AIR MSAE: Mnalikumbuka hili basi?

AIR MSAE: Mnalikumbuka hili basi?

Watu8

Platinum Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
76,285
Reaction score
108,302
Hili ni basi lililokuwa maarufu sana miaka ya 90, na lilikuwa likifanya safari zake kati ya Arusha na Dar es Salaam.

302831_366282966809997_556338185_n.jpg
 
nalikumbuka sana mkuu.

na ni gari ambalo familia yetu haiwezi kulisahau kamwe..

Kwenye ajali ya 1995 tulimpoteza mjomba wetu mpendwa, ..(R.I.P)..
 
nalikumbuka sana mkuu.

na ni gari ambalo familia yetu haiwezi kulisahau kamwe..

Kwenye ajali ya 1995 tulimpoteza mjomba wetu mpendwa, Jaspert..(R.I.P)..

Hii kampuni baada ya kuwa chinja chinja wakabadili jina la kampuni kwasababu watu walikuwa wanayakimbia haya mabasi saizi wanajiita Kilimanjaro Express.ukipanda kilimanjaro ujue umepanda air masae
 
Umenikumbusha mbali mkuu enzi hizo Dar express ikiwa mbele lenyewe lipo nyuma ila umaarufu wake ulianza kupotea 2000 kabla ya 2003 kufutika kabisa. Alafu kwa kipindi kile lilikuwa linaonekana bonge ya bus ajabu sasa hivi kizazi cha Yutong au Marcopolo linaonekana kama ngalangala flani hivi
 
Hii kampuni baada ya kuwa chinja chinja wakabadili jina la kampuni kwasababu watu walikuwa wanayakimbia haya mabasi saizi wanajiita Kilimanjaro Express.ukipanda kilimanjaro ujue umepanda air masae

Kilimanjaro express ilikuwa Sawaya ambao nao walikuwa na mapungufu ya gari linaokoteza abiria pia mara mafuta yanakata likiwa njiani
 
Bila kusahau Masama, Mapande, na Royal smai,na Bedui,na Fresh ya shamba.duh kitambo!

Fresh ya shamba lilikuwa la VIP baadae likaja Royal Smai, ni vizuri kutunza picha aisee kuna kipindi zinakumbusha good memories ya enzi hizo na ndio maana hapa Mwanza kuna watu wanapiga picha kwenye round about ya samaki kuna watu wanawaona kama washamba ila baada ya miaka kadhaa pale pakiwa na kitu kingine inakuwa kumbukumbu nyingine nzuri
 
Hii kampuni baada ya kuwa chinja chinja wakabadili jina la kampuni kwasababu watu walikuwa wanayakimbia haya mabasi saizi wanajiita Kilimanjaro Express.ukipanda kilimanjaro ujue umepanda air masae

Sio kweli Msae kwa sasa inaitwa Metro Coach...office zao ni pale karibu na Shoprite kamata. Kilimanjaro ni kitu tofauti mazee. Acha upotoshaji
 
aiseeee babayangu naunga mkono hoja ni kweli kabisa

Kuna kipindi nilikuwa Tanga inabidi nisipande gari za Arusha zinazotokea Tanga napanda Hiace mpaka Segera nasubiri Dar express au Air Msae yalikuwa yanaondoka Dar saa 12 asubuhi Segera saa 3 kasoro mpaka kamili yanakuwa yanafika pale na ukilikosa unapata huzuni kabisa
 
Back
Top Bottom