Anyongwe
Nani ana ubavu wa kukiotesha kibarua cha chenge na wenzake majani? Naona wewe unaota ndoto za mchana na siasa za Tz huzijui kabisaa. Nani wa kusema katika chama cha magamba kukiotesha kibarua cha chenge na wenzake majani? Nape alikurupuka hata mwezi haukuisha akanyamazishwa kimyaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!Kwa vile kibarua chake karibu kitaota majani anatafuta namna mbadala ya kujikimu.
Huyu Baba ni Mtanzania kweli?
unamaanisha?hehehehe...Chenge the Clean Man = CCM
Malumbano yasio kuwa na tija.Looo. Mdini = msema kweli. Kwa hapo ume analyze vizuri sana. Mimi ni mdini tena Muislaam, Jee wewe?
Hiyo picha yako inaonesha una busara kumbe!!! huo utaalam wa sheria alionao sana huyo Chenge si ndio ule ulioitia aibu serikali yake mpaka waziri wa mambo ya nje analalama kwa waingereza? Zaidi ya miaka kumi iliyopita alikuwa mbumbumbu wa kisheria tena akiwa mwanasheria mkuu, akaishauri serikali kununua rada kwa double price hakuona athari zozote. Huo ujuzi kautoa wapi leo kuona athari za kutoilipa Dowans?Nakumbuka Bunge lililopita, Mbunge mpya kwa tiketi ya cdm, Tundu Lissu, alipokuwa anajitafutia umaarufu Bungeni kwa kufanya u"tundu" na kuzua malumbano kwa kila hoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alisimama Chenge na kumpa Tundu hoja moja tuu ya kisheria ambayo ilimfanya Tundu kuwacha utundu wake wa kulumbana, kwani kwa pale ilidhihirika wazi kuwa Tundu ni katoto kwa Chenge kisheria. Nani anaekumbuka?
Kwa mantiki hiyo, ikiwa Chenge kasema fedha ya Dowans walipwe, basi ujuwe kaiona sheria kwa jicho la wazi na anajuwa kutokuwalipa Dowans kunaweza kuleta utata zaidi na kuliingiza Taifa kwenye utata zaidi, Jee, inawezekana kuwa hata Symbion hawatakubali kulipia mitambo ambayo bado ina deni?
Kwa Nchi kama TZ mafisadi HUMWAGA MBOGA wengine wakimwaga ugali!!Kwa nchi kama China Mafisadi hunyongwa..hivi haoni aibu.
Jee kuna sababu yoyote ya maana kwa kutumia huduma ya mtu halafu usimlipe?
kwa ulichokiandika hapo unataka kutuambia kwamba Chenge anajua sana sheria siyo?Inawezekana kwamba anaijua kweli sheria lakini kujua kwake sheria hakujaisaidia hii nchi!Serikali iliingia mikataba mibovu ya madini Chenge akiwa mwanasheria mkuu,je kwa wakati huo alikua hajui sheria au alikua na manufaa binafsi?kama nitakua sahihi basi inawezekana pia akawa ana manufaa binafsi katika hili suala la Dowans.Tatizo si Chenge kujua sheria bali ni kujua kwake sheria kunaisaidia nini hii nchi!Nakumbuka Bunge lililopita, Mbunge mpya kwa tiketi ya cdm, Tundu Lissu, alipokuwa anajitafutia umaarufu Bungeni kwa kufanya u"tundu" na kuzua malumbano kwa kila hoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alisimama Chenge na kumpa Tundu hoja moja tuu ya kisheria ambayo ilimfanya Tundu kuwacha utundu wake wa kulumbana, kwani kwa pale ilidhihirika wazi kuwa Tundu ni katoto kwa Chenge kisheria. Nani anaekumbuka?
Kwa mantiki hiyo, ikiwa Chenge kasema fedha ya Dowans walipwe, basi ujuwe kaiona sheria kwa jicho la wazi na anajuwa kutokuwalipa Dowans kunaweza kuleta utata zaidi na kuliingiza Taifa kwenye utata zaidi, Jee, inawezekana kuwa hata Symbion hawatakubali kulipia mitambo ambayo bado ina deni?
Asee hili andiko nimelipenda liko kwenye kitabu gani?
Siku 90 watatatoka tu.Nape ndiyo kiboko yao...watakoma
hehehehe...Chenge the Clean Man = CCM