Air Tanzania kwanini haitui Nairobi?

Hapa ni sawa tu na kuuliza ni kwanini basi la Hood lisianzishe Route ya Dar - Arusha, akapambane na wakongwe wa ile njia...
Unamaanisha nini mkuu kwa hii comment yako!!..maana ninavyojua mimi HOOD iliwahi kudominate route ya Arusha Dar enzi hizo kabla haijafa na kuna kipindi ilikuwa Arusha to Nairobi
 
Wanakwenda; hiyo bni ruti ya siku nyingi sana. Inawezekana hawajaiandika kwenye vijitabu vyao vipya lakini ruti hiyo ipo.

Ndiyo iliyowahi kusababisha serikali ya Tanzania wakati wa Magufuli ifute leseni ya KQ kutua nchini kwa sababu Kenya walipofungulia ndege za nje kuingia kwao wakaiacha ATCL. Magufuli akipga tit for tat, ikabidi Kenyata aseme basi yaishe wakaifungulia ATCL.

1657473599152.png
 
Nimeangalia ruti za Shirika letu sijaona Dar-Nairobi, kuna sababu yoyote ya msingi labda ? Kwani hiyo ruti kwa maoni yangu ni nzuri hata kwenye mambo tu ya utalii, mfano kuna mashirika mengi makubwa ya ndege hayatui Dar lkn yanatua Nairobi halafu Kenya airways inaleta abiria mpaka TZ, sasa kwa nini hatuendi huko ?
Labda wanatudai
 
Wanakwenda; hiyo bni ruti ya siku nyingi sana. Inawezekana hawajaiandika kwenye vijitabu vyao vipya lakini ruti hiyo ipo. Ndiyo iliyowahi kusababisha serikali ya Tanzania wakati wa Magufuli ifute leseni ya KQ kutua nchini kwa sababu Kenya walipofungulia ndege za nje kuingia kwao wakaiacha ATCL. Magufuli akipga tit for tat, ikabidi Kenyata aseme basi yaishe wakaifungulia ATCL

View attachment 2286557
Jiwe alikuwa na jazba sana ndiyo maana aliikwamisha nchi yetu kwa majirani zetu
 
Jiwe alikuwa na jazba sana ndiyo maana aliikwamisha nchi yetu kwa majirani zetu
Tit for tat. Hakuwa na makosa; jirani yako hawezi kusema wewe usiingie ndani ya nyumba yake lakini yeye anataka aingie ndani ya nyumba yako.

Hata wakenya wenyewe wengi walisema serikali yao ilikuwa imekosea kuitenga Tanzania. Usipokuwa kiongozi thabiti kama Magufuli, basi utaonea sana na majirani zako, hasa Kenya.

Majuzi tu wamezuia maroli ya Tanzania yasingize mahindi nchini kwao bila taarifa yoyote na kuwaacha wamekwama hapo mpkani, wakati ni wao wenyewe wali[pokuwa na njaa walikuja kuomba kuuziwa mahindi hayo wakati wa Magufuli siku waliporudisha dhahabu iliyoibiwa Tanzania
 
kandege hako kana baguliwa sana kwa sababu hata kaki haribika hakuna Mbadala mpaka kaende karakana karudi!! halafu ATC washamba sana! wamekaa kiswahil Swahili sana!

yaani wakihairisha safari unzo paswa kenda wanawacha hapo uwanjani mjijue!...wanaona ni hasara kuwalisha na kuwapa mahali pazuri pa kujihifadhi!! ukisafiri na hii utakoa hasa!! hawajali muda wao!

mashrika mengine ya ndege mnapewa chakula na mahali pazuri pa kulala!....wakichelewa abiria mnapewa chakula kizuri ajabu!
 
Back
Top Bottom