Ajali - simba video bus | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali - simba video bus

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Abdillahjr, Mar 25, 2012.

 1. Abdillahjr

  Abdillahjr JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  BUS LA SIMBA VIDEO KUTOKA ARUSHA KWENDA TANGA LIMEPATA AJALI MCHANA HUU HAPA MKUMBARA,LIMEACHA BARABARA NA KUINGIA KICHAKANI/PORINI.
  KATI YA ABIRIA WOTE 67 NA DEREVA,WAKIWEMO WAZUNGU WAWILI,HAKUNA ALIYEPATWA NA MAUTI ILA DEREVA NA MAKONDAKTA WAWILI WAMEUMIA VIBAYA BAADA YA KIOO CHA MBELE KUPASULIWA NA MTI NA KUANGUKIA NDANI PALE MBELE WANAPOKAA MAKONDA NA DEREVA.

  CHANZO CHA AJALI HII NI KUPASUKA KWA TYRE YA MBELE LAKINI PIA MWENDO KASI MKALI KWANI BUS HILI LILIKUWA LIKIFUKUZANA NA BUS LA MTEI LA KUELEKEA TANGA PIA.
  MUNGU MKUBWA/ALLAH AKBAR,ALHAMDULILAH!

  source:MIMI MWENYEWE KAMA ABIRIA NILIYEKUWEMO KWENYE AJALI HII
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  pole sana mkuu.umeshaenda hospitali kucheki afya,isije ikawa unavuja damu ndani kwa ndani.
   
 3. D

  Dan Geoff P Member

  #3
  Mar 25, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 78
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 25
  poleni sana abiria wote mliokuwemo ndani ya basi, Mungu awape kupona kwa haraka majeruhi wote.
   
 4. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2012
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye wazungu wawili ndio umeniacha hoi!!
   
 5. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  pole ndugu, Pia mshukuru Mungu kwa kuwaokoa wote mkiwa salama.
   
 6. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Poleni kwa yaliyowakuta. Mungu ashukuriwe kwa kuwanusuru.

   
 7. Chali wa Moshi

  Chali wa Moshi JF-Expert Member

  #7
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 258
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  mungu mkubwa.
   
 8. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #8
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwani WAZUNGU SIO ABIRIA? Pole ziwafikie wote! Mungu Mkubwa!
   
 9. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #9
  Mar 25, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  poleni sana wasafiri. Ila kwanini kila mwaka ajali zinakuwa nyingi tunapokaribia kipindi cha sikukuu?
   
 10. Abdillahjr

  Abdillahjr JF-Expert Member

  #10
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  asanteni. Nashukuru sijaumia kabisa (Mungu mkubwa) kwani nilikaa siti ya tatu toka kwa dereva tena dirishani,nimeangukiwa na vipande vya vioo tu na kuramba vumbi,sasa nimeshapanda gari ndogo naendelea na safari kuelekea tanga!!
   
 11. Abdillahjr

  Abdillahjr JF-Expert Member

  #11
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni abiria,nimetaja uasili wao kuonyesha kuwa tulikuwamo wazawa na ndugu zetu wa nje pia!
   
 12. SALOK

  SALOK JF-Expert Member

  #12
  Mar 25, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 2,684
  Likes Received: 880
  Trophy Points: 280
  Pole mkuu, (shafaakumullah) ila hapo kwenye 'mwendo kasi mkali' mie huku hoi!
   
 13. Aggrey86

  Aggrey86 JF-Expert Member

  #13
  Mar 25, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 856
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Dah! Poleni sana wasafiri wote tunamshukuru Mungu kama hakuna aliyepoteza maisha!
   
 14. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #14
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pole sana mdau mungu kawaokoa.
   
 15. Abdillahjr

  Abdillahjr JF-Expert Member

  #15
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni abiria,nimetaja uasili wao kuonyesha kuwa tulikuwamo wazawa na ndugu zetu wa nje pia!
   
 16. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #16
  Mar 25, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Pole ndugu yangu na nashukuru mmetoka salama!
   
 17. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #17
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Pole::::kwani njungu chi ntu?
   
 18. m

  matawi JF-Expert Member

  #18
  Mar 25, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Wape pole abiria wenzako, kwa nini hamkumtia makonzi dereve kama mliona anafukuzana na mtei? Hao wazungu watawaambia wenzao wakija tz wasipande mabasi
   
 19. Abdillahjr

  Abdillahjr JF-Expert Member

  #19
  Mar 25, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante,mkuu na wewe ulikuwemo nini kwenye bus maana nilisikia sauti toka nyuma ya yowe "ooohh nkono yangu"!!!
   
 20. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #20
  Mar 25, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,829
  Trophy Points: 280
  Poleni sana nyote. Kwa walio na uzoefu tanga, watu makini huwa hawapandi haya mabasi ni pale mtu unapozidiwa. Yanaua sana, ajali kila wajkati, watu tu hawasikii. Lakini poleni sana, tunawaombea mpone haraka na msipandetena hayo majeneza
   
Loading...