dada white
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 1,228
- 515
Moja ya kitu ambacho kilikuwa kinavutia vijana kununua line za airtel na kuachana na dhana iliyozoeleka kuwa airtel ni mtandao wa watu walionazo tu hapa Tz ni ile bundle yenu ya MB400 kwa siku 30 ambayo ilikuwa ikiuzwa kwa sh 2500.Naona hii bundle imebadilika bei na kuwa ya ni Tsh3500 kwa siku 10 tu na unapewa MB500.Kwa mchanganuo ina maanisha mtu anatumia Tsh 350 kwa siku hii kitu ni gharama sana hasa kwa watu wenye kipato cha chini.Kwa kulinganisha ni kifurushi cha extrema park cha tigokinakuwa kina faida sana kwa maana unapata sms zaidi ya 100,dakika 15,Mb50 kwa masaa 24.Kwa kweli airtel mtatufukuza wengi kwa ongezeko hili.Kile kifurushi chenu kilikuwa kina induce watu wanunue line zenu. Mi mwenyewe mtanikosa kwa kweli