Pwani: Ajali ya Magari imeua Watu 21 na wengine 15 kujeruhiwa. Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi

kimbendengu

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
6,052
10,303
Kuna tetesi kuwa kuna ajali imetokea huko mkoani Pwani wilaya ya Mkuranga, Gari ya kampuni ya Dangote imegongana uso kwa uso na gari aina ya Costa.

1586934693011.png

Sent from my itel S32 using Tapatalk

=====

Watu 18 wamefariki na wengine 15 kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana katika kijiji cha Kilimahewa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Aprili 15, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema ajali hiyo imehusisha lori na gari la abiria aina ya Toyota Coaster.

“Ni Kweli tuko kwenye eneo la tukio, ajali imetokea na imesababisha vifo vya watu 18 na majeruhi 15,” amesema Lyanga.

Amesema ajali hiyo imetokea leo asubuhi baada ya Coaster hiyo iliyokuwa ikitokea mikoa ya Kusini kwenda Dar es Salaam iligongana na lori hilo lililokuwa likitokea Kimanzichana.

Kamanda Lyanga amesema majeruhi katika ajali hiyo wamepelekwa katika kituo cha afya cha Kilimahewa.

======

UPDATES:

======

VIFO VYAONGEZEKA AJALI YA MKURANGA

Idadi ya watu waliofariki katika ajali iliyotokea wilayani Mkuranga leo asubuhi imeongezeka kutoka 18 na kufikia watu 21, Kamanda wa Mkoa wa kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema.



Rais Magufuli atoa salaam za rambirambi...


Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa ndugu, jamaa na marafiki wa watu takribani 18 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyotokea leo asubuhi Jumatatu Aprili 15, 2020 katika kijiji cha Kilimahewa Kaskazini Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Ajali hiyo imehusisha basi dogo la abiria lililokuwa likitoka kijiji cha Magawa wilayani Mkuranga kwenda jijini Dar es Salaam ambalo limegongana uso kwa uso na lori la mizigo lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya kusini.

Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu imemnukuu Magufuli akimtaka mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo kufikisha salamu zake za pole kwa familia za marehemu na ameeleza kwamba anaungana nao katika kipindi hiki cha majonzi ya kuondokewa na wapendwa wao.

Nawaombea familia za marehemu wote, ndugu, jamaa na marafiki kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, kuwapoteza Watanzania wenzetu kwa idadi kubwa namna hii inaumiza sana, ” amesema Magufuli.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi amevitaka vyombo vya usalama barabarani kuhakikisha vinachukua hatua madhubuti za kuzuia ajali za barabarani na amewataka madereva na wote wanaotumia barabara kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali ambazo zinagharimu maisha ya watu na uharibifu wa mali.


Mkuranga.jpg
 
Back
Top Bottom