Kimara Suka, Dar: Watu wawili wamefariki na nane kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
1643352394685.png

Picha: Sehemu ambayo ajali imetokea

Watu kadhaa wahofiwa kufa na wengine kujeruhiwa kufuatia ajali ya lori lililovamia kituo cha daladala cha Kimara Suca jijini Dar es Salaam leo Januari 28, 2022.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Usalama wa Barabarani Taifa, ACP Abdi Isango ndiye aliyefika eneo la tukio, lakini amesema hawezi kutoa taarifa mpaka atembelee hospitali zote ili ajuwe idadi ya majeruhi na waliopoteza maisha.

Mwandishi wa habari aliyekuwepo katika eneo hilo, ameshuhudia baadhi ya majeruhi na maiti ziliogongwa zikiwa zimetapakaa katika eneo hilo, huku nyingine zikiwa chini ya lory hilo.

Baadhi ya watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema gari hilo lilionekana kupoteza mwelekeo baada ya kukatiba breki.

"Mimi nimesimama pembeni naona gari linanifuata na lilikuwa katika spidi kubwa sana niliruka mtaroni ndicho kilichonisaidia bila hivyo sijui," amesema John Kelvin aliyekuwa amepaki boda boda yake pembeni.

“Rafiki yangu mshtuko alikimbia mbio limemkuta huko huko nikamuona anaingia chini ya lori ndio wamemtoa ameshakufa jamani," amesema.

Mmoja wa ndugu wa majeruhi ambaye hakuta jina lake kuandikwa gazetini amesema amefuatwa nyumbani na boda boda akaambiwa mke wake Aisha amekatika sikio.

"Nilitoka nyumbani haraka sana, nilikuwa mke wangu amewekwa kwenye Kirikuu nikamtoa nimeleta mwenyewe hapa Bochi nikasaidia na wengine wawili.

"Ajali ni mbaya jamani maana imewafuata watu pembeni mimi mke wangu alikuwa anaenda kazini jamani hali yake sio nzuri," amesema.

Taarifa ya kamanda wa Polisi
Kamanda wa Polisi Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amethibitisha watu wawili wamefariki, nane kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mbezi Suka Dar es Salaam, ameeleza waliofariki ni waliokuwa wakivuka kivuko cha watembea kwa miguu.

=====

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI
JESHI LA POLISI TANZANIA

Telegraphic Address “” Ofisi ya:-
E-mail: dsmzhabari@gmail.com
Kamanda wa Polisi,
Telephone No.0222117705
Faksi No: 022-2121524. Kanda maalum ya Polisi,
Facebook: dsmz habari S.L.P.9140,
Twitter; dsmzhabari1 DAR ES SALAAM.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.
Dar-es-salaam 28/01/2022
AJALI YA GARI KUWAGONGA WATEMBEA KWA MIGUU
NA KUPELEKEA VIFO VYA WATU WAWILI NA MAJERUHI
KUMI

Watu wawili wamefariki Dunia na wengine kumi kujeruhiwa katika ajali ya Gari iliyotokea tarehe 28/01/2022 majira ya saa kumi na mbili na robo asubuhi eneo la Kimara Suka, ikihusisha Gari lenye namba za usajili T. 814 DGA aina ya scania Lori ikiwa na Trailer lenye namba T.605 CHR likiendeshwa na dereva aitwaye Paul Peter Muhagama, miaka 37, mngoni likitokea mbezi kwenda kimara aliyagonga kwa ubavuni magari namba t. 940 bwn toyota coaster na t. 726 dxw toyota coaster kisha kugonga bajaji yenye namba za usajili mc 993 ckb aina ya tvs kisha kuwagonga watembea kwa miguu waliokuwa wakivuka upande wa pili wa barabara. Na kupelekea vifo vya watu wawili 1. Amiri shabani, miaka 15 Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mugabe kidato cha tatu na 2. Isaka Hassan, miaka 26 na majeraha kwa watu 10 wote ni wakazi wa Kimara Suka
Majeruhi hao ni 1. Asha Ramadhani, miaka 43, Mbondei 2. Peris Johnson, miaka 46, 3. Tuli Ambwene, Mnyakyusa, 4. Maria Linda, miaka 15, Mwanafunzi wa st. Gasper se sekondary 5. Ena Gadau Mbena, miaka 42, 6. Marry Modest, miaka 45 Mchaga 7.

Zulfa Hassan, Msambaa miaka 44, 8. Manfred Mtitu Mpagwa, miaka 63, 9. Magreth Alex, Mhehe miaka 18 na 10 Amanda Luembu, miaka 12 Mwanafunzi Darasa la Saba Shule ya Msingi Chuo Kikuu, Majeruhi wote wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali za Mloganzila na Bochi.

Chanzo cha ajali hiyo ni Dereva wa Gari T. 814 dga aina ya scania lori kuendesha gari bila kufuata alama za watembea kwa miguu. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Mloganzila, na Dereva wa gari hilo amekamatwa kwa hatua zaidi za Kisheria.

Jeshi la Polisi Kanda Maaalumu ya Dar es salaam linatoa wito kwa waendesha vyombo vya moto kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama Barabarani ili kuepuka ajali.

Muliro J. MULIRO– ACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM DAR ES SALAM.

Watu kadhaa wahofiwa kufa na wengine kujeruhiwa kufuatia ajali ya lori lililovamia kituo cha daladala cha Kimara Suca jijini Dar es Salaam leo Januari 28, 2022.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Usalama wa Barabarani Taifa, ACP Abdi Isango ndiye aliyefika eneo la tukio, lakini amesema hawezi kutoa taarifa mpaka atembelee hospitali zote ili ajuwe idadi ya majeruhi na waliopoteza maisha.

Mwandishi wa habari aliyekuwepo katika eneo hilo, ameshuhudia baadhi ya majeruhi na maiti ziliogongwa zikiwa zimetapakaa katika eneo hilo, huku nyingine zikiwa chini ya lory hilo.

Kamanda wa Polisi Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amethibitisha watu wawili wamefariki, nane kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mbezi Suka Dar es Salaam, ameeleza waliofariki ni waliokuwa wakivuka kivuko cha watembea kwa miguu.
 
Kuna taarifa za ajali mbaya Kimara Suka. Lori limegonga raia pembezoni mwa barabara. Inasemekana kuna vifo na majeruhi.

Waliopo eneo hilo mtujuze kama ni kweli.

NB: Barabara ya Kimara-Kibaha: Serikali iangalie namna ya kumaliza tatizo maeneo haya
 
Watu kadhaa wahofiwa kufa na wengine kujeruhiwa kufuatia ajali ya lori lililovamia kituo cha daladala cha Kimara Suca jijini Dar es Salaam leo Januari 28, 2022.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Usalama wa Barabarani Taifa, ACP Abdi Isango ndiye aliyefika eneo la tukio, lakini amesema hawezi kutoa taarifa mpaka atembelee hospitali zote ili ajuwe idadi ya majeruhi na waliopoteza maisha.

Mwandishi wa habari aliyekuwepo katika eneo hilo, ameshuhudia baadhi ya majeruhi na maiti ziliogongwa zikiwa zimetapakaa katika eneo hilo, huku nyingine zikiwa chini ya lory hilo.

Baadhi ya watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema gari hilo lilionekana kupoteza mwelekeo baada ya kukatiba breki.

"Mimi nimesimama pembeni naona gari linanifuata na lilikuwa katika spidi kubwa sana niliruka mtaroni ndicho kilichonisaidia bila hivyo sijui," amesema John Kelvin aliyekuwa amepaki boda boda yake pembeni.

“Rafiki yangu mshtuko alikimbia mbio limemkuta huko huko nikamuona anaingia chini ya lori ndio wamemtoa ameshakufa jamani," amesema.

Mmoja wa ndugu wa majeruhi ambaye hakuta jina lake kuandikwa gazetini amesema amefuatwa nyumbani na boda boda akaambiwa mke wake Aisha amekatika sikio.

"Nilitoka nyumbani haraka sana, nilikuwa mke wangu amewekwa kwenye Kirikuu nikamtoa nimeleta mwenyewe hapa Bochi nikasaidia na wengine wawili.

"Ajali ni mbaya jamani maana imewafuata watu pembeni mimi mke wangu alikuwa anaenda kazini jamani hali yake sio nzuri," amesema.

Taarifa ya kamanda wa Polisi
Kamanda wa Polisi Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amethibitisha watu wawili wamefariki, nane kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mbezi Suka Dar es Salaam, ameeleza waliofariki ni waliokuwa wakivuka kivuko cha watembea kwa miguu.
Taarifa ya kamanda wa Polisi
Kamanda wa Polisi Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro amethibitisha watu wawili wamefariki, nane kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha magari matatu katika eneo la Mbezi Suka Dar es Salaam, ameeleza waliofariki ni waliokuwa wakivuka kivuko cha watembea kwa miguu
 
Yaaani hata kama sheria hairuhusu inabidi tu waweke matuta potelea mbali kupunguza hizi ajali, maana hapo barabara hazijakamilika zote, ikikamilika si ndio itakuwa balaa zaidi

Pole nyingi ziwafikie wahanga na wafiwa
 
Back
Top Bottom