Aina za udanganyifu kwa wapendanao au wanandoa

KikulachoChako

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
18,147
32,950
1. Kuwa na uhusiano wa kingono na mwingine (sexual cheating). Huu wengi mnaujua. Na ndio kiwango cha juu kabisa katika udanganyifu. Lakini zipo aina nyingine.

2. Kuficha mapato na matumizi (financial cheating). Ukiona mwenza anafichwa kipato na matumizi ujue kaanza udanganyifu. Mara nyingi anakuwa anatumia fedha kugharamia mwingine au anapokea fedha Kwa mtu mwingine. Na hataki ujue. Anaelekea kwenye sexual cheating kwa kasi.

3. Online cheating (udanganyifu wa kimtandao). Hapa anaanza kuficha password na akaunti zake. Hataki usome anachoandika au kuandikiwa. Ndio pale ukigusa simu yake anataka akuue. Akipokea simu anatembea mita 20 au anaingia chumbani ama anajibu "baadae" na kukata.

4. Kudanganya kihisia (emotional cheating). Mfano ni pale hisia zake anahamishia Kwa mtu mwingine. Anamhurumia mtu mwingine kuliko mwenza. Yuko tayari kumwambia mtu mwingine siri ambayo wewe hujui na Wala hataki uijue.

5. Kudanganya kupitia njozi (fantasy cheating). Mfano ni pale anaona mtu mtu , anasikia sauti ya mtu au anatizama video ya mtu anaanza kufikiria namna ya kumpata, nani angecheza naye shoo ya kibabe, n.k. Wengi hawajui huu ni udanganyifu. Siku akikutana na huyo aliye kwenye njozi ohoooo! Nina kisa cha Binti mmoja Togo ambaye alikuwa anamfanyia njozi Koredo Bello kale kaimbaji ka Naija. Hakakumaliza shule. Story siku nyingine .

6. Kupenda kitu kingine kupita kiasi (hobby cheating) . Mfano upende mpira kuliko mwenza. Au upende music kuliko mwenza. Utaanza kudanganya. Utaanza kutotumia muda mwingi na mwenza. Unaenda kutizama mpira utadai unaenda kutizama mgonjwa au kuna kazi ofisini jumapili.

7. Udanganyifu mguso (physical cheating). Mfano unajifariji nitambusu au kumkumbatia tu hatuta nani hii! Tatizo mkishakunbatiana au kubusiana mnakuwa mnakaribia kunanii. Ni suala la muda tu. Mwenzio akihoji mbona unamkumbatia mtu unaanza "lakini hatujananii" huku kichwani kuna kitu kinakwambia "ipo siku" aka "one day yes"!

Ukimuona mwenza mchunguze anadanganyaje? Usipojua style yake ya kudanganya utashindwa kumdhibiti.

Imeandaliwa na kuandikwa na
Yahya Msangi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom