Kiukweli wengi wanaomkosoa mtoa mada wakidai ni ubinafsi na uchoyo me napingana nao. Unakujaje gheto kwangu bila taharifa?
Mkuu binafsi huwa kama ndo muda nimetulia natafakari life na mipango ya hapa na pale then ukafika ghafla bila taharifa yaani mda huohuo nakuambia nina safari kuna sehemu nataka niende kukamilisha harakati. Wengi wanaweza ona hiki jambo la kawaida ila ni jambo jema sana kumjulisha mtu kabla ya kufika kwake kila mmoja anahitaj uhuru so unapokuja ghafla hata maongezi yanakuwa ya kulazimisha sana.
Mshkaj unakuja gheto, nijulishe kisha nakupanga uje au lah kiasi kwamba ukifika hata mzuka wa kupiga story mbili tatu inakuwepo na unaona umuhimu wa kampani kwa siku hiyo.
Toa taharifa unapoenda kwa mtu, ni ustaarabu wa kawaida unaonyesha kiwango cha hekima na busara yako. Acha kujiondokea kisha unafika mshkaj anaanza kukujudge kama huyu wa mtoa mda, mara ananuka jasho, sasa huo ni ushkaji au unafiki.