Ajali mbaya: Basi la Sumry laua 14 huko Singida!

Ajali mbaya: Basi la Sumry laua 14 huko Singida!

Hii kauli siipendi basi tu. Mambo mengine ni ya kibinadamu alaa!!!
"Kazi ya Mungu haina makosa" haina exceptions.

Tusimchagulie mungu vifo ambavyo tunadhani vinakubalika au visivyokubalika.

Mungu kasababisha ajali ya baiskeli akaona haitoshi, akapeleka wengine kushangaa shangaa eneo la ajali, ukaja m-basi mwingine ukawazoa. Busara za kimungu anazielewa yeye mweyewe, tusijaribu kumchunguza. Warumi 11:33
 
Mimi ni shuhuda ambaye nilikuwa ndani ya bus la Al Saedy toka Kigoma kuja Dar na gari letu ndilo lilitumika kuipa escort Sumry ili lifike Police maana taa zake za mbele zilikufa.

Ukweli ni kuwa hao wananchi walitaka kufunga barabara baada ya mwenzao kugongwa na hata Sumry alipowapigia horn waligoma kuondoka na kuendelea na zoezi la kupanga mawe. Dereva wa Sumry alijitahidi kuwakwepa lakini akashindwa kutokana na mwendo kasi na pia kulikuwa na gari jingine mbele yake.

Ubishi wa hawa ndugu zetu ndio umepelekea maafa yote.

Sasa nimeelewa nilijiuliza mara mbili mbili inamaana dereva hakupga honi, je hawakusikia muungurumo wa basi wala kuona mwanga wa bus ulioelekea kwao? All God knows rest in peace marehemu wote!!
 
Police waliofariki ni wanne...tumeaga leo na wameshasafirishwa makwao.
 
kwani askari anapima vipi ajali mnijuze tafashali.

hao watu Mungu kawakusanya wote waliopaswa kumaliza maisha yao duniani ndo wakapitiwa na sumry
 
asante mkuu kwa ufafanuzi mambo mengi hapo kwenye sehemu sikupaona
 
Mwenyenzi Mungu awape pumziko la maisha marehemu wote wapumzike kwa Amani yake Bwana wetu!
 
"Kazi ya Mungu haina makosa" haina exceptions.

Tusimchagulie mungu vifo ambavyo tunadhani vinakubalika au visivyokubalika.

Mungu kasababisha ajali ya baiskeli akaona haitoshi, akapeleka wengine kushangaa shangaa eneo la ajali, ukaja m-basi mwingine ukawazoa. Busara za kimungu anazielewa yeye mweyewe, tusijaribu kumchunguza. Warumi 11:33

Unapotosha. Ni mafundisho ya uongo kama haya ndiyo yanayofanya binadamu wamchukie Mungu.

Mungu hasababishi kamwe uovu amabao unaouona ulimwenguni. (Ayubu 34: 10-12) Ni kweli kwamba anaacha mambo mabaya yatukie. Hata hivyo, kunatofauti kubwa kati ya kuacha jambo litukie na kulisababisha.

Isitoshe, Mungu ni mtakatifu. (Isaya 6:3) Hilo linamaanisha kwamba yeye ni safi wala hana uovu hata kidogo.
 
Ni kweli kwamba anaacha mambo mabaya yatukie.
Sasa Mungu gani huyo "safi na hana uovu" ambae ana uwezo wa kuepusha jambo baya anaacha litokee amekaa tu anatazama kama ngoma? Huyo atakuwa ni Mungu mzembe n​a ajiyejali na hafai kwa sababu hata kiongozi wa kidunia angetuletea uzembe kama huo tungemtoa madarakani.

Mungu ndio anapanga kama kesho utaishi ama huishi, Yakobo 4:15, na siku zako ameshaziandika, Zaburi 139:16.

Lakini hii si kusema alichofanya ni kibaya, ipendeze isipendeze kwetu, kazi ya Mungu haina makosa. Torati 32:4
 
Back
Top Bottom