AJALI: Leina Tours lapata ajali maeneo ya Kimara, Dar

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,660
58,999
Kimara bucha kuna gari linatoka mkoani imetumbukia kwenye mtaro..

Kuna majeruhi na waliopoteza maisha.

Wezi wamejazana wanaiba..

Kama kuna mwenye kuweza kuviambia vyombo vya dola afanye hivyo.

=======================

UPDATE

Basi la LEINA TOURS Lilikuwa likitokea Kahama Shinyanga kuja Dar es salaam ambapo idadi ya waliofariki haijatolewa ila waliojeruhiwa ni zaidi ya 30 na walikimbizwa Mwananyamala Hospitali na Muhimbili.

IMG-20160313-WA0048.jpg


IMG-20160313-WA0049.jpg
 
Ni shida apa daradara zinarudi nyuma cjajua whats happening huko mbele lets seee
 
Kimara bucha kuna gari inatoka mkoani imetumbukia kwenye mtaro.. Kuna majeruhi na waliopoteza maisha.. Wezi wamejazana wanaiba.. Kama kuna mwenye kuweza kuviambia vyombo vya dola afanye hivyo .. Kimara bucha
Ni gari ya abiria au.....????
 
Inasemekana ni basi la abiria kutoka mikoani na kwa mujibu wa Clouds TV breaking news ni kwamba kuna watu wamefariki na wengi kujeruhiwa.Ila hali ya usalama kwa mali za abiria hakuna maana vibaka wamefanya sehemu ya kujineemesha badala ya kuokoa maisha ya majeruhi na mali zao.Hii tabia sio ya kiungwana aisee!
 
leina tours bus la kahama dah siamini juzi nimetoka kule na newforce,nimesikitika zaid baada ya kusikia ni kimara nimejiuliza sana na nimekosa majibu,yanakotoka ni mbali na mwendo kama tunavyojua yaani inafika dar ndio ajali,poleni sana majeruhi na waliopoteza ndugu zao.
 
Nilisha wahi kupost uzi hapa, mabasi ya LEINA pamoja na KISBO, ni shida, serikali yamulikeni mabasi haya.
 
Asante kwa taarifa hebu dodosa tujue hata hali za majeruhi pia weka hata picha habari itakaa vzr zaidi
 
Back
Top Bottom