Torra Siabba
Senior Member
- Jul 24, 2016
- 105
- 102
Shirika la Ndege Tanzania ATCL ni moja ya mashirika ambayo kwa kipindi cha nyuma walikua na nidhamu ya muda wa kusafirisha abiria kuliko wengine Hususan kipindi cha mwendazake JPM Magufuli, Usiku wa kuamkia jana Aprili 16 nilipaswa kusafiri kutoka Mwanza kwenda Dar majira ya saa 8:30 usiku, lakini ndeg iliondoka Saa tatu asubuhi, watu tumekesha Uwanja wa Ndege Mwanza, na Mbaya ni kwamba ATCL walikua wanajua wazi kwamba ndege yao itakuja Asubuhi lakini wakatupambapamba kwamba ndege inakuja mpaka kukacha.
Na hii sio mara ya kwanza kwa ndege hizi kutokwenda na wakati ambao wanakua wamepanga na ukiona safari ni saa mbili Usiku badi ujue kuondoka ni saa nne au saa sita Usiku.
kinachoniumiza ni kwamba tumezoea mashirika mengine ya Ndege Kote duniani kunapokua na dharula mashirika yanaingia gharama ya chakula na malazi kwa wateja wao lakini Air Tanzania wako radhi wakutelekeze VIP Mpaka kuche hata maji ya kunywa hawatoi.
Nadhani wanatukosea sisi wateja wao na natamani ndege ikipata dharula watuhudumie sisi Abiria ila sio kututelekeza kama Mizigo.