Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,780
- 10,710
Wakuu, Jana nilipatwa na mkwamo wa kununua umeme ambapo nilikuwa napokea ujumbe huu:
Unahitaji kupata Key Change. Wasiliana na TANESCO kwa 0768985100. Key Change Tokens are due. Please call 0768985100 or visit any nearby TANESCO office (038).
Niliamua kupiga namba huyo hapo juu, ikaniacha na kilio. Nikapiga ikapokelewa na mhudumu, wakati tukitambulishana simu ikakata. Nikajua kubwa nitahitaji kuwa na salio kwenye simu na si kifurushi. Nikaweka shilingi 1000, nikapiga tena. Mara hizi tukafikia sehemu ya mhudumu kuniomba mita namba. Nilipomaliza kutaja tu, ikakata salio limeisha. Sikuamini, nikaweka vocha ya 1000 tena. Nikapiga, nikaishia kutaja mita namba, salio likaisha! Sikuendelea tena. Jamani, huyo so wizi wa mchana kweupe?
Wakati nahangaika kununua umeme kwa airtel money, kuna pesa ilikatwa. Najaribu kuwapigia airtel money kwa namba 100, hakuna option ya kuongea na mhudumu. Hii ni mbaya sana na ni njia ya kuwakatisha tamaa wateja wasitafute huduma. Je, wewe una experience gani na hii mitandao?