Ajali mbaya ya Hiace Jimboni kwa Mwigulu Nchemba.

Wakati anafika kulikuwa na mwili mmoja wa marehemu. Alimuita ndugu wa huyo marehemu na kuongea nae. Kisha aliingiza mkono mfukoni na kumpa huyo kijana pesa.
Weka habari kamili kama Baada ya kupiga picha, kuhoji wananchi, kumuita ndugu wa maiti iliyokuwepo na kumpa pesa je aliondoka? au alisaidiana na ndugu waliokuwepo na kubeba maiti ilyokuwepo na kuipeleka Motuary na kwenda kuangalia majerui wengine? ebu tuambie tunataka kujua hawa viongozi wetu wanathamini watu au wanajithamini wao tu na familia zao. tupe uhondo
 
Marehemu wote ndg zetu walale kwa Amani yake Bwana wetu!

Azilaze roho zao mahala pema peponi!

Na wafiwa wote MUNGU mwenye mamlaka awape nguvu mwenyewe!
 
Pia alikuwa anaficha uso ikiwa ni kama ishara ya kuogopa.

Ndiyo first class wetu wa Uchumi!!! Yaani badala ya kusaidia majeruhi na kutumia simu kutaka msaaada anapiga picha!!! Kweli waliompa kura wana kazi sana!
 
Kina Mama wawili walishuka kutoka kwenye hiyo gari baada ya kugombana na Konda maeneo ya Misigiri.

Baada ya 2km, ajali hiyo ikatokea.

Pamoja na kudra za Mwenyezi Mungu kina mama hao wanastahili pongezi kwa maamuzi yao, watanzania abiria wote tungekuwa na misimamo ya jinsi hiyo hizi ajali zisizokuwa za lazima zingepungua sana, tatizo kubwa ni kuwa wengi wetu hatuna tabia au ujasiri wa kumkanya dereva tunapoona anavuka mipaka, na wengine huwa wana support madereva pale abiria mmoja anapokuja juu huku wakitoa sababu nyingi za kipuuzi tu.

Labda nitoe mfano mmoja wa ujinga wa abiria wa kitanzania, mnaweza kuwa ndani ya daladala, wakati mkikaribia kufika kituo cha mwisho konda; baada ya kuona abiria ni wachache, anawashusha halafu anawatafutia gari nyingine ili mmalizie safari ili wao wageuze, na watanzania watakubali bila matatizo, ni mara chache sana huwa wanapinga.
 
Back
Top Bottom