Ajali Mbaya Iringa 5 wafa papo hapo

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,896
1.JPG
DSCF9378.JPG


Basi la kampuni ya New Force lenye namba za usajili T666 BCR lililokuwa likisafiri kutoka jijini Dar es Salaam Kwenda Mkoani Mbeya limepata ajali na kuua watano papo hapo.

Akizungumza na mtandao huu wa Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima eneo la tukiommoja Kati ya abiria walionusurika katika ajali hiyo John Sanga alisema kuwa dereva wa basi hilo alikuwa akiendesha basi kwa mwendo kasi na uzembe mwingina hata abiria walipojaribu kumkanya alishindwa kusikiliza.

Katika ajali hiyo abiria wengine zaidi ya 16 walijeruhiwa vibaya na kulazwa katika hospital ya wilaya ya Mufindi huku wengine zaidi ya 20 wakipata michubukomidogo midogo na kutibiwa na kuruhusiwa .Mashuhuda wa ajali hiyo walimweleza mwandishi wa habari hizi kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 9 alasiri Leo wakati basi hilo likielekea mkoani Mbeya na kuwa chanzo ni mwendo kasi na uzembe wa dereva.

Alisema eneo hilo ambalo ajali imetokea ni eneo ambalo linamteremko na kuwa mbali ya basi hilo kupinduka pia magari mengine Mawili likiwemo gari la serikali lenye namba za usajili STK 2340 na IT yamegongana na Lori katika eneo hilo. Maiti zilizotolewa katika ajali hiyo hadi saa 2.usiku zilikuwa ni nne na hadi mwandishi wa habari hii anatoka eneo la tukio jitihada za kunyanyua basi hilo ilikutazama maiti nyingine lilikuwa likieendelea chini ya usimamazi wa mkuu wawilaya ya Mufindi Evarista Kalalu na mkuu askari wa Kikosi cha usalama barabarani wakiongozwa na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa Kedmundi Mnubi lilikuwa likiendelea .

Majeruhi wa ajali hiyo ambao wamelazwa katika hospital hiyo ya wilaya ya Mufindi ni pamoja na mtoto wa kiume wa mwaka mmoja ambaye mama yake alikufa katika ajali hiyo , Alen Kilima mkazi wa Kyela , Mwanahabari wa radio Kyela Fm Prakseda Mburu (24) ,Maria Mtawa (46) mkazi wa Tukuyu,Lutusyo Kabenjela (45) mkazi wa Kyela, Elizabeth Andwer(27)Dina Mwasongela (14) mwanafunzi wakidato cha tatu sekondari ya Lutengano Mbeya,Alex Mwaibambe (28) mwanafunziwa mwaka wa pili injinia katika chuo kikuu cha Dar es Salaaam ,Amon Luvanga(30) mkazi wa Mbeya,Yohana Mwasomola(28)

Wengine ni Aggrey Mwangulu (56) mfanyakazi wa TRA Kibaha , Runna Mwampate (36) mkazi wa Kilawani Dar es Salaam , Iman Mwakifwage (32) mkazi wa Mbeya

Mbali ya majeruhi hao kulazwa katika Hospital ya wilaya ya Mufindi baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika Hospital ya wilaya ya Ilembula wilayani Njombe.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Claus Mwasyeba alithibitisha kutokeakwa ajali hiyo na kuwa majeruhi Ramadhan Kipangule (28) mkazi wa TukuyuMbeya amefariki usiku wa leo wakati akipatiwa matibabu katika Hospital ya wilaya ya Mufindi.
Alisema kuwa kati ya abiria waliokufa katika ajali hiyo watatu ni wanawake na abiria wawili ni wanaume na mmoja ametambuliwa kwa jina la ramadhan Kipangule (28) mkazi wa Uyole Mbeya .

Hata hivyo alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea kumsaka dereva wa basi hilo Yahaya Abdalla (35) mkazi wa Dar es Salaam na msaidizi wake Nasib Salum ambao baada ya ajali hiyo walikimbia.Mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista kalalu amewataka wananchi popote pale nchini kujitokeza kutambua miili ya marehemu hao akiwemo mwanamke huyo aliyeacha mtoto wa mwaka mmoja na nusu.

Source: Kwa hisani ya Mzee wa matukio daima
 
Mh hizi ajari mpaka lini jamani. polen watu waliohuska na ajari. Kwa marehemu RIP.
 
Mh hizi ajari mpaka lini jamani. polen watu waliohuska na ajari. Kwa marehemu RIP.

Tumeiweka habari hii hapa na majina ya waathirika tukijua baadhi hapa wanaweza kuwa wanawafahamu na kuwahabarisha ndugu, jamaa na marafiki baada ya kusoma majina ya wahusika.
 
Asante kwa taarifa,ila naomba uweke wazi ni basi la kampuni gani?


Basi la kampuni ya New Force lenye namba za usajili T666 BCR lililokuwa likisafiri kutoka jijini Dar es Salaam Kwenda Mkoani Mbeya limepata ajali na kuua watano papo hapo.
 
Nimegundua watu hawasomi habari wanaangalia picha tu manake maswali yao mhh
 
New Force zinajulikana kwa kutoka bunduki! sasa hivi kuna Mbeya Express nazo zinatisha kwa mafuta
 
Katika picha hizo nimemfahamu mtu mmoja! Nimempigia simu anasema yeye ni kati ya shuhuda wa ajali hiyo na hakuwa abiria katika basi husika. Hata hivyo kakiri na kusema ajali hiyo imesababishwa na uzembe wa dereva wa basi kulazimisha overtaking bila tahadhari yoyote.
 
Kwa hili tuwe wazi, tuanzishe kampeni ya kuorodhesha askari wanaoongoza kupokea kitu kidogo, madereva na magari yaendayo kasi sana. Ajali zinachukua uhai wetu na wengine wanabaki na ulemavu wa kudumu
 
Back
Top Bottom