ajent45
Senior Member
- Mar 20, 2017
- 158
- 162
Mimi ni wakala na nina laini za uwakala za mitandao yote: Tigo, Voda, Halotel, na Airtel. Sasa, kwenye hizi laini, Airtel ndiyo wanaongoza kwa kunipa kamisheni kubwa. Hii ni kwa sababu huku kwetu kuna wateja wengi wa mtandao huu. Pia, nina laini za lipa kwa simu kwa mitandao ya Voda, Tigo, na Airtel, ambazo ninazitumia.
Mwezi wa nane, Tigo wamenipa 77,000, Voda 78,000, Halotel 17,000, na Airtel nilishazoea kupata laki na chenji, lakini nakuta wamenipa 7,000. Nimeuliza kwa watu, eti kosa hela za lipa kwa simu kwa Airtel huwa naamishia laini ya uwakala, na majina yanafanana. Sasa, mbona mitandao mingine majina yanafanana na hawana shida na mimi? Napiga kazi na nategemea hapa, lakini wao wananiletea huu upuuzi.
Nilipiga huduma kwa wateja, na wao hawajui. Dah! Nimepigwa, naomba msaada.