitosha na waliozingatia tafiti mbalimbali na mazingira ya barabara zetu.

Wewe kama umewahi kendesha TANKER au Semi Trailer ungejua ni kwa nini hayo magari makubwa yamewekewa speed limit hasa ikitokea jambo la ghafla na dereva akafunga brake.
Magari madogo kama Land Cruiser na Benzi hata kama lipo speed 180 likikutana na jambo la dharura kama dereva analazimika kufunga brake madhara yake sio kama gari kubwa kama basis au Lori.

Hata hivyo magari yote barabarani na madereva wote wanatakiwa kufuata speed signs za barabarani muda wote isipokuwa magari ya viongozi wakati yakiwa yanasindikizwa na king'ora cha polisi kwa ajili ya kutoa tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara.
Kwa hiyo kama kuna alama ya speed 30 km/hr. Hapo hakuna cha basi wala cha private car. Dereva unatakiwa uongee na alama tu.

Kama kuna kibao cha 60km /hr kwenye mteremko au kona hakuna mjadala madereva wote wanapaswa kufuata.
Sasa huo ubaguzi uko wapi?

Speed limit imewekwa kuzingatia utaalam na tafiti zilizofanywa kwa kuangalia uwezekano wa kulimudu gari kubwa au dogo wakati wa dharura. Sio suala la rushwa.
Hata kupata Leseni ya Urubani wa kuendesha ndege za abiria kuna masharti magumu zaidi ya ndege za abiria na hata usimamizi wake ni tofauti lengo hasa ni kulinda abiria wenye lengo la kufika salama. Sio suala la rushwa.

Serikali iko makini haiwezi kutunga sheria za kuhamasisha utoaji wa rushwa.
Ndio maana kuna shule za udereva ili kila dereva asome na kujua kanuni na maadili ya udereva kabla ya kuingia barabarani. Na ajue kuwa anaendesha gari la aina gani na afuate kanuni ili asiangukie kwenye mikono ya sheria.
 
S

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Messages
8,517
Points
2,000
S

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2017
8,517 2,000
Mkuu wenye magari hawanikeri. Tafadhari nisome kwa makini. Nina tatizo na RUSHWA. Pana RUSHWA sana penye mwendo kasi na pia zaidi ya 80 per cent ajali kwa takwimu zao polisi sababu za ajali ni mwendokasi.

Sioni ni sahihi kuwepo barabarani magari yasiyokuwa na restriction katika speed. Kwa nini mabasi yawe limited speed lakini si mengine?

Ajali zitaendelea kuwepo kwa sababu kwa human nature restriction kwako ni sawa lakini si kwangu. Ndiyo maana wale wasimamia Sheria hata 50km/h haziwahusu.

Siku sote tukiwa sawa mbele ya Sheria hizi tutakuwa na Sheria muafaka kwa ajili yetu sote na si kwa kundi fulani tu na hapo ndipo utii bila shuruti utawezekana.
Ni siri iliyowazi kua kuna rushwa tena ya wazi wazi inayohusisha madereva na askari wa usalama barabarani, hili jambo hata mtoto mdogo anajua. Angalia wanavyofanyakazi Dar Es Saaam, utashangaa kama taifa tunaelekea wapi. Jinsi wanavyo jipanga, makosa wanayowakamatia watu,, kona wanazokaa na menginge ni mkakati wa wazi kabisa wa kupiga hela na sio kuhakikisha wanasimamia kudhibiti ajali za barabarani, na suala hili hata mamlaka rasmi za kupambana na rushwa zingeenda extra mile kidogo zingegundua hilo kama kweli mamlaka hizo hazilijui!

Dsm kwa logistics zake sio zone ya ajali mbaya na zahatari kutokea kama maeneo mengine ya nchi, lakini ndio kuna makundi makubwa ya askari wa trafiki wakifanya kazi ya kupiga faini au kuchukua hela kwa mtu aliyeendesha kwa speed ya 52kph au aliyewakiwa na taa ya manjano katikati ya junction, maana ukisimama hapo ni kosa, ukienda mbele ni kosa na ukirudi nyuma pia ni kosa na utalazimika kuingia mfukoni kumalizana nao

Ni rai yangu askari wengi zaidi wa usalama barabarani wapelekwe kwenye high ways na maeneo mengine hatarishi na Dsm wabaki wachache wa kuongoza magari hasa nyakati za kwenda na kutoka makazini kwani watatosha kabisa. Wingi wa trafik polisi kwa jiji la Dar haujasidia kuondoa magari mabovu na kinyume chake ndio yanaongezeka sababu wahusika wanafanya kitu kingine kilicho tofauti na maadili yao ya kazi japo ukiuliza utaambiawa ufate sheria maana wao wanatekeleza wajibu wao na wewe usiendeshe gari kwa speed ya 51kph laa sivyo tunakuandikia tu! Ni Dar pekee unawza endesha gari mwaka mzima bila leseni na isiwe kitu
 
Kididimo

Kididimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Messages
2,929
Points
2,000
Kididimo

Kididimo

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2016
2,929 2,000
Kuwa makini, mwendokasi ni sehemu ndogo sana ya kusababisha ajali, inaonekana wenye magari wanakukera sana. Ajali nyingi za sasa ni sababu ya miundombinu mibovu (barabara) ila kwa kuwa serikali inahusika hawataki kuliona hili. Sababu nyingine ni ubovu wa magari...hapa ndio kuna rushwa ya ukaguzi. Na sababu ya tatu ni rushwa katika upatikanaji wa leseni hapa pia Polisi na TRA wanahusika
100% true.
 
1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2012
Messages
4,455
Points
2,000
1000 digits

1000 digits

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2012
4,455 2,000
Ni siri iliyowazi kua kuna rushwa tena ya wazi wazi inayohusisha madereva na askari wa usalama barabarani, hili jambo hata mtoto mdogo anajua. Angalia wanavyofanyakazi Dar Es Saaam, utashangaa kama taifa tunaelekea wapi. Jinsi wanavyo jipanga, makosa wanayowakamatia watu,, kona wanazokaa na menginge ni mkakati wa wazi kabisa wa kupiga hela na sio kuhakikisha wanasimamia kudhibiti ajali za barabarani, na suala hili hata mamlaka rasmi za kupambana na rushwa zingeenda extra mile kidogo zingegundua hilo kama kweli mamlaka hizo hazilijui!

Dsm kwa logistics zake sio zone ya ajali mbaya na zahatari kutokea kama maeneo mengine ya nchi, lakini ndio kuna makundi makubwa ya askari wa trafiki wakifanya kazi ya kupiga faini au kuchukua hela kwa mtu aliyeendesha kwa speed ya 52kph au aliyewakiwa na taa ya manjano katikati ya junction, maana ukisimama hapo ni kosa, ukienda mbele ni kosa na ukirudi nyuma pia ni kosa na utalazimika kuingia mfukoni kumalizana nao

Ni rai yangu askari wengi zaidi wa usalama barabarani wapelekwe kwenye high ways na maeneo mengine hatarishi na Dsm wabaki wachache wa kuongoza magari hasa nyakati za kwenda na kutoka makazini kwani watatosha kabisa. Wingi wa trafik polisi kwa jiji la Dar haujasidia kuondoa magari mabovu na kinyume chake ndio yanaongezeka sababu wahusika wanafanya kitu kingine kilicho tofauti na maadili yao ya kazi japo ukiuliza utaambiawa ufate sheria maana wao wanatekeleza wajibu wao na wewe usiendeshe gari kwa speed ya 51kph laa sivyo tunakuandikia tu! Ni Dar pekee unawza endesha gari mwaka mzima bila leseni na isiwe kitu
Umewaza sawasawa lakini kwa kuangalia kuwa Dar es salaam ndio sehemu yenye watumiaji wengi wa Barabara kuliko maeneo mengine yote!!

Dar es salaam kuna misafara mingi ya viongozi wa ndani na nje ya nchi sasa kusema kuwa pawe na askari wachache wa usalama barabarani ni jambo la kutia mashaka tafakuri ya mtu mwenye wazo kama hilo. Dar es salaam kuna traffic light nyingi kuliko maeneo yote ya nchi kwa hiyo ni lazima maeneo kama hayo yawe na askari wengi.

Wingi wa faini zinazoandikwa Dar es salaam zinaonyesha wazi kuwa kuna madereva wengi wazembe , wasiojali na wanaovunja sheria.

Sijaelewa kuwa kama kwa sasa watu wanakamatwa kwa wingi kwa uvunjaji wa sheria jijini Dar es salaam makosa na uvunjaji huo utapungua vipi kwa kupunguza Traffic ambao hata hivyo uwiano wao ni mdogo ukilinganisha na wingi wa magari.
 
Kididimo

Kididimo

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2016
Messages
2,929
Points
2,000
Kididimo

Kididimo

JF-Expert Member
Joined Sep 20, 2016
2,929 2,000
Miundombinu itizamwe. Mfano ukitoka Tunduma hadi Mbeya,maeneo ya Mbozi kuna sehemu lami imetengeneza matuta na mifereji. Gari ndogo zinasumbuka sana,pia semis , zinaonekana kuyumba sana pindi inapotokea kuhama upande mmoja kwenda mwingine. Pia barabara ni nyembamba sana.
Hali kadhalika maeneo ya Chalinze, Ruvu nililiona hilo, sina uhakika kama lilirekebishwa. Maeneo mengine utakuta katikati ya Highway kuna punda na mikokoteni.
 
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
35,502
Points
2,000
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
35,502 2,000
Waziri wa Usafirishaji, sijui ujenzi back then ndio alijenga Barabara sub standard. Hili halisemwi
 
S

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Messages
8,517
Points
2,000
S

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2017
8,517 2,000
Umewaza sawasawa lakini kwa kuangalia kuwa Dar es salaam ndio sehemu yenye watumiaji wengi wa Barabara kuliko maeneo mengine yote!!

Dar es salaam kuna misafara mingi ya viongozi wa ndani na nje ya nchi sasa kusema kuwa pawe na askari wachache wa usalama barabarani ni jambo la kutia mashaka tafakuri ya mtu mwenye wazo kama hilo. Dar es salaam kuna traffic light nyingi kuliko maeneo yote ya nchi kwa hiyo ni lazima maeneo kama hayo yawe na askari wengi.

Wingi wa faini zinazoandikwa Dar es salaam zinaonyesha wazi kuwa kuna madereva wengi wazembe , wasiojali na wanaovunja sheria.

Sijaelewa kuwa kama kwa sasa watu wanakamatwa kwa wingi kwa uvunjaji wa sheria jijini Dar es salaam makosa na uvunjaji huo utapungua vipi kwa kupunguza Traffic ambao hata hivyo uwiano wao ni mdogo ukilinganisha na wingi wa magari.
Misafara mingi na inayosababisha foleni kwa Dar ni suala linalohitaji mjadala wa pekeyake mkuu.

Uwiano wa askari na wingi wa magari yaliyopo Dar ni jambo ambalo halijaleta tija ya kutosha kwa sababu ya makosa wanayo angalia na kuyatoza faini mara nyingi hayahusiani na yale yakuhakikisha magri mabovu na hatarishi hayapo barabarani, kwa uchache wao kama unavyosema walipaswa ku deal na vyanzo halisi vya ajali kuliko wanavyofanya kazi kwa kuvizia ili mtu afanye kosa hata la bahati mbaya na lisilo htarishi ili hela ipatikane

Kwa Dar taa zikiweza kutumika vizuri na kwa msaada wa sakari wachache wa usalama barabarani, misafara ikiandaliwa utaratibu mwingine na wenye ufanisi basi nguvu kubwa ingepelekwa mikoani ambapo miaka na miaka zinatokea ajali nyingi, mbaya na zinazopoteza maisha ya watu wengi ukilinganisha na Dar.

Nakupa changamoto moja uifanyie utafiti mkuu. Siku askari wa usalama barabarani wa Dar wakiamua kufanya kazi hasaa ya kuongoza magari siku hiyo kunakua hakuna foleni kabisaaa. Sometimes foleni kubwa husababishwa na hayo majukumu mengi ya ukusanyaji mapato waliyonayo
 
B

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Messages
1,541
Points
2,000
B

brazaj

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2016
1,541 2,000
Kwanza sijakuelewa unapohusisha rushwa na sheria ya speed limit na ubaguzi wa sheria.
Nimesema tutawalaumu Trafiki bure wakati kazi yao ni kusimamia sheria zilizopo na sio kutunga sheria.

Gari za abiria na gari za mizigo na gari zote zenye uzito wa zaidi ya Tani 3 na nusu ziwe ama za mizigo ,abiria au la zimeelekezwa na sheria kuwa zisizidi 80KM /HR.
Hii ni sheria iliyowekwa na Bunge ambalo lina watu wenye busara ya kitosha na waliozingatia tafiti mbalimbali na mazingira ya barabara zetu.

Wewe kama umewahi kendesha TANKER au Semi Trailer ungejua ni kwa nini hayo magari makubwa yamewekewa speed limit hasa ikitokea jambo la ghafla na dereva akafunga brake.
Magari madogo kama Land Cruiser na Benzi hata kama lipo speed 180 likikutana na jambo la dharura kama dereva analazimika kufunga brake madhara yake sio kama gari kubwa kama basis au Lori.

Hata hivyo magari yote barabarani na madereva wote wanatakiwa kufuata speed signs za barabarani muda wote isipokuwa magari ya viongozi wakati yakiwa yanasindikizwa na king'ora cha polisi kwa ajili ya kutoa tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara.
Kwa hiyo kama kuna alama ya speed 30 km/hr. Hapo hakuna cha basi wala cha private car. Dereva unatakiwa uongee na alama tu.

Kama kuna kibao cha 60km /hr kwenye mteremko au kona hakuna mjadala madereva wote wanapaswa kufuata.
Sasa huo ubaguzi uko wapi?

Speed limit imewekwa kuzingatia utaalam na tafiti zilizofanywa kwa kuangalia uwezekano wa kulimudu gari kubwa au dogo wakati wa dharura. Sio suala la rushwa.
Hata kupata Leseni ya Urubani wa kuendesha ndege za abiria kuna masharti magumu zaidi ya ndege za abiria na hata usimamizi wake ni tofauti lengo hasa ni kulinda abiria wenye lengo la kufika salama. Sio suala la rushwa.

Serikali iko makini haiwezi kutunga sheria za kuhamasisha utoaji wa rushwa.
Ndio maana kuna shule za udereva ili kila dereva asome na kujua kanuni na maadili ya udereva kabla ya kuingia barabarani. Na ajue kuwa anaendesha gari la aina gani na afuate kanuni ili asiangukie kwenye mikono ya sheria.
Mkuu haipo sheria iliyotungwa na bunge inayotaka mabasi, malori zaidi ya tani 3 na nusu kama ulivyosema inayo limit speed yake kwenye 80km/h. Vile vile hakuna sheria ya bunge inayo toa fursa kwa magari mengine yoyote yaliyobakia kuwa ati yana ruksa ya sheria ya kutembea vyovyote bila limit.

Kilichotokea hapa ni matamko tu ya polisi ambayo pia ni kinyume na sheria zinazobebwa na alama za barabarani zilizowekwa na makandarasi na pia TANROADs wao wakajiwekea mabasi na malori speed limit iwe 80km/h. Hii ikiwa ni hata kama kuna sehemu alama za barabarani zinaonesha 100km/h. Hapo hapo wakaendelea na matamko yao yenye kuvunja sheria kuwa magari private yanaweza kwenda speed yoyote hata 500km/h kinyume cha alama zote za barabarani ati kuwa hawa waheshimu 50km/h peke yake.

Cha kushangaza ni hivi hawa wasiokuwa limited kwenye speed, wanatuhakikishia vipi sisi watumiaji wengine wa barabara wakiwamo watembea kwa miguu, pikipiki, mifugo nk,na hata wale kina yakhe tulio kwenye mabasi?

Ninaamini kwa maelezo haya ya awali nimejibu hoja yako ya benz na land cruiser na hizo ulizosema brake za ghafla. Babarani kuna watumiaji wengine. How do we coexist kama kuna vichaa na wenda wazimu na magari yao binafsi wanatembea 180km/h humo humo wakibarikiwa na polisi? Si kuweka maisha yetu sisi rehani kwa tamaa zenu?

Utaona hapa sheria za bunge zinatambua vibao vya barabarani kwa kila mtumia barabara -- hazina ubaguzi. Kwamba palipo na kibao cha 80km/h ni kwa magari yote mabasi, malori, pikipiki na hata magari binafsi. Hali kadhalika katika 50km/h na 100km/h. Tofauti na hapo kwa ubaguzi polisi wamekuja na yao ambayo ni kinyume cha sheria na ni ya kibaguzi au wewe huoni hivyo?

Kwa nini pana rushwa inayopaliliwa kwenye ubaguzi huu?

Mabasi na malori rushwa wanazochukua ni kubwa zaidi. Hawa wala rushwa wamejipanga kupiga bingo kwenye mabasi na malori. Basi moja tu wanakula rushwa ya kutosha magari labda kuzidi hata madogo 100. Mabasi na malori yamewekewa sheria za matamko zisizo rafiki kwa makusudi mazima ili kupalilia rushwa huku private wakipewa incentive ya hakuna limit ili wasihoji kwa niaba ya hawa wanaokamuliwa ili ukamuaji uendelee pasipo na wapigaji kelele kama sisi mitandaoni.

Kwa kukuibia ni kuwa pana polisi wengi tu humu jamii forums. Kwa bandiko hili wote wameingia mitini. Rushwa yake ilivyo hapa walidhani hatuna sababu ya kusema kwani tumepewa incentive ya kutokuwapo na limit barabarani. Inatugharimu maisha lazima tuseme!

Wanajua vyema kuwa sote tungekuwa sawa mbele za sheria, sheria mbovu tungezipigia kelele ingekuwa kuwa na lazima ya maboresho au marekebisho. Hapo wana bank kwenye divide and rule. Wataalaamu hawa wa rushwa kwa matamko ya kibaguzi waliyoyafanya ni sheria wametufanya tudhani kuwa kwa ku limit speed 80km/h kwa mabasi na malori wakituacha sisi huru na speed yoyote tungeamini kuwa wamekuja na mwarobaini wa ajali. Kwa mahesabu yao walijua tutakaa kimya waendelee kupiga pesa ndefu.

Hili la limitless speed ni janga kubwa la kitaifa hatupaswi kulikubali hili.

Tunaingia vipi barabarani wakati pana watu wanaendesha hata 180km/h? Huu ni wendawazimu unaopigiwa chapuo na polisi Tanzania peke yake. Hakuna nchi duniani yenye kitu limitless speed.

Huu ndiyo ule ukweli kuhusu ajali ambao hauongelewi.
 
B

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Messages
1,541
Points
2,000
B

brazaj

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2016
1,541 2,000
1. Limitless max speed kwa magari ya binafsi si sheria ya bunge
2. Limited max speed kwa malori na mabasi si sheria ya bunge

Yote mawili hapo juu ni matamko ya polisi waliyoyafanya kuwa sheria.

Kwa kuanzia polisi wazuiwe kuja na matamko na kuyafanya sheria. Wao wasimamie sheria zilizowekwa na Bunge peke yake. Believe me ajali zitapungua mno kwa utaratibu huu. Uzoefu umeonyesha wanapotoa matamko na kuyasimamia wao wenyewe wanakuwa na maslahi yao peke yao. Tumechoka kufa barabarani kwa tamaa zao za pesa.
 
moto2012

moto2012

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2012
Messages
2,262
Points
1,500
moto2012

moto2012

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2012
2,262 1,500
Mkuu haipo sheria iliyotungwa na bunge inayotaka mabasi, malori zaidi ya tani 3 na nusu kama ulivyosema inayo limit speed yake kwenye 80km/h. Vile vile hakuna sheria ya bunge inayo toa fursa kwa magari mengine yoyote yaliyobakia kuwa ati yana ruksa ya sheria ya kutembea vyovyote bila limit.

Kilichotokea hapa ni matamko tu ya polisi ambayo pia ni kinyume na sheria zinazobebwa na alama za barabarani zilizowekwa na makandarasi na pia TANROADs wao wakajiwekea mabasi na malori speed limit iwe 80km/h. Hii ikiwa ni hata kama kuna sehemu alama za barabarani zinaonesha 100km/h. Hapo hapo wakaendelea na matamko yao yenye kuvunja sheria kuwa magari private yanaweza kwenda speed yoyote hata 500km/h kinyume cha alama zote za barabarani ati kuwa hawa waheshimu 50km/h peke yake.

Cha kushangaza ni hivi hawa wasiokuwa limited kwenye speed, wanatuhakikishia vipi sisi watumiaji wengine wa barabara wakiwamo watembea kwa miguu, pikipiki, mifugo nk,na hata wale kina yakhe tulio kwenye mabasi?

Ninaamini kwa maelezo haya ya awali nimejibu hoja yako ya benz na land cruiser na hizo ulizosema brake za ghafla. Babarani kuna watumiaji wengine. How do we coexist kama kuna vichaa na wenda wazimu na magari yao binafsi wanatembea 180km/h humo humo wakibarikiwa na polisi? Si kuweka maisha yetu sisi rehani kwa tamaa zenu?

Utaona hapa sheria za bunge zinatambua vibao vya barabarani kwa kila mtumia barabarani -- hazina ubaguzi. Kwamba palipo na kibao cha 80km/h ni kwa magari yote mabasi, malori, pikipiki na hata magari binafsi. Hali kadhalika katika 50km/h na 100km/h. Tofauti na hapo kwa ubaguzi polisi wamekuja na yao ambayo ni kinyume cha sheria na ni ya kibaguzi au wewe huoni hivyo?

Kwa nini pana rushwa inayopaliliwa kwenye ubaguzi huu?

Mabasi na malori rushwa wanazochukua ni kubwa zaidi. Hawa wala rushwa wamejipanga kupiga bingo kwenye mabasi na malori. Basi moja tu wanakula rushwa ya kutosha magari labda kuzidi hata madogo 100. Mabasi na malori yamewekewa sheria za matamko zisizo rafiki kwa makusudi mazima ili kupalilia rushwa huku private wakipewa incentive ya hakuna limit ili wasihoji kwa niaba ya hawa wanaokamuliwa ili ukamuaji uendelee pasipo na wapigaji kelele kama sisi mitandaoni.

Kwa kukuibia ni kuwa pana polisi wengi tu humu jamii forums. Kwa bandiko hili wote wameingia mitini. Rushwa yake ilivyo hapa walidhani hatuna sababu ya kusema kwani tumepewa incentive ya kutokuwapo na limit barabarani. Inatugharimu maisha lazima tuseme!

Wanajua vyema kuwa sote tungekuwa sawa mbele za sheria, sheria mbovu tungezipigia kelele ingekuwa kuwa na lazima ya maboresho au marekebisho. Hapo wana bank kwenye divide and rule. Wataalaamu hawa wa rushwa kwa matamko ya kibaguzi waliyoyafanya ni sheria wametufanya tudhani kuwa kwa ku limit speed 80km/h kwa mabasi na malori wakituacha sisi huru na speed yoyote tungeamini kuwa wamekuja na mwarobaini wa ajali. Kwa mahesabu yao walijua tutakaa kimya waendelee kupiga pesa ndefu.

Hili la limitless speed ni janga kubwa la kitaifa hatupaswi kulikubali hili.

Tunaingia vipi barabarani wakati pana watu wanaendesha hata 180km/h? Huu ni wendawazimu unaopigiwa chapuo na polisi Tanzania peke yake. Hakuna nchi duniani yenye kitu limitless speed.
Mkuu, umeandika points nzuri sana, una hoja za msingi sana, ila kuna haya
1. Limit less speed sio Tanzania pekee, zipo nchi za SADC, nimekuwa South Africa, Zambia na Uganda, ukiacha maeneo yenye vibao vya speed limit unatembea, kama sipo sahihi naomba niambie kwenye hizo nchi nilizotaja bara bara zao limit ni ipi (na bahati nzuri mtaala wa uderva wa nchi za SADC ni mmoja, unaitwa K50)
2. Ni kweli hilo la speed limit za bara bara zetu inabidi liwepo na ni jukumu la TANROADS/TARURA kuset hizo limit kulingana na viwango vya ubora wa bara bara.

3. Ni kweli Polisi na TANROADS wametengeneza mianya ya Rushwa.
 
Forum statistics

Threads 1,403,290
Members 531,177
Posts 34,419,832
Top