Airtel kwa wizi huu nawahama

Chimo

JF-Expert Member
Aug 31, 2008
711
500
Nitasikitika mamlaka Kama hazitakaa kuichukulia hatua kali za kisheria kampuni hii ya mawasiliano ya Simu za mkononi ya Airtel hapa nchini kwetu kwa wizi.

Airtel wafanyakazi wenu wasio waaminifu hawawezi kuzibeba wala kuwa Na Dhamana baina yao na sisi wateja wenu bali ni nyie waajiri wao kwa kushindwa kuwa waangalifu mnapowapa ajira wezi na wasio waaminifu nafasi kwenye kampuni yenu Airtel wamekuwa wezi Hasa kwenye upande wa Bando zao (Bundles) tena bila aibu hivi nyie wafanyakazi kwanini hamkuwa wezi kipindi bando zikiuzwa na kampuni yenu kwa bei poa na kwa wingi wa MBs Na Ma GB Mnakuja kuwa wezi kipindi hichi Kampuni imepandisha bei?

Kwa hali hii bora nitafute mtandao mwingine huku nikitafuta Simu yenye uwezo wa kutumia line mbili (Duos) huku nikibaki na line lenu kwa ajili ya kupokelea Ni Ujinga kuendelea kununua Bando linalotuniwa na ma Super Users wenu kwenye Server zenu bila aibu unanunua GB 2 Ndani ya masaa mawili imekwisha kweli? Sijadownload chochote wala kuUpgrade kuUpdate App yoyote Huu wizi pelekeni India
 

keypass

Member
Dec 2, 2017
79
150
Shida Mitandao yetu hii, hapa unavyolalamika kuhusu Airtel kuna mwingine huko anatamani apasuke anawalalamikia Halotel na Voda. Komaa nao hao hao tu. Unaweza zunguka Mitandao Yote afu ukakutana na Upuuzi unaofanana.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
58,974
2,000
Sijawahi kukopa na sijui wanakopaje, Jana nikashangaa napiga simu Kuna kimwanamke kinajiongelesha eti nadaiwa, nadaiwa Nini?

nikapiga 100 kuuliza hilo deni nadaiwa deni gani, maaana huwa vifurushi najiunga kutoka kwenye salio la Airtel Money.

Akaniambia eti kulikuwa na tatizo la ufundi wataondoa hicho ki reminder. Hadi Sasa hawajakiondoa.
 

Chimo

JF-Expert Member
Aug 31, 2008
711
500
Sijawahi kukopa na sijui wanakopaje, Jana nikashangaa napiga simu Kuna kimwanamke kinajiongelesha eti nadaiwa, nadaiwa Nini?

nikapiga 100 kuuliza hilo deni nadaiwa deni gani, maaana huwa vifurushi najiunga kutoka kwenye salio la Airtel Money.

Akaniambia eti kulikuwa na tatizo la ufundi wataondoa hicho ki reminder. Hadi Sasa hawajakiondoa.
Bujibuji kote huko nimewahi kuzungukia ila hapa ni kiboko hawa ni wezi wasio na Aibu na wala hawana aibu pia hawajui kuiba wanadhani wote wanaotumia Simu za mkononi ni washamba.
 

FOCAL

JF-Expert Member
Jun 25, 2019
1,226
2,000
Bujibuji kote huko nimewahi kuzungukia ila hapa ni kiboko hawa ni wezi wasio na Aibu na wala hawana aibu pia hawajui kuiba wanadhani wote wanaotumia Simu za mkononi ni washamba
Mimi hutumia moderm kwenye PC kwa ajili ya mtandao. Jana nimetoa laini ya airtel nikaweka kwenye kitochi na kujiunga bundle ya MB 500. Baadaye nikawa busy sikutoa laini kwenye kitochi, baada ya muda nasikia SMS kuangalia wananiambia umetumia 75% ya bundle lako. Nilishangaa sana simu ya kitochi (Techno) tena zile za mwanzoni kabisa inatumia bundle.
 

Msanii

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
8,546
2,000
Nitasikitika mamlaka Kama hazitakaa kuichukulia hatua kali za kisheria kampuni hii ya mawasiliano ya Simu za mkononi ya Airtel hapa nchini kwetu kwa wizi.

Airtel wafanyakazi wenu wasio waaminifu hawawezi kuzibeba wala kuwa Na Dhamana baina yao na sisi wateja wenu bali ni nyie waajiri wao kwa kushindwa kuwa waangalifu mnapowapa ajira wezi na wasiowaaminifu nafasi kwenye kampuni yenu Airtel wamekuwa wezi Hasa kwenye upande wa Bando zao(Bundles)tena bila aibu hivi nyie wafanyakazi kwanini hamkuwa wezi kipindi bando zikiuzwa na kampuni yenu kwa bei poa na kwa wingi wa MBs Na Ma GB Mnakuja kuwa wezi kipindi hichi Kampuni imepandisha bei?

Kwa hali hii bora nitafute mtandao mwingine huku nikitafuta Simu yenye uwezo wa kutumia line mbili (Duos)huku nikibaki na line lenu kwa ajili ya kupokelea Ni Ujinga kuendelea kununuwa Bando linalotuniwa na ma Super Users wenu kwenye Server zenu bila aibu unanunuwa GB 2 Ndani ya masaa mawili imekwisha kweli? Sijadownload chochote wala kuUpgrade kuUpdate App yoyote Huu wizi pelekeni India P u m b a v u
Ninapata hisia kwamba TCRA wapo nyuma ya wizi huu.

Ina maana hakuna mfanyakazi wa TCRA anayetumia hii mitandao akaona mwenendo mbovu wa hii mitandao?

Mimi ninachokiona ni kwamba tupige kelele serikali iifumue TCRA maana ndiyo behind ya haya yote
 

Siasa mbaya sana

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
1,122
2,000
Kuna siku nilijiunga bando la gb 1 voda aisee skuamini kilichotokea ndani ya masaa Kama manne tuu bando likawa limeisha aisee sjawah kujiunga tena
 

Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
554
1,000
Aiseee airtel ni wezi mnooo. Mimi nilinunua 1.3GB kifurushi cha 3000 kwa wiki. Siku mbili tu nikaambiwa umetumia salio lako lote la MB 700.
Daah nilishangaa sana sasa imeluaje mb 700 wakati nilinunua gb 1. Hapo hapo nikawahama nikaona hawa jamaa ni wezi sana yani kwenye kifurushi kwenye menu yao wameweka gb 1.3 kumbe ni mb 700 tena kwa 3000.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom