Ajali kubwa daraja la mto Nduruma - Arusha

Chammy

Member
Dec 16, 2010
27
9
Ajali mbaya za malori 3 ya mizigo Arusha imesababisha barabara kufungwa na hakuna uwezekano wa kuyatoa hayo magari mapema.

Inasemekana truck moja ilifeli brake na ndipo ilipojaribu kulipia Lori jingine na kujikuta likigongana uso kwa uso na Lori aina ya fuso lililobeba machungwa kuelekea Nairobi.

Hali ni tete na wasafiri wamekwama kwani hakuna gari linaloweza kupita hapo darajani kwa sasa.

attachment.php

Picha ikionesha gari aina ya fuso likiwa limeharibika vibaya.
 

Attachments

  • IMG-20140619-WA001.jpg
    IMG-20140619-WA001.jpg
    107.5 KB · Views: 2,718
  • Arusha 1.jpg
    Arusha 1.jpg
    42.4 KB · Views: 7,011
  • arusha 2.jpg
    arusha 2.jpg
    113.3 KB · Views: 3,291
Ajali mbaya za malori 3 ya mizigo Arusha imesababisha barabara kufungwa na hakuna uwezekano wa kuyatoa hayo magari mapema. Inasemekana truck moja ilifeli brake na ndipo ilipojaribu kulipia Lori jingine na kujikuta likigongana uso kwa uso na Lori aina ya fuso lililobeba machungwa kuelekea Nairobi. Hali ni tete na wasafiri wamekwama kwani hakuna gari linaloweza kupita hapo darajani kwa sasa.

Pole kwa majeruhi wote
 
Hakika tufike mahali, kama Taifa, tukomeshe ajali hizi. Trafiki wanachokagua ni kadi za gari na leseni za udereva. Vehicle Inspectors hawakagui breki wala uimara wa gari. Poleni sana wana Arusha na wote walioumia.
 
Vey sad indeed.

Poleni na natumaini wahusika watajitahidi malori yaondolewe maisha yaendelee.
 
Daah haya malori haya jamani!! Na hapa si pale pale lori la soda lilipoangukiaga mtoni?
 
Sasa hao watu na magari yaliyojazana juu ya daraja hawajui kama ni hatari.madaraja yenyewe ya mda mrefu na hayana uangalizi wa karibu.
 
Mkuu Chammy mbona taarifa yako haijakamilika?

Hakuna majeruhi wala maiti?
 
Last edited by a moderator:
asante kwa picha mkuu mleta mada.
hilo daraja lina bomps kibao ila ajali bado haziishi hapo.
 
Hakika tufike mahali, kama Taifa, tukomeshe ajali hizi. Trafiki wanachokagua ni kadi za gari na leseni za udereva. Vehicle Inspectors hawakagui breki wala uimara wa gari. Poleni sana wana Arusha na wote walioumia.


Kwakweli waonee huruma, kwani wanavijua? Kuna siku pale Doma mmoja kanambia "nenda kapige photocopy motor vehicle halafu peleka TRA wakugongee mhuri usitumie original itachakaa"
 
Taarifa za awali kuhusu waanga wa hii ajali ni kwamba dereva wa Lori aina ya fuso kvunjika miguu na Hali yake si nzuri sana,yupo hospitali.Msaidizi wake ana majeraha si makubwa sana. Wale wa malori yaliyobeba makontainer wote wamenusulika.
 
Back
Top Bottom