Ajali - simba video bus

Ajali - simba video bus

BUS LA SIMBA VIDEO KUTOKA ARUSHA KWENDA TANGA LIMEPATA AJALI MCHANA HUU HAPA MKUMBARA,LIMEACHA BARABARA NA KUINGIA KICHAKANI/PORINI.
KATI YA ABIRIA WOTE 67 NA DEREVA,WAKIWEMO WAZUNGU WAWILI,HAKUNA ALIYEPATWA NA MAUTI ILA DEREVA NA MAKONDAKTA WAWILI WAMEUMIA VIBAYA BAADA YA KIOO CHA MBELE KUPASULIWA NA MTI NA KUANGUKIA NDANI PALE MBELE WANAPOKAA MAKONDA NA DEREVA.
CHANZO CHA AJALI HII NI KUPASUKA KWA TYRE YA MBELE LAKINI PIA MWENDO KASI MKALI KWANI BUS HILI LILIKUWA LIKIFUKUZANA NA BUS LA MTEI LA KUELEKEA TANGA PIA.
MUNGU MKUBWA/ALLAH AKBAR,ALHAMDULILAH!

source:MIMI MWENYEWE KAMA ABIRIA NILIYEKUWEMO KWENYE AJALI HII

pole sana na Mungu awape nguvu kuendelea na safariLakini sijapenda kauli yako kuwa lilikuwa mwendo kasi,kwanini abiria wanafiki?mlishindwa kumwambia abiria kuwa mchezo huo ni mauti kwenu?Haya mambo unayakuta hata kwenye daladala,limejaza lakini abiria hawasemi kitu wanasubiri lipate ajali waseme lilijaza.Tubadilike jamani.
 
asanteni. Nashukuru sijaumia kabisa (Mungu mkubwa) kwani nilikaa siti ya tatu toka kwa dereva tena dirishani,nimeangukiwa na vipande vya vioo tu na kuramba vumbi,sasa nimeshapanda gari ndogo naendelea na safari kuelekea tanga!!

Mkuu, hapo kwenye rangi! - usiombe! - mimi nakumbuka nilipata ajali sasa balaa lilikuwa kwenye vumbi na michanga iliyoingia mdomoni! - yaani unatema michanga kama nusu saa nzima! - mpaka nkashangaa iliingia saa ngapi?!

Duu! - pole Mkuu ... umenikumbusha mbali ... haya mambo ya ajali usiombe yakukute! - wewe yasikiage kwa mbali!
 
poleni sana, Mungu ashukuriwe mmetoka salama.
 
Pole sana mkuu. Kupasuka tyre kunaweza kusababishwa na mambo mengi lakini mojawapp ni ubora wa matairi. Matairi mengi yanayouzwa mtaani yameexpire. Kumbuka tairi lifespan yake ni miaka minne tu. Hata kama ni jipya. Manufacturing date huwa imeandikwa kweny tyre. Kwa mfano 3208 inamaanisha tairi ilitengenezwa wiki ya 32 ya mwaka wa 2008. Taarifa nyingine kwenye tairi huwa joto la juu, uzito n.k. Kwa mara nyingine tena wadau ukaguzi wa tairi kwenye gari lako au unalopanda ni muhimu. Poleni sana mliopatwa na ajali.

Hazina Yako ilipo ndio na Moyo wako ulipo.
Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Asante kwa darasa na pia concern yako mkuu,stay blessed!!
 
Wadau hebu twende mbali zaidi,wimbo wa ajali tumezoea tujiulize sababu zingine licha ya mwendo kasi,kuna issue ya kuingiza mabasi mtumba,watu wanaunda bodi ambazo quality yake ni poor,mabasi yaliyo mengi body zake zimerust....zinakaguliwa na firm za serikali wanapewa baraka ya kuendelea kubeba roho za wtz,
Lingine ni uhuru wa kuingiza matairi ambayo kiwango chake ni cha chini sana na ya bei poa
KWENYE HILI LA AJALI SERIKALI NDO YA KULAUMIWA SIYO VYOTE VYAKULAUMU MADEREVA,
 
Back
Top Bottom