Onesmo Olengurumwa alia na Air Tanzania baada ya kutelekezwa kwenye uwanja wa ndege, Lusaka

SOVIET UNION

JF-Expert Member
Sep 2, 2017
455
1,283
Air Tanzania , Mmebadilisha ndege ya Lusaka Dar es Salaam bila utaratibu , Watu zaidi ya 10 tumeambiwa ndege imejaa baada ya kuletwa ndege ndogo.

Cha kushangaza zaidi hamna utaratibu wa kuhamishia abiria kwa ndege zingine hapa na zipo nyingi zinazofika Dar Leo usiku kama Ethiopia na Airlink.

Hakuna huduma ya kurizisha hapa , watu wanaisema vibaya ndege yetu kwa kukosa umakini. Kwanza imechukua zaidi ya masaaa mawili hapa kucheck in watu wasiofika hata mia. Tupeni utaratibu abiria walioachwa hapa - Mnashindwaje kuwa na makubaliano na ndege zingine kwa ajili ya kusaidia hizi challenges.

Mkiendelea hivi abiria watawakimbia - Hakkisheni abiria tulioachwa kwa sababu zenu tunafika Dar leo , vinginevyo mtajiingizia hasara zisizokuwa na msingi watu watakapo amua kwenda mahakamani.

Air Tanzania Company Limited Jana imebidi tujiokoe wenyewe na kuchukua ndege zingine, mimi nilikuwa na Ethiopians Airline pamoja na wenzangu wanne . ATC hadi sasa hamna muelekeo wa kurudisha hela zetu wala kutaka kujua hali za abiria mliowatelekeza.

Hizi ndege ni zetu lakini tu naona huruma sana Taifa letu kwa namna ambavyo mnaendesha biashara hii ya ndege. Mnaharibu sana jina la ATC. Within seven days muwe mmetulipa hela zetu , Nina list ya wote walioachwa na contacts zao.
FB_IMG_1670122667293.jpg
 
Sasa hivi tunafanya vitimbi vya maksudi ili apewe mwekezaji. Kule kivukoni Magogoni to Kigamboni tayari vitimbi vimezidi keshapewa Bakhresa.

Bandarini Mchakato unaendelea tuwape wawekezaji.

Huko kwenye ndege subir sarakasi kama zoteee kuanzia Januari kufikia June kwisha kabisaaa, hiyo ndege kukamatwa Uholanzi ni picha limeanza. Bwana yule kesha ichukua Coastline Air hashindwi jambo.
 
Hovyo kabisa, what if kuna abiria wana flight to connect? Shida sana hii.
 
ATCL ishashtuka maana wadaiji wanazizaka ili walipwe .serikali wekeni wazi mnadaiwa na wangapi !

mswisi wa bagamoyo
msauzi wa manyara au arusha
....

mtaluka humu humu ndani
 
Sasa hivi tunafanya vitimbi vya maksudi ili apewe mwekezaji. Kule kivukoni Magogoni to Kigamboni tayari vitimbi vimezidi keshapewa Bakhresa.
Bandarin Mchakato unaendelea tuwape wawekezaji.

Huko kwenye ndege subir sarakasi kama zoteee kuanzia Januari kufikia June kwisha kabisaaa, hiyo ndege kukamatwa Uholanzi ni picha limeanza. Bwana yule kesha ichukua Coastline Air hashindwi jambo.
Coastline Air ilikuwa ya Serikali?
 
Back
Top Bottom