Airtel mtandao wa wizi

simba wa dodoma

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
925
1,010
Week moja iliyopita nilinunua umeme kupitia airtel money cha ajabu mpaka leo sijapata meseji hela yangu wakaiba elfu 10 ukiwapigia huduma kwa wateja hawapokei simu.

Jana tena nimelipia kingamuzi hela wamekata ila kingamuzi hakijaanza kufunguka ukiwapigia hawapokei nimejaribu kuwapigia huduma kwa wateja wa dstv wanasema hela haijafika kwenye account ila kwenye salio langu wamekata.

Huu mtandao ushakua wa wizi kabisa ndugu zangu msijaribu kuutumia mtaibiwa hela zenu sio salama kabisa na hawana no ya kuongea huduma kwa wateja.

Serikali kupitia wizara yenye dhamana shughulikeni ili tatizo wananchi wanaibiwa fedha zao hivi hivi.

Naambatanisha na baadhi ya watu wengine wakiendelea kuwalaaumu kwenye page zao.
Screenshot_20200614-075146.jpeg
Screenshot_20200614-075215.jpeg
Screenshot_20200614-075520.jpeg
 
Ulichosema ni sahihi, hawa jamaa wamekuwa wahuni sana siku hizi, ikifika mida ya jioni mtandao hakuna, kama kuna watu unahitaji kuongea nao mida hiyo unaweza ukalia! Pia utaratibu wao wa kuongea na mtoa huduma wameu-complicate utafikiri unaomba kibali cha kuonana na rais. hovyo kabisa!
 
napita wakuu, Mimi natumia Airtel ila si Airtel money
Upande wa data,haisumbui kabisa naenjoy.

Kero yangu wanatoa mb chache sana alafu hawana kifurushi cha video tu cha kuangalia YouTube kama wafanyavyo Tigo.

Nawatakia Jumapili njema ya Ibada.
 
Ni kweli, nilishanunua LUKU umeme nikaupata baada ya wiki na karaha ya kwenda ofisini kwao, ukipiga 100 ni kastama kero,
Wiki 2 zilizopita nikatumia airtel money kununua bando hela wakakomba bando sikupata..kuwapigia simu wakadai 24hrs nitarekebishiwa, 2wks zikapita nikaenda ofisini kwao wakasema bando uliunganishwa na ulilitumia usiku...
Nikawaambia wameniibia, usiku huo sikuwa na bando nililila mapema mpaka saa 9 usiku, nikaamka nifanye kazi za watu nikashindwa...wamekomaa nikawauliza iweje nikanunue tena bando kesho yake?? Hawa jamaa ni kutumia vocha ya kukwangua..

Airtel MONEY siyo ya kutumia kwa huduma zozote zile! Be warned!
Wanadisable mtandao makusudi waibie wateja!
TCRA wanaangalia gawio tu kwa serikali!

Everyday is Saturday......................... :cool:
 
Huku mikoani Airtel ni kero hasa network kua unstable, unaongea simu inakatika tu alafu customer care wanatoa majibu ya kipuuzi kwa issues sensitive, naona mmetuchoka!
 
Hawa jamaa wajinga sana.... Juzi waliniibia vocha yangu nikiwapigia naona hakuna kipengele kuongea na muhudumu maana wanabahati kila siku nawasaka nikiwapata nitawatapikia yote
 
Hawa jamaa wajinga sana.... Juzi waliniibia vocha yangu nikiwapigia naona hakuna kipengele kuongea na muhudumu maana wanabahati kila siku nawasaka nikiwapata nitawatapikia yote
Nafikiri kampuni uongozi, menejimenti, watumishi wa AIRTEL wote, wamepitia kozi na ni wahitimu wa kwanza kile chuo pendekezwa cha wizi...

Huduma kwa wateja hakuna, ni KASTAMA KERO TUPU..

Everyday is Saturday........................ :cool:
 
Mimi sijui hii Kampuni wanampango gani nayo.....

Kama kuna muhusika humu awafikishie ujumbe warudishe kitengo cha customer care ....
 
Airtel money wakati mametoa charges za kutuma pesa airtel kwa airtel walijitangaza sana sasa wana charge kimya kimya na hawatuambii chochote; hatujui hata viwango vya chagres zao. Nimetuma elfu 12 kwa namba ya airtel wamketa 1000 pllus.
 
Back
Top Bottom