Airtel Tanzania yapandisha gharama za internet!

Status
Not open for further replies.
Asante mrimi kwa taarifa, hata huku niliko network imeanza kupatikana kwenye saa tano hivi, bt muwe mnatujulisha mapema
 
Bad news
Nimejaribu kujiunga kwa maelezo yao nikiwa na salio la sh 2800 kwa kutuma 500MB ikasema sina salio la kutosha, nikajaribu 250MB ikasema sina salio la kutosha, nikajaribu 150MB ikasema sina salio la kutosha, mwisho nikajaribu 50 MB ikakubali bila kusema imenikata sh ngapi wala ni kwa muda gani.
Na ukiangalia salio unatumiwa majibu haya "Ndugu Mteja Salio lako ni: 1. 50MB : 50MB 2. BUNDLE : 1MB"
Sasa sijui kama nilitakiwa nitumie MWEZI au vipi?
 
Bad news
Nimejaribu kujiunga kwa maelezo yao nikiwa na salio la sh 2800 kwa kutuma 500MB ikasema sina salio la kutosha, nikajaribu 250MB ikasema sina salio la kutosha, nikajaribu 150MB ikasema sina salio la kutosha, mwisho nikajaribu 50 MB ikakubali bila kusema imenikata sh ngapi wala ni kwa muda gani.
Na ukiangalia salio unatumiwa majibu haya "Ndugu Mteja Salio lako ni: 1. 50MB : 50MB 2. BUNDLE : 1MB"
Sasa sijui kama nilitakiwa nitumie MWEZI au vipi?

Wanaringa. Wameona wenzao wako high sasa na wao wanaadjust. Sikatai kweli ilikuwa cheap, lkn vipi kuhusu speed manake tulikuwa tunalivumilia hilo kwa kupenda slop
 
Habari ya asubuhi wana JF.

Asubuhi ya leo imekuwa ni mbaya sana kwangu, mimi kama walivyo wateja wengine wa airtel, nimekuwa nikitumia huduma ya airtel internet, kwa kutumia kifurushi cha 400MB/2500Tsh tangu mwaka 2010. Leo asubuhi nikagundua kuwa kifurushi changu kimekwisha. Basi kama kawaida, nikanunua tena vocha ya Tsh 2500, nikaingiza, nilipo subscribe ile huduma yetu rafiki kwa kutuma neno internet kwenda 15444, nikapata ujumbe ambao sikutarajia kuupata asubuhi hii, ujumbe ulisomeka hivi
"Name:
Number: 15444
Content:
Neno ulilotuma sio sahihi, Tafadhali chagua kati ya :- 10MB,25MB,50MB,150MB,250MB,500MB,1GB,2GB,5GB,15GB,30GB,SIKU,WIKI,MWEZI ama SALIO kwenda 15444.Asante.
Time: 01/03/2012 08:14:49"
Nikajaribu mara kadhaa nikapata ujumbe huohuo. Ndipo nilipogundua huduma yetu hii kipenzi is no more. Kwa hela hiyo hiyo nikajaribu kutuma mwezi, nikaambiwa hela haitoshi, nikajaribu wiki, nayo nikaambiwa hela haitoshi. Ndipo nikatuma 10MB ambayo naitumia hivi sasa na muda si mrefu itaisha.

Naomba kuchukua wasaa huu kuwaomba ndugu hawa wa Airtel kuirudisha huduma hii, kwani imewakusanyia wateja wengi wa internet ambao wengi watalazimika kuachana na huduma zao kama ile huduma wameiondoa. Mimi binafsi nina modem ya mtandao mwingine wa hapa TZ lakini niliichakachua ili niweze kutumia airtel kitu ambacho ni faida kwa airtel.

PLZ AIRTEL THINK TWICE!!

BAD DAY!!

Huduma ya 400MB for 2500 kwa mwezi bado ipo, service hii ya internet kwa mwezi ipo kwa two categories kwa sasa mitambo ipo katika marekebisho kwa kuweka arrangement nzuli za bundles mdau jaribu tena baadae itakuwa sawa.
 
Inabidi watupatie maelezo ya ziada la sivyo wasije wakawa wanatuibia, maana hata gharama za mitandao sasa wamepandisha kinyemela. Ile shilingi kwa sekunde naona haipo tena maana unakuta pesa iliyokatika ni nyingi sana japo mtandao mmoja
 
Mimi nimepata bundle yangu ya 400MB jana tu na naendelea kutesa nayo hadi sasa. Labda iwe ndio ya mwisho, ambayo kwa kweli itakuwa mbaya sana.
 
Nimenunua recharge vocha bahati mbaya muuzaji alikuwa na haraka kaikwaruza vibaya akarudia rudia kuingiza na SIM yangu ikafungiwa ku-recharge.

Sasa tangu jana usiku nahangaika ku-dial 100 ambayo ni huduma kwa wateja lakini kinachoonekana ni network busy. Je, mmeweka hiyo huduma ya nini kama wateja hawawezi kuitumia????

Nawapa mpaka leo usiku kama hamfungui namba yangu nahamia Vodacom.
 
Mimi nimepata bundle yangu ya 400MB jana tu na naendelea kutesa nayo hadi sasa. Labda iwe ndio ya mwisho, ambayo kwa kweli itakuwa mbaya sana.

hata hivo bado tunawasihi wazidi kupunguza bei ya hiyo 400MB kiukweli wafanye walau elfu mbili! au kama vipi waongeze bandle iwe 500MB! wanatunyonya mno hawa!
 
Duh kama itakuwa hivyo nimekwisha maana hata modem yangu ya voda niliuza nije huku aitel mteremko
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom