AIR MSAE: Mnalikumbuka hili basi?

AIR MSAE: Mnalikumbuka hili basi?

Poleni mkuu...ila hivi ile ajali yao iliyomaliza zaidi ya watu 20 nadhani ilitokea mwaka 1999....
Maana nakumbuka baada ya ile ajali basi mimi ndio nikawa napanda sana haya mabasi nikiwa na imani hayawezi tena kupata ajali...

nalikumbuka sana mkuu.

na ni gari ambalo familia yetu haiwezi kulisahau kamwe..

Kwenye ajali ya 1995 tulimpoteza mjomba wetu mpendwa, Jaspert..(R.I.P)..
 
Nikiwa Arusha enzi hizo...nilipanda sana Msae maana wenyewe tulikuwa tunaita "chai Arusha, ugali Dar".....

Mie nilikuwa mdau wa Dar express though nikikosa napanda Air Msae, pia kulikuwa kuna bus moja jamii ya haya Taqwq, Taafiq lenyewe lilikuwa linaitwa TAWHEED kama sikosei moja lilikuwa limeandikwa nyuma KOFFI ANNAN na lingine limeandikwa KITI MOTO yalikuwa yanatembea mpaka basi
 
nani anakumbuka kipindi hicho salehe bus, midimu bus mwezi mpya, trans afrika, Tanganyika bus, na mengine mengi yalishakwisha.
 
nani anakumbuka kipindi hicho salehe bus, midimu bus mwezi mpya, trans afrika, Tanganyika bus, na mengine mengi yalishakwisha.
Hii Mwanza sasa na mikoa jirani ya Tabora na Shinyanga, Tanganyika yupo ila kwa style nyingine ila kuna gari inapiga Musoma - Mwanza kwa jina la Sandhu, na njia ya Mwanza - Dar enzi hizo kulikuwa na Mashiku Investment huku Dodoma to Dar kukiwa na Champion na Yarabi Salama kabla ya kupata ajali mbaya na kusababisha mfumo huu wa sasa wa mabasi kusafiri mchana
 
Umenikumbusha mbali sana, wale wa matawi ya juu(VIP Class) na watalii wakizungu walikuwa wanapenda sana kusafiri na basi la FRESH YA SHAMBA. Hilo basi mbali ya kuwa ni Luxury lilikuwa na upekee wake, kwa mfano Lilikuwa na Rangi nyeupe kabisa, Nauli yake iko juu sana, Ni lazima ukate tiketi siku moja kabla(Booking), Halisimami ovyoovyo njiani, kuna wahudumu wanatema ung'eng'e, Kuna Stereo muziki laini nk.
Nakumbuka 'ascent' ya kike ya mzungu kwenye tangazo lao kupitia Radio One mwaka 1996 ikisema ''Safiri kwa raha mustarehe na mabasi ya Fresh ya Shamba''

Humo utasafiri na Watalii, wafanyabiashara mashuhuli, Wakurugenzi, Wabunge, Wakuu wa mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wanandoa wapya(Honeymoon)
 
Poleni mkuu...ila hivi ile ajali yao iliyomaliza zaidi ya watu 20 nadhani ilitokea mwaka 1999....
Maana nakumbuka baada ya ile ajali basi mimi ndio nikawa napanda sana haya mabasi nikiwa na imani hayawezi tena kupata ajali...

Mkuu hili gari liliwahi kupata ajali tena December 1995..

Na alifariki ancle wetu. Jaspat..

Alikuwa pamoja na binamu zetu ambao walipata majeraha makubwa..

Mpaka leo wangalinayo, ila Mungu aliwasaidia sana

Wanaendelesa na maisha ya kawaida..
mmoja yupo hapo Dar na Mwingine anaishi shinyanga wangali na mafanikio..
Nakumbuka kabisa hili tukio ni la 1995 mwezi disemba!!
 
Kuna ngoma ilikuwa inaitwa mwanamara, mugumu - musoma, terema bhaghambe, musoma - ngoreme ikizikosa inabidi utembee kkwa mguu
 
Naam kaka nadhani hayo magari uliyoyataja yalikuwa yakifanya routes za Dar - Nairobi kupitia Namanga na Arusha...

Mie nilikuwa mdau wa Dar express though nikikosa napanda Air Msae, pia kulikuwa kuna bus moja jamii ya haya Taqwq, Taafiq lenyewe lilikuwa linaitwa TAWHEED kama sikosei moja lilikuwa limeandikwa nyuma KOFFI ANNAN na lingine limeandikwa KITI MOTO yalikuwa yanatembea mpaka basi
 
Nakumbuka kabisa hili tukio ni la 1995 mwezi disemba!!

Ooh! basi 1999 kulikuwa na ajali mbaya sana iliyohusisha hili basi maeneo ya Misugusugu kama sikoe hap Kibaha...
Watu wengi sana walifariki katika ajali ile kwani nusu ya juu ya basi ilimeguka kutoka kwenye bodi na kuwanchinja watu wengi..
Sababu ya ajali ilikuwa ni mwendo kasi kwani Air Msae ilikuwa inajaribu kulipita basi la Dar Express, lakini wakati wakiwa sambamba ghafla mbele yao upande ambao Msae lilikuwepo kukawa kuna lori linakuja...dereva wa Msae akaamua kulielekeza gari porini ili akwepe kugongana uso kwa uso...
 
nalikumbuka sana mkuu.

na ni gari ambalo familia yetu haiwezi kulisahau kamwe..

Kwenye ajali ya 1995 tulimpoteza mjomba wetu mpendwa, Jaspert..(R.I.P)..

mwaka 95 mwezi wa kumi hili basi lilipata ajali pale wami darajani liligongana na tayassar iliyokuwa ikitokea tanga, unazungumzia ajali hii?
 
mwaka 95 mwezi wa kumi hili basi lilipata ajali pale wami darajani liligongana na tayassar iliyokuwa ikitokea tanga, unazungumzia ajali hii?

exactly mkuu..yule aliyefariki pale ni mjomba wangu
CC, watu8
 
Last edited by a moderator:
katika hiyo ajari kuna dada mmoja tulisoma naye..naye alikuwemo bahati nzuri alipona...ila aliumia mguu..nalikumbuka sana hasa hiyo ajari ya 95
 
:angry::angry::angry::angry:.......MMILIKI WAKE ALIPISHANA NA SERIKALI KUHUSU MALIPO YAKE YA KUSAFIRISHA "WAPIGA KURA" KWENDA ZANZIBAR KUPITIA BAGAMOYO MWAKA ULEEE WA 1995....MIMI NILIMSIKIA MWENYEWE AKISEMA....SASA HIVI ANA MA YUTONG YANAENDA MTWARA

yanaitwaje? nisije panda yakawa mengine

maana niliapa siji panda gari za kampuni hiyo.,.
 
Hili ni basi lililokuwa maarufu sana miaka ya 90, na lilikuwa likifanya safari zake kati ya Arusha na Dar es Salaam.

302831_366282966809997_556338185_n.jpg

nahisi huyo jamaa wa pili toka myuma ndio alimpa ndugu yake yashika ampige picha akiwa kwenye basi huku anaigiza ananunua kitu
 
Siku hizi kuna PRINCESS MURO magari yake bomba; yanafika mpaka Musoma wacha Nairobi!!!
 
Hili jina linanitisha
Lilipata ajali likaua watu wengi sana kama sijasahau
 
Sio kweli Msae kwa sasa inaitwa Metro Coach...office zao ni pale karibu na Shoprite kamata. Kilimanjaro ni kitu tofauti mazee. Acha upotoshaji

Nakubaliana na wewe mkuu, Metro nilipanda kuna siku nikawa naiangalia vizuri tiketi kuna somewhere something like msae group... ila ana ma Youtong makali.
 
Back
Top Bottom