Ajali mbaya ya Hiace Jimboni kwa Mwigulu Nchemba.

S2dak_Jr

Senior Member
Jul 15, 2012
198
45
Wanajamvi,

Muda si mrefu natokea kwenye tukio la ajali ya Hiace iliyopinduka eneo la barabara ya Misigiri-Kiomboi na kusababisha vifo vya watu watatu.

Baada ya muda wa nusu saa, Mh. Mwigulu alipita eneo la ajali akitokea Kiomboi akiwa na makada wa CCM. Alisimama eneo la tukio huku akirekodi tukio hilo kwa simu yake. Pia alifanya mahojiano na baadhi ya vijana huku akiwarekodi.

Nitawaletea picha za tukio kwani simu ninayotumia haina uwezo wa kufanya uploading.

Source: Nilikuwepo kwenye tukio.


Hiace hiyo hufanya safari kati ya Igunga, Singida na Kiomboi.
 
mheshimiwa ametoa msaada gani kwa wahanga wa tukio hilo!!au kapiga picha na kuondoka!!
 
Sasa hapa kwenye kurekodi ndipo raia watajikita zaidi kujadili....twende kazi
 
teh teh the

Naona ameamua kuishi huko ili alilinde jimbo linaloelekea kutokomea
 
Poleni sana kwa wafiwa na mungu awajaalie majerui wapone haraka. Tunaomba kuuliza Mwigulu alipofika hapo Alihairisha safari na kwenda kwa majerui wa ajali hiyo Hospitali au aliendelea na safari yake baada ya kuchukua picha na kuhoji wananchi?
 
sasa hizo recording anataka akaombe msaada au.anawachora tu? ndio wabunge wetu. hawa
 
mheshimiwa ametoa msaada gani kwa wahanga wa tukio hilo!!au kapiga picha na kuondoka!!



Wakati anafika kulikuwa na mwili mmoja wa marehemu. Alimuita ndugu wa huyo marehemu na kuongea nae. Kisha aliingiza mkono mfukoni na kumpa huyo kijana pesa.
 
Breki za gari lililopata ajali zilikuwa mbovu, ni engine stopper tu ilikuwa inatumika.

Ilishawahi kuua mara mbili.

Dereva wa leo ni mgeni wa barabara na amekimbia.

Gari ilikaguliwa Check Point ya Misigiri.
 
Kina Mama wawili walishuka kutoka kwenye hiyo gari baada ya kugombana na Konda maeneo ya Misigiri.

Baada ya 2km, ajali hiyo ikatokea.
 
Huogopi kupigwa bomu wakati ukipiga picha kama Daud Mwangoka? Wee hujui akina Mwigulu ni haohao?
 
Kina Mama wawili walishuka kutoka kwenye hiyo gari baada ya kugombana na Konda maeneo ya Misigiri.

Baada ya 2km, ajali hiyo ikatokea.

Wewe ni mmoja wa walionusurika? Pole sana kwa kupona katika ajali hiyo mbaya.
 
Back
Top Bottom