Ajali - simba video bus

Ajali - simba video bus

Hapo kwenye wazungu wawili ndio umeniacha hoi!!

Aaaaahha Rejao,nimekuacha hoi kwa kipi?? Bahati yako hii si thread ya siasa/dini so nakusamehe maana wewe ndugu yetu bwana!!
 
BUS LA SIMBA VIDEO KUTOKA ARUSHA KWENDA TANGA LIMEPATA AJALI MCHANA HUU HAPA MKUMBARA,LIMEACHA BARABARA NA KUINGIA KICHAKANI/PORINI.
KATI YA ABIRIA WOTE 67 NA DEREVA,WAKIWEMO WAZUNGU WAWILI,HAKUNA ALIYEPATWA NA MAUTI ILA DEREVA NA MAKONDAKTA WAWILI WAMEUMIA VIBAYA BAADA YA KIOO CHA MBELE KUPASULIWA NA MTI NA KUANGUKIA NDANI PALE MBELE WANAPOKAA MAKONDA NA DEREVA.


CHANZO CHA AJALI HII NI KUPASUKA KWA TYRE YA MBELE LAKINI PIA MWENDO KASI MKALI KWANI BUS HILI LILIKUWA LIKIFUKUZANA NA BUS LA MTEI LA KUELEKEA TANGA PIA.
MUNGU MKUBWA/ALLAH AKBAR,ALHAMDULILAH!

source:MIMI MWENYEWE KAMA ABIRIA NILIYEKUWEMO KWENYE AJALI HII


Mkuu mawasiliano yameimarika sana siku huzi, umeturushia news toka Mkumbara! Hongera na asante mkuu
 
Poleni sana nyote. Kwa walio na uzoefu tanga, watu makini huwa hawapandi haya mabasi ni pale mtu unapozidiwa. Yanaua sana, ajali kila wajkati, watu tu hawasikii. Lakini poleni sana, tunawaombea mpone haraka na msipandetena hayo majeneza

Mkuu mara moja moja huwa tunakwenda Tanga na tunapanda haya mabasi.
Umeniogopesha, sasa tupande yapi?
 
duuu hawajachoka tu kunywa damu zetu ....poleni mungu yupo nanyi
 
Ni abiria,nimetaja uasili wao kuonyesha kuwa tulikuwamo wazawa na ndugu zetu wa nje pia!

Poleni sana! Hata hivyo ungefuatilia zaidi maana pengine kulikuwa na wenzetu toka nje kama vile Kenya, Uganda, Burundi...Tofauti ni rangi tu.
 
Poleni sana tunawaombea majeruhi wapone haraka ili waweze kujumuika na familia sao na kuendelea na shughuli zao za kila siku, Amina.
 
Mkuu mara moja moja huwa tunakwenda Tanga na tunapanda haya mabasi.
Umeniogopesha, sasa tupande yapi?

Panda Raha Leo. Uliza popote Dar na Tanga line. Haya yakijaza ndio mabasi haya mengine yanapopata abiria. Raha Leo ni salama zaidi sana. Nimeyasafiria over 20 years. Kizuri hujiuza kibaya hujitembeza-hata ukienda Ubungo bus stand huwezi kukuta wapiga debe wa Raha Leo wanaita abiria maana wanajua kuwa abiria watakuja maana ndio usafiri wa kuaminika.
 
Mabasi ya simba yanatembea barabarani kwa kudra ya wale polisi wenye njaa ni marafiki wa karibu sana, sio magari ya kukaa barabarani, japo kila ajali ina sababu yake. Poleni sana na tushukuru kuwa hakuna baya kubwa lililotokea
 
Haya mabasi ya SIMBA ni ya kufuatilia kwa karibu ,mengine ni mabovu mikanda ndani ipo ushahidi tu imekatikakatika na hata ile mizima sisi abiri tunadharau kufunga mikanda, swala la kufunga mikanda liwe la lazima inasaidia kupunguza ajali, mungu awajalie kupona haraka wale majeruhi!!
 
Aaaaahha Rejao,nimekuacha hoi kwa kipi?? Bahati yako hii si thread ya siasa/dini so nakusamehe maana wewe ndugu yetu bwana!!

kumbe unajua sio thread ya kisiasa sasa kwa nini umeipost kwenye jukwaa la siasa??
 
Hapo kwenye wazungu wawili ndio umeniacha hoi!!
..kumbe na wewe umeistukia hiyo. Uncle wangu mmoja aliwahi kupata ajali maeneo ya singida miaka ya 90 akitusimulia kuwa walikufa abiria wawili na mmasai mmoja. Tulicheka mpaka jamaa akakasirika. Poleni wahanga wote!
 
kumbe unajua sio thread ya kisiasa sasa kwa nini umeipost kwenye jukwaa la siasa??

Mkuu, jamaa yetu msamehe kwani ametoka ajalini na amenusurika kufa ... sasa hata akili bado hazijakamata Network vizuri. Kwanza tumshukuru kwani wakati anawapa taarifa ndugu zake pia wakati huo huo katukumbuka na ndugu zake wa JF.
 
Hapo kwenye wazungu wawili ndio umeniacha hoi!!

Kuna ajali ilitokea jamaa wakaripoti kuwa waliofariki ajalini ni watu sita na Wamasai wawili! - Ilitufanya kujiuliza maswali mengi!
 
Back
Top Bottom